Search This Blog

Tuesday, May 22, 2012

MERIK HAMSIK ANYOLEWA KIDUKU CHAKE BAADA YA NAPOLI KUWAFUNGA JUVENTUS

Napoli waliwafunga Juventus 2-0 katika fainali ya Coppa Italia na kuharibu msimu wa Juventus ambao walikuwa hawajafungwa na kuifanya siku ya mwisho ya De Piero akiwa ndani ya jezi ya Juve kuwa mbaya. Lakini kubwa kuliko siku hiyo, ni tukio la Merek Hamsik, ambaye alifunga bao la ushindi katika dakika ya 83 kuweza kutimiza ahadi yake aliyoitoa kwamba atanyoa nywele zake zote alizonyoa kwa mtindo wa kiduku.

Hamsik alihaidi ikiwa Napoli watabeba ndoo hiyo basi angenyoa nywele zake zote siku hiyo hiyo.

"Paolo Cannavaro na Christian Maggio walininyoa nywele zangu zote baada ya timu yetu kupata kombe. Ilikuwa ni ahadi niliyoitoa. Nilifanya hivi hata pale timu yangu ya taifa ya Slovakia ilipofuzu kushiriki kombe la dunia."

No comments:

Post a Comment