Search This Blog

Friday, February 24, 2012

VIINGILIO STARS VS MSUMBIJI


Kiingilio cha chini katika mechi ya mchujo ya Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Msumbiji (Mambas) itakayochezwa Februari 29 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 3,000.
 
Jumla viti 36,693 (rangi ya bluu na kijani) ndivyo vitakavyotumika kwa kiingilio hicho katika uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 60,000 wakiwa wameketi.  
 
Viingilio vingine ni sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 10,000 kwa VIP C, sh. 15,000 kwa VIP B wakati kwa watakaokuwa miongoni mwa watakaokaa katika viti VIP A ambavyo viko 748 tu watalazimika kulipa sh. 20,000 kwa kila mmoja.
 
Tiketi zitaanza kuuzwa siku moja kabla ya mchezo katika vituo vya Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Kituo cha mafuta cha Bigbon kilichopo Msimbazi (Kariakoo), mgahawa wa Steers ulioko Barabara ya Samora/Ohio, Kituo cha mafuta cha Oilcom Ubungo na Uwanja wa Taifa.
 

1 comment:

  1. Mimi ni mdau na mfuatiliaji mzuri sana wa blog hii pamoja na kipindi cha Sportsbar cha Clouds Tv,nampongeza sana bwana shaffih dauda kwa program zote mbili ila namshauri yeye pamoja na waandaaji wenzie wa sports bar wasionyeshe dhahiri ushabiki wa timu wanazozisapoti kwani ni kinyume na taaluma zao,tukio kubwa katika soka weekend hii ni fainali ya carling cup kati ya Liverpool na Cardiff city ambapo ilimalizika kwa Liverpool kuchukua Ubingwa huo,cha kushangaza kwenye kipindi cha jana 27/02/2012 cha sportsbar haikuzungumziwa hata kidogo na badala yake wakakaa kujadili mechi ya Man U na Norwich ambayo ilikua ni mechi ndogo na isiyo na msisimko kwa weekend hii,Acheni ubaguzi kwani hiyo sio Manchester au Arsernal Tv bali ni Clouds Tv,Badilikeni!!!!!!!

    ReplyDelete