Search This Blog

Thursday, May 31, 2012

BARCELONA NA MADRID NA WAZO LA KUSHEA FAIDA YA HAKI ZA MATANGAZO YA TV NA VILABU VINGINE - ILI KUIFANYA LA LIGA IWE NA USHINDANI

Katika kuifanya ligi kuu ya Spain iwe ya ushindani serikali ya nchi hiyo imesema imeanza kuchukua hatua kadhaa moja wapo kuongea na giants wa soka nchini Hispania Real Madrid na Barcelona ambao wanaweza wakawa tayari kushea faida ya haki za matangazo ya Televison miongoni mwa vilabu vya La Liga, kwa mujibu wa Waziri wa Michezo wa nchi hiyo.

Jose Ignacio Wert alisema: "Naamini kwamba Madrid na Barcelona wapo tayari kuweza kushea mapato yatokanayo na kuuza haki za matangazo ya TV.

Vilabu kwenye La Liga huwa vina utaratibu wa kuongea kila mmoja kimpango wake na wamiliki wa TV, tofauti na  ligi nyingine barani ulaya ambazo zina mfumo wa kuungana kwenye suala la haki za  matangazo ya TV. Real na Barca wanapata nusu ya mapato yote yatokanayo na kuuza haki za matangazo ya mechi - nusu ya £511million.

Utafiti uliotoka mwezi April na chuo kikuu cha Barcelona, ulionyesha kwamba kwenye msimu wa 2010-11 Barca walipata kiasi cha £130 kutokana na haki za matangazo ya TV, Madrid walipata £124million huku Valencia wakipata £33.5million.

Pengo hili hili kubwa la mapato ndio linalochangia ligi kuu ya Spain kutokuwa na ushindani huku vilabu hivi vikubwa vikiwa vina msuli mkubwa wa fedha ukilinganisha na timu nyingine.
 Msimu Valencia wameshika nafasi ya tatu nyuma kwa pointi 30 dhidi ya Barcelona walioshika nafasi ya pili, na pointi 39 nyuma ya mabingwa Real Madrid.

Kuanza kutumia mfumo wa umoja kwenye kupata haki za matangazo ya TV, ambao unatumiwa na vilabu vya ligi kuu ya England kutapunguza na kuzuia vilabu vya La liga kuwa na madeni makubwa.

Vilabu vya Spain kwa ujumla vina madeni yanayofikia £2.7billion mpaka msimu wa 2010-11.
 

No comments:

Post a Comment