Search This Blog

Thursday, March 15, 2012

TBL yaidhamini Taifa Stars miaka mitano kwa Sh. 15bil


LAMPS COLLIN
KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) imemwaga zaidi ya Shilingi 15 bilioni kuidhamini timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kwa muda wa miaka mitano.

Habari za uhakika kutoka vyanzo vyetu vya habari, zinasema kuwa siku chache zijazo TBL na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) watasaini mkataba huo mkubwa na aina yake kuwahi kutokea nchini.

Taifa Stars ipo katika mechi za kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika Afrika Kusini mwakani huku pia ikijiandaa kwa michuano ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil mwaka 2014.

Habari za uhakika zinasema kuwa TBL imekubali kuidhamini Taifa Stars kwa Shilingi tatu bilioni kila mwaka hivyo kwa miaka mitano itakuwa Sh.15 bilioni.

Huu utakuwa ni udhamini mkubwa zaidi kuwahi kutokea katika historia ya soka nchini.

Hakuna upande uliokuwa tayari kuzungumzia suala hilo kwani pande zote zinataka kufanya hafla ya nguvu wakati wa kusaini mkataba huo mbele ya vyombo vya habari.

Siku chache zilizopita TFF ilitangaza kuwa haitaongeza mkataba na wadhamini wao wa zamani Kampuni ya Bia Serengeti (SBL) ambao kwa miaka mitano walioidhamini Taifa Stars kulikuwa na msisimko mkubwa wa soka.
Source: mwanaspoti.co.tz

1 comment:

  1. Fedha nyingi lakini zinaishia kwenye matumbo yao tu na hatuoni maendeleo yoyote ya soka. Chakushangaza hata hizo program zilizokuwepo za kuendeleza soka la vijana zimekufa.
    Sijui kwanini wadhamini wanaendelea kudhamini kitu kisicho na muonekano wa maendeleo zaidi ya manufaa kwa wachache tu..Kwanini wasidhamini michezo mengine? Au kwanini wasidhamini wadau au taasisi zinazokuza vipaji badala ya hii TFF? Au na wao wanapata % fulani nini?..

    Bebeto.

    ReplyDelete