Search This Blog

Friday, February 24, 2012

SIMBA NA AZAM KUCHUANA CHAMAZI WIKIENDI HII



Kikosi cha Simba kinataraji kushuka dimbani kesho kuvaana na Azam Fc katika mchezo wa kirafiki utakaochezwa kwenye uwanja wa Azam Chamazi ikiwa ni sehemu ya maandalizi yao.

Akizungumza jijini jana Katibu mkuu wa Simba Evodius Mtawala alisema mbali na mchezo huo wanaamini mechi kati ya  Taifa Stars na Msumbiji pia itakuwa kipimo tosha kwa wachezaji wao kabla ya kuivaa Kiyovu siku mbili baadae.

Simba itaingia uwanjani kuivaa Azam bila ya nyota wake walioitwa kwenye kikosi cha Stars, imefufua matumaini baada ya majeruhi wake Amir Maftah, Ulimboka Mwakingwe pamoja na Haruna Moshi kupona na kucheza katika pambano hilo.

Mtawala alisema timu hiyo inaendelea na mazoezi chini ya kocha Milovan tayari kwa pambano hilo na wamepani kuendeleza heshima nyumbani na kuhakikisha wanatoka na ushindi.

"Jumamosi hii tutacheza na Azam asubuhi katika pambano la kirafiki, tunaendelea vyema na maandalizi ya mchezo wetu wa marudio ambao utachezwa hapa nyumbani wikiijayo na kila kitu kinakwenda vizuri," alisema Mtawala.

No comments:

Post a Comment