Search This Blog

Thursday, April 19, 2012

RAUL: NAONDOKA SCHALKE SIONGEZI MKATABA

BYE BYE BYE
Mshambuliaji wa kihispania Raul Gonzalez Blanco hatoongeza mkataba wake na Schalke na ataondoka mwsihoni mwa msimu. klabu hiyo ya Bundesliga imetangaza.

Taarifa iliyotolewa na klabu ya Gelsenkirchen kupitia webiste yao imethibitisha kuwamba Raul, 34, ambaye alijiunga na tiu hiyo akitokea Real Madrid miaka miwili iliyopita, ameamua kutoendelea kuichezea timu hiyo.



Mshambuliaji huyo amesema atatoa sababu zake katika mkutano wake na waandishi wa habari mjini Gelsenkirchen jioni hii. Raul kwa haraka zaidi aliweza kuteka mioyo ya mashabiki wa Schalke baada ya kufunga magoli 13 katika msimu wake wa kwanza, zikiwemo hat tricks mbili.

Na msimu huu tayari ameshatupia kambani magoli 14 na kuwasogeza The Royal Blues kukaribia kupata nafasi ya kushiriki Champions league msimu ujao, lakini baada ya miezi mitatu ya tetesi sasa Raul ameamua kuondoka katika klabu hiyo.

No comments:

Post a Comment