Search This Blog

Friday, April 27, 2012

TITO VILANOVA KOCHA MPYA WA BARCA: RAFIKI WA GUARDIOLA TANGU UTOTO - ADUI WA MOURINHO UKUBWANI

Pamoja na Barcelona kuvunja rekodi ya mafanikio chini ya Pep Guardiola katika miaka minne iliyopita - akiiongoza timu hiyo kubeba jumala ya makombe 13 - msaidizi wake mkuu Tito Vilanova amekuwa mara nyingi hazungumziwi.
Mpaka leo, pindi kocha huyu mwenye miaka 42 alipoushangaza ulimwengu wa soka baada ya kuthibitishwa kwamba ndiye kocha atakayemrithi Guardiola na kuliongoza benchi la ufundi la Barcelona katika msimu ujao wa 2012-13.

Alizaliwa katika ukanda wa Catalan eneo la Bellcaire d'Emporda mwaka 1969, Vilanova amekuwa mtu wa karibu sana na kocha huyu wa sasa Blaugrana kwa wakati wote. Wawili hawa wamekuwa pamoja katika kituo cha La Masia katika miaka 1980s. Lakini wakati Guardiola alipoenda na kuwa star katika kikosi cha Johan Cruyff -Dream Team - wakishinda makombe sita ya La Liga na moja la Ulaya katika miaka 11 - Vilanova alishindwa kuhitimu, na miaka miwili baada ya kukaa na kikosi cha Barcelona aliamua kuondoka na kwenda kucheza katika timu za Figueres, Celta Vigo, Badajoz, Mollorca, Lleida, Elche na Gramenet - ambapo aliamua kustaafu mwaka 2002, miaka 14 baada ya kuanza kucheza katika evel ya juu.

Vilanova baadae akaamua kuhamia katika ukocha. Experience kubwa zaidi ni pale alipokuwa mjurugenzi mkuu wa klabu ya daraja la 3 kuanzia mwaka 2006-07. Baadae akaamua kurudi Barcelona wakati kiangazi cha 2007 kama kocha msaidizi wa kikosicha Barca B chini ya Pep Guardiola.
Wakati Guardiola alipomrithi Frank Rijkaard mwaka 2008, Vilanova alijiunga na Guardiola katika kikosi cha kwanza na kuwa kocha msaidizi katika kikosi cha kwanza cha Barcelona.




Mourinho na Vilanova wakizinguana

Tukio kubwa ambalo lilimuhusisha msaidizi wa Guardiola lilitokea mwezi wa nane tarehe 18 mwaka 2011 katika muda wa nyingeza wa mechi ya Supercopa mechi ya pili kati ya Barcelona na Real Madrid pale Nou Camp. Rafu ya kijinga ya Marcelo dhidi ya Cesc Fabregas ilizusha ugomvi mkubwa katika timu zote mbili, na mwishowe Jose Mourinho akamtia kidole cha jicho Vilanova - kitendo ambacho kiliripotiwa sana na vyombo vya habari vya Hispania.
 Kwa mujibu wa mkurugenzi wa ufundi wa Barcelona Andoni Zubizarreta, uteuzi wa Vilanova kama mrithi wa Guardiola ni sahihi kabisa kwa sababu ni watu wanaoshea mawazo na mbinu za kimchezo pamoja na staili ya kucheza yenye filosofi moja.

Lakini baada ya makombe 13 - au 14 ikiwa Barca watashinda Copa del Rey mwezi ujao - ndani ya miaka 4, Vilanova ana kazi ngumu sana ya kufuata nyayo za rafiki yake kipenzi.

3 comments:

  1. Guardiola anastahili pongezi kubwa sana. Miaka minne makombe 13/14 si mchezo ati.

    ReplyDelete
  2. itakuwa jambo la maana sana kama atakuja chelsea angalau tupate vikombe. kabati letu la vikombe linatia aibu hata panya hawakai??

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hapana,bwana! Aje kwetu Anfield. Kidogo Chelsea mulipata chochote enzi za Maurinho. Sisi Liverpool ni juzi tu, baada ya miaka mingi, tumepata kikombe ambacho hakina maana yoyote England mpaka ManU, Arsenal, Chelsea, nk wanachezesha vikosi vya pili.

      Delete