1.Nafasi ya Balotelli iko hatarini baada ya kurejea kwa Carlos Tevez.
Mario Balotelli anaweza kuwa amefunga mabao 15 kwenye michezo 29 ya Man City kwenye ligi msimu huu huku Sergio Aguerro akiwa amefunga mabao 24 kwenye michezo 41 ya mchuano mbalimbali huku Carlos Tevez akiwa hajafunga bao lolote msimu huu baada ya kukaa nje kwa miezi sita . Kwa takwimu kama hizi , Mancini kwa vyovyote atakuwa na imani kuwa wachezaji hawa wanaweza kuipa City ubingwa wa wa EPL . Tatizo la dhana hii ni mwamba Mario Balotelli hucheza kama homa za vipindi , kuna wakati homa inapanda wakati mwingine inashuka . Balotelli alipata nafasi ya kuipa City bao la kuongoza huku Tevez akiwa anapasha nje ya uwanja lakini Balotelli alikosa umakini na kutoa mpira nje .Alipoingia Tevez hali ilikuwa tofauti na alitengeneza bao lililoipa City pointi zote tatu . Dhana kubwa iliyoko hapa ni kwamba kuelekea mwishoni mwa msimu kuna uwezekano mkubwa kwamba nafasi ya Balotelli ikawa Hatarini kutokana na kurejea kwa Carlos Tevez hasa ukipiga mahesabu ya dakika 45 alizocheza Balotelli bila msaada na dakika chache alizocheza Tevez na kurejesha matumaini ya City kutwaa ubingwa .
2.Torres kucheza mechi nyingi kuliko Drogba .
Taarifa za vyombo vya habari vya England jana zilisema kuwa Fernando Torres angeanzia benchi lakini kufikia wakati wa mechi haikuwa hivyo . Torres alianza na Drogba alisubiri benchi. Pamoja na kutofunga Torres alifanya kazi kubwa sana ya kuwapa tabu mabeki wa man City hali iliyowafanya City kushindwa kuingia kwenye eneo la hatari mara nyingi hasa kwenye kipindi cha pili . Roberto Di Matteo alifanya kosa ambalo hakika atakuwa amelijutia katika maisha yake mafupi kama kocha wa muda wa Chelsea nalo ni kumbadilisha Didier Drogba kuingia nafasi ya Torres . Hapa ndipo Chelsea waliiruhusu City kurudi mchezoni kwani mabeki wa City walrelax na kuwa wanaanzisha mashambulizi kwa wepesi na baada ya hapo City walipata mabao mawili na pointi tatu muhimu . Kimsingi Di Matteo kama mtu ambaye anaufahamu vyema mchezo wa soka atakuwa amegundua kosa alilofanya na kwa sababu hiyo nafasi ya Torres kwenye kikosi cha kwanza itakuwa ya uhakika zaidi.
3.Matumaini ya ubingwa wa EPL kwa City bado yako hai.
Kabla ya mchezo wa jana Mancini alizungumza na waandishi wa habari na aliwaambia kuwa wanaenda Etihad kuendeleza mapambano ya kutwaa ubingwa EPL na baada ya dakika 90 walidhihirisha kuwa hawajakata tama na matumaini ya kutimiza lengo lao bado yako hai.Zikiwa zimesalia mechi dhidi ya timu kama Arsenal , Newcastle United na nyinginezo bado City wanaiona nafasi ya ubingwa kuwa ya kwao na endapo wataifunga United kwenye mchezo wao utakaopigwa Aprili 30 hakika ubingwa utakuwa wa kwao.
4.Matumaini ya Chelsea kufuzu Ligi ya mabingwa barani ulaya yako Hatarini.
Moja ya mambo ambayo wengi wamezungumza kuhusu ligi kuu ya England ni jinsi Man United walivyo na faida ya ratiba nyepesi ya mechi tofauti na Man City . Hata hivyo kama kuna timu ina wakati mgumu ni Chelsea . Ugumu wa kampeni ya Chelsea unadhihirika kwenye nafasi waliyopo ambayo inawaweka hatarini kuikosa michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya . Kwa sasa Chelsea wanashika nafasi ya tano nyuma ya Tottenham na Arsenal pamoja na michezo mingine migumu dhidi ya Liverpool , QPR,Aston Villa, Newcastle United na hata Blackburn Rovers . Ugumu huu unaongezeka kwenye ukweli kuwa bado Chelsea ina michezo dhidi ya timu hizi na kwa ishara zilizoonekana jana kwenye mchezo wao dhidi ya City nafasi yao ya kufanya vizuri kwenye michezo hiyo ni finyu sana .
5. Nafasi ya Roberto Di Matteo kama kocha wa muda mrefu Chelsea.
Pamoja na ukweli kuwa hajaweka wazi dhamira yake , kila mtu anajua kuwa Roberto Di mtatteo angependa kupewa nafasi ya kuifundisha Chelsea kwa muda mrefu zaidi . Hata hivyo baadhi ya makosa ya kimaamuzi aliyoyafanya jana hasa kwenye mabadiliko aliyoyafanya kwa Torres na Didier Drogba yameonyesha udhaifu mkubwa wa kuusoma mchezo na kujua unahitaji mabadiliko ya aina gani . Kinachotofautisha kocha mkubwa na mdogo ni maamuzi kama haya na hili ni jambo ambalo Roman Abramovich atalitazama kwa umakini.

BALOTTELI ANAWEZA AKAKOSA NAFASI KWENYE NAMBA YA CLUB
ReplyDeleteAcha kujifanya unajua sana jana Torres was nothing zaidi ya kuruka ruka tu uwanjani. City kuanzia dakika ya kwanza ya kipindi cha pili walipiga kambi kwenye half ya Chelsea na sio baada ya Torres kutoka.
ReplyDeleteAcheni kumtetea Torres kwani ameshapewa nafasi nyingi sana lakini wapi. A proper striker does not need all that time to show his skills. He is just another Shevchenko!!