Search This Blog

Thursday, February 9, 2012

WATAKAOTHIRIKA NA WATAKAOFAIDIKA NA KUONDOKA KWA FABIO CAPELLO KATIKA KIKOSI CHA ENGLAND






Fabio Capello alijiuzulu ukocha wa England jana, baada ya kufanya mazungumzo makali dhidi ya FA juu ya chama hicho cha soka kumvua unahodha John Terry.
FA walimnyang’anya kitambaa cha unahodha mlinzi wa Chelsea kutokana na kesi ya ubaguzi wa maneno ya ubaguzi dhidi ya Anton Ferdinand.

Capello aliamua kwenda hadharani na kuuponda uamuzi wa FA, na kwa haraka aliitwa na mwenyekiti wa FA David Bernstein @Wembley Stadium.
Baada ya mkutano huo ilitangazwa kwamba FA imekubali uamuzi wa Capello kujiuzulu.
Maamuzi ya kujiuzulu kwa Fabio Capello yameacha majeruhi kwa baadhi ya watu huku wengine wakiwa  na furaha tupu.
Sasa tuangalia watu waliothirika na waliofaidika na uamuzi wa Fabio Capello.

ALIYEATHIRIKA: JOHN TERRY
Fabio Capello alikuwa anamuona John Terry kama kiongozi asilia katika timu yake, na maoni yake kupitia television ya Italia yalionyesha dhahiri kuwa kesi ya ubaguzi inayomkabili Terry haikubadili chochote kuhusu anavyomchukulia Nahodha huyo wa Chelsea.
Sasa Capello akiwa hayupo kwenye picha, kuna wasiwasi mkubwa kwamba kocha ajaye anaweza asiwe na mtazamo kama wa Capello kuhusu Terry.
Pia anaweza asimuite kabisa Terry katika kikosi cha England, akizingatia hali inavyoweza kuwa mbaya katika dressing room ya Three Lions. Uwepo wa John Terry unaweza kuleta hali ya kutokuwepo kwa umoja na mshikamano.
Hivyo John Terry anakosa mtu wa kumtetea kutokana na kuondoka kwa Capello – Ameathirika.


ALIYEFAIDIKA: HARRY REDKNAPP
Bila shaka Harry Redknapp ndio chaguo la watu wengi katika mchakato wa kumpata mrithi wa Capello na kuna asilimia kubwa anawza akawa ndiye kocha ajaye wa England.
Hali imekuwepo siku zote, lakini sasa hata baadhi ya wachezaji wa sasa na zamani na makocha kama Wayne Rooney,  Martin Oneill, Gazza, Rio Ferdinand, Gary Lineker wamekuwa wamkitaja Redknapp kama chaguo sahihi la nafasi ya ukocha wa England.
Harry Redknapp amefaidika na kuondoka kwa Capello.


WALIOTHIRIKA: CHAMA CHA SOKA ENGLAND – FA
FA walikuwa wakimlipa Fabio Capello £6million kwa mwaka kwa kuiongoza England, na kiukweli Capello hakufanya jambo lolote la kukumbukwa katika timu hiyo.
Walipata nafasi ya kucheza kombe la dunia 2010, lakini England walienda South Africa na kufanya madudu.

Capello pia aliiongoza England kupata nafasi ya EURO 2012, lakini matumaini ya kufanya vizuri katika michuano hiyo madogo mno.

Japokuwa hakufanya vibaya sana, lakini matokeo ya World Cup 2010 yanaficha mazuri yote ya wakati wa utawala wake.
Kwa fedha aliyokuwa akilipwa iliyomfanya kuwa kocha anayelipwa zaidi ulimwenguni na mambo aliyoifanyia England – FA wamepata hasara kubwa.


WALIOFAIDIKA: MEDIA
Ni fair kusema kwamba vyombo vya habari vya Uingereza havikuwa na mapenzi na Capello.
Pia ni sawa kusema vita yao au mapmbano yao ya kuona muingereza Harry Redknapp anakuwa manager mpya wa England karibia inaanza kufanikiwa kwa kuwa watapata kazi rahisi zaidi kufanya coverage ya matukio ya timu ya taifa.

Pia waandishi wa habari wa England wanakaribia kufanikisha adhma yao ya kumuweka kocha raia wa Uingereza kuwa kiongozi wa benchi la ufundi la England.

Pia kikubwa zaidi kwa media, kuondoka kwa Capello kutauuza sana habari zao, kwa kuwa watu wengi watakuwa wakisubiri kupitia vyombo vya habari tangazo la nani atakuwa kocha mpya.
Kuondoka kwa Fabio Capello ni ushindi kwa vyombo vya habari vya England.


WALIOTHIRIKA: TOTTENHAM HOTSPUR?
Mashabikiw wa Spurs siku zote walikuwa wanajua huu wakati unakuja. Harry Redknapp amekuwa mwokozi wao katika misimu ya hivi karibuni, ikiirudisha Spurs katika kushindana na vilabu vikubwa na kuleta matumaini mapya ya makombe @White Hart Lane.

Kama atapewa ukocha wa England, kiukweli Spurs wataathirika. Kocha mpya kwao anaweza asiwe na ushawishi wa kuwazuia Gareth Bale, Van Der Vaart na Luka Modric kubaki London ya kaskazini.
Kama ikiwa Redknapp atapewa jukumu la ukocha wa England, at least mashabiki wa Spurs wataomba apewe option la kumalizia kwanza msimu huu huku akiwa kocha England mpaka utakapoisha msimu wa EPL 2011-12.

No comments:

Post a Comment