Search This Blog

Thursday, February 16, 2012

TUNAHITAJI VIJANA KUENDELEZA SOKA LETU

Na Simon Chimbo
Hapo zamani vijana walichukuliwa na jamii kanakwamba hawajui kitu na
tena ni 'wahuni' hivyo hawawezi kuongoza. Lakini hebu twende katika
siasa kidogo, ni nani hazijui changamoto kutoka kwa wabunge vijana
Pale mjengoni kwa Makinda? watu kama akina Kabwe, Mnyika, Kafulila na
wengine vijana wengi wamekua mstari wa mbele kutetea na kuleta
changamoto katika suala zima la siasa, hebu tuachane na huko na turudi
katika soka letu la bongo.
Hatuwezi kufikia mafanikio ya Zambia 'mabingwa wa AFCON 2012' kama
hatutofanya mabadiliko ya kusudi katika uongozi wa mpira wa miguu
'soka'. Sijasema wazee hawawezi kuongoza na kufikia mafanikio, La
hasha! Lakini twende mbele turudi nyuma, ni lazima uwe na malengo
(objectives) katika kutimiza azma fulani. Waswahili wanasema katikati
ya ukweli, uongo  hujitenga, hivi ni nani anaamini au kayaona malengo
(objectives) ya TFF na maendeleo ya soka letu? Jibu mnalo.
Mwaka 2006 wakati mbrazili Marcio Maximo akitua nchini alisema maneno
yafuatayo, NANUKUU,"while we're refining stars, we should progress
youth soccer." mwisho wa kunukuu, Maximo alieleza kua ili kujenga
ubora wa stars ni lazima tuendeleze soka ya vijana, nani alimsikia?
Jibu unalo.
Katika kumbi mbali mbali za kuoneshea mpira, nilikua nikisikia
'wabongo' wengi wakisema "dah, natamani Zambia ingekua Stars"..."hivi
Tanzania tuna matatizo gani?" n.k n.k n.k Mie naongeza yangu, "hivi
Zambia waweze wana nini na sisi tushindwe tuna nini?" Bila program
endelevu hatuwezi fikia malengo, AFCON, world cup vyote tutaendelea
kuwasifia wenzetu akina Ghana na Zambia. Wakati umefika kwa vijana
kushika hatamu za uongozi ili kuleta changaoto kama zile za pale
mjengoni kwa Makinda, tunawahitaji akina Kabwe katika soka ili nasi
siku moja  tuwe kama Zambia na Ghana.. Vijana mnaweza jitokezeni.

1 comment:

  1. Unachokisema ni kweli . lakini nahisi haukwenda mbali zaidi katika kutuelezea ni nn kilichokwamisha tusifikie hatua ya zambia na ghana.

    Pia nini tufanye kupata pesa za kusaidia vijana hao unaowasema .(kuhusu pesa chukua mfano wa club ka yanga sc kushindwa kulipia fedha za hoteli mjini Arusha), Je vijana hao wataweza?

    Pia umesahau kuwa soka letu sasa limeingiliwa na usiasa ndani yake.
    mfano wewe nakunukuu "Vijana mnaweza jitokezeni".! WAPI?

    Much respect Bro , "Bado nimefulia"

    ReplyDelete