Search This Blog

Friday, March 2, 2012

WAPINZANI WA SIMBA KUWASILI KESHO


Wapinzani wa vinara wa Ligi kuu ya Vodacom Simba SC katika michuano wa kombe la shirikisho CAF, Kiyovu SC wanataraji kuwasili kesho badala ya leo.

Kiyovu ilitarajiwa kuwasili leo jioni lakini kutokana na kukosa ndege watakuja nchini kesho kwa ajili ya mchezo wa marejeano, utakao chezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Katika mchezo wa awali uliochezwa katika jiji la Kigali ulimalizika kwa timu zote kutoka sare ya goli 1-1. Goli la Simba likifungwa na Mwinyi Kazimoto.

Katika hatua nyingine Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi anatarajiwa kuwasili nchini kesho na kujiunga na kambi ya Simba moja kwa moja. Okwi alikuwa na timu ya taifa ya Uganda iliyofungwa goli 3-1 na Congo.

Wakati huo huo Mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga wamewasili salama jijini Cairo, kwa ajili ya mchezo wa marejeano dhidi ya Zamalek, mchezo utakao chezwa katika uwanja wa jeshi bila ya mashabiki.

Vilevile na Jamhuri ya Pemba nayo iliwasili salama nchini Zimbabwe, ambapo wanataraji kucheza na Hwange ya Zimbabwe, baada ya kuchapwa goli 3 katika mchezo wa awali wa kombe la shirikisho CAF uliochezwa katika uwanja wa Gombani.

Wawakilishi wengine wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mafunzo FC wao watasafiri machi 7 kwenda Msumbiji kwa ajili ya mchezo wa marejeano.


No comments:

Post a Comment