Search This Blog

Monday, April 23, 2012

UPEPO UMEBADILIKA: UNITED WAMEWEKA UBINGWA REHANI - DERBY KUAMUA BINGWA - FERGUSON ASEMA ITAKUWA MECHI YAKE MUHIMU KULIKO ZOTE KATIKA MAISHA YAKE.


Hatimaye zimebakia pointi 3 tu zinazowatenganisha mahasimu wawili katika kuelekea mwishoni mwa mbio za ubingwa wa ligi kuu ya England.  Jambo hili linaufanya mchezo wa jumatatu ijayo uwe mtamu zaidi katika historia ya upinzani kati ya Manchester United na Manchester City.

Kiukweli hivi sasa Roberto Mancini hawezi tena kujifanyisha kwamba City hawana nafasi ya kubeba taji na usiku huu muitaliano huyo atakuwa akigongesha glass na Stevn Pienaar huku akiwa na mawazo ya Manchester Derby jumatatu ijayo.

Siku zote ilikuwa ikionekana kwamba mchezo huu wa jumatatu ya tarehe 30 ndio utaamua ubingwa pamoja na mabadiliko ya mapishano ya pointi katika mbio hizi ambazo tangu mwanzoni mwa msimu zimekuwa zikiongozwa na vilabu hivi vya Manchester.

City wataenda katika mchezo huo pale Etihad Stadium wakijua kwamba ushindi wa mara 3 katika michezo yao ya mwisho utakuwa unatosha sana kuwafanya wawe mabingwa wa premier league kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 44. Wana wastani mzuri wa magoli dhidi ya majirani zao - tofauti ya magoli 6 - kwa maana watakuwa on top hata kama watafungana pointi na United mwishoni mwa msimu.

Haikuwa ikionekana mambo yatakuwa hivi wakati zikiwa zimebaki dakika 7 za kucheza pale Old Trafford leo jumapili na United wakiongoza 4-2 dhidi ya Everton. Kwa muda huo, Sir Alex Ferguson inawezekana alikuwa akifikiria namna ya kwenda kubeba ubingwa pale pale nyumbani kwa majirani zake wapiga kelele kama anavyowaita.

Lakini magoli mawili kutoka Nikica Jelavic na Pienaar yalibadilisha kila kitu, na mbio za ubingwa, matokeo yakawa 4-4 katika ubao wa matokeo mwishoni mwa mchezo na kuwarudisha City katika mbio hizo ambazo zilionekana zinakaribia kuisha.

Wakati City walipofungwa na Arsenal April 8, walikuwa nyuma kwa pointi 8 nyuma ya United huku ikiwa imebakia michezo 6 ya kucheza. Maswali yalielekezwa kwa Mancini na hatma yake wakati baadhi ya mashabiki wa United walitengeneza t-shirts za kusherekea ubingwa wa 20.

Wiki 6 kabla ya kuisha kwa msimu, kila mtu alidhani muda ulikuwa bado, lakini hakuna aliyefikiri wala kutegemea United wataachia mahasimu wao kurudi katika mbio za ubingwa kirahisi hivyo. City walicheza vizuri na kuutumia udhaifu na makosa ya United leo na kuwafunga Wolves na kubakisha pointi 3 kabla ya derby yao pale Etihad.

"Tumewapa City dhumuni la kupigana zaidi, hakuna mashaka juu ya hilo. Makosa yetu ya leo yameufanya mchezo wa Etihad kuwa derby muhimu zaidi katika maisha yangu hapa Old Trafford. Mechi itaamua kila kitu. Tumejitengenezea mazingira magumu wenyewe - lakini tutaenda pale kwao tukiwa tunajua tuna uwezo wa kupata matokeo mazuri dhidi yao." - Alikaririwa Ferguson leo baada ya mechi.

Ama kwa hakika sasa mambo yamegeuka, na derby ya manchester itakuwa vita kubwa kuliko zote ambazo timu hizi mbili zimewahi kupigana. City watamkosa kiungo wao na roho ya safu ya kiungo Yaya Toure ambaye leo amepata kadi ya njano ya tano hivyo ataukosa mchezo. Hii itakuwa derby itakayofanana na El Clasico ya jana.
Ukiachana na Derby - City wamebakisha mechi dhid ya Newcastle @Sports Direct Arena na watamaliza dhidi ya QPR pale Etihad Stadium. Huku United wenyewe wakiwa wamebakia na mchezo dhidi ya Swansea City pale Old Trafford na watamaliza ugenini  dhidi ya Sunderland.
 

No comments:

Post a Comment