Search This Blog

Thursday, March 15, 2012

CHISORA ANYANG'ANYWA LESENI.

Kwenye masumbwi Bondia mzaliwa wa Zimbabwe Mwenye uraia wa Uingereza Derek Chisora amenyang'anywa leseni Yake kwenye Mchezo wa masumbwi ikiwa ni adhabu ya bodi ya Mchezo huo kwa chisora kufuatia vitendo vya utovu wa nidhamu Alivyoonyesha chisora kabla na Baada ya pambano Kati Yake na Bondia toka Ukraine Vitaly Klitschko.

Taarifa iliyonukuliwa kwenye barua aliyoandikiwa Chisora juu ya adhabu hiyo imesema kuwa Derekc Chisora hayuko kwenye Hali sahihi a kiakili anayotakiwa kuwa nayo mtu aliyeaminiwa kuwa na leseni a Mchezo wa masumbwi.

Bodi hiyo imeweka wazi milango ya rufaa kwa Chisora na amepewa siku 14 za Kufanya hivyo endapo atahisi Kutoridhishwa na adhabu aliyopewa. Derek Chisora Alimpiga kofi mpinzani wake wakati wa hafla ya kupimwa uzito na alienda mbali zaidi pale alipomtemea mate Usoni mdogo wa Vitali  vladmir na Kali kuliko zote ilikuwa Ugomvi Kati Yake na aliyekuwa Bondia wa uzito wa juu ambaye kwa sasa amestaafu Mchezo huo David Haye kwenye mkutano wa waandishi wa habari Baada ya pambano lake dhidi ya Vitaly Klitschko huko Munich.

No comments:

Post a Comment