Search This Blog

Saturday, May 5, 2012

DIDA AGOMA KURUDI SIMBA KWA KUMUHOFIA JUMA KASEJA


LICHA ya kwamba Simba haikuwahi kuonyesha nia ya kumrejesha kipa namba moja wa Mtibwa Sugar, Deogratius Munishi 'Dida', kipa huyo ametamka kwamba hawezi kurejea Msimbazi kama Juma Kaseja atakuwapo klabuni hapo.

Dida, ambaye aliwahi kuichezea Simba na kukalia benchi kwa kipindi kirefu kabla ya kutemwa, alisema: "Hata kama Simba ikinihitaji sasa, kama Kaseja yupo sitakubali kuichezea. Ni kwa sababu ninajua nitaenda kukaa benchi.

"Najua siwezi kupata nafasi ya kucheza kutokana na uwezo wa Kaseja kwa sasa, lakini pia kwa jinsi anavyoaminiwa na Simba.

"Hakuna anayeweza kumwondoa Kaseja pale kwa sasa, kwanza yeye ni nahodha lazima acheze, kipa mwingine hatapata nafasi hadi Kaseja awe ameumia au awe amechoka kiuwezo, jambo ambalo kwa sasa si rahisi.

"Hivyo ndivyo ilivyo hata Ulaya, si umeona klabu kama Chelsea, Petr Cech au Iker Casillas wa Real Madrid, hao wakipata matatizo ndiyo wengine wataonekana."

Dida naye amecheza mechi zote za ligi isipokuwa mbili za mzunguko wa kwanza, alizosaidiwa na Hussein Sharif 'Casillas'.

Katika msimu huu wa Ligi Kuu Bara, Kaseja ndiye amedaka mechi zote, lakini pia ndiye amesimama katika lango katika mechi za kimataifa.
Hali iliyomfanya msaidizi wake, Ally Mustapha 'Barthez' kukalia benchi msimu mzima wa ligi.
  
www.mwanaspoti.co.tz

No comments:

Post a Comment