Mchezaji wa Yanga Haruna Niyonzima akikokota mpira mbele ya beki wa timu ya Polisi Dodoma Idd Ramadhan wakati wa mchezo wao wa ligi kuu ya Vodacom unaofanyika kwenye uwanja wa Taifa jioni hii, mpaka sasa ni kipindi cha pili na yanga imefanikiwa kuongoza katika vipindi vyote baada ya kupata magoli matatu kupitia kwa wachezaji wake Davis Mwape magoli mawili na Idrisa R.Senga goli moja na sasa inaongoza 3-0 dhidi ya Polisi Dodoma .
Wachezaji wa Yanga na Polisi Dodoma wakipeana mikono kama ishara ya kusalimiana kabla ya kuanza kwa mchezo huo kwenye uwanja wa Taifa jioni hii.
Leo mashabiki wa Yanga wamejitokeza kwa uchache katika uwanja wa taifa, huenda hii inatokana na mwenendo wa timu hiyo katika michezo yake ya hivi karibun, ambapo imepoteza matumaini ya kuchukua ubungwa na hata nafasi ya pili, Yanga ndiyo walikuwa mabingwa watetezi wa kombe la ligi kuu ya Vodacom walilochukua mwaka jana.
MABAO YA YANGA KWENYE MCHEZO WA LEO YAMEFUNGWA NA DAVIS MWAPE ( 2 ) NA IDRISSA RASHID.
No comments:
Post a Comment