Search This Blog

Thursday, April 12, 2012

RENE MEULENSTEEN - FERGIE ANAVUTIWA SANA NA EDEN HAZARD


Kocha wa kikosi cha kwanza cha Manchester United Rene Meulensteen amemsifu kiungo mshambuliaji wa Lille Eden Hazard akisema ni "ana kipaji maalum" huku klabu yake ikijipanga kutuma bid kwa ajili ya mbelgiji.

United wanafahamika kuwa wamekuwa wakivutiwa na Eden, 21, na Sir Alex Ferguson alienda kumuangalia nchini Ufaransa mwezi uliopita katika mechi dhidi ya Lyon.

"Manager alitaka kumuona Hazard," Meulensteen aliiambia Voetball International. "Hiyo inaonyesha ni kiasi gani anavutiwa naye, mimi na Fergie tumekuwa tukimuongelea sana  Hazard.

"Ni muhimu kwa klabu kuwa inabadilisha wachezaji inapotokea umuhimu wa kufanya hivyo. Hazard ana kipaji cha juu, lakini ili kujua kwa uhakika kama anafaa inachukua muda kidogo. Kwa mfano, tulikuwa tunamfuatilia David De Gea kwa muda mrefu sana kabla hatujamsaini.



"Ferguson anapenda kujua character ya mchezaji, na kwa sababu hiyo ndio maana alienda kumuangalia mwenyewe. Hazard ndio moyo ya timu ya Lille na Fergia alitaka kuona macho yake kipaji cha kinda huyu."

Ikiwa United wataamua kutuma ofa kumsajili kinda huyo ni dhahiri watakutana na upinzani mkubwa kutoka kwa mahasimu wao Man citu pamoja na Bayern Munich.

No comments:

Post a Comment