Search This Blog

Friday, February 24, 2012

NIZAR KHALFANI HATIHATI KUIKWAA MSUMBIJI!

Timu ya Philadelphia Union imemuacha kiungo Mtanzania Nizar Khalfan ikiwa ni wiki chache baada ya klabu hiyo kuwa imemsajili toka Vancouver Whitecaps. Philadelphia Union ilimsajili Nizar kwenye mchakato wakubadilishana wachezaji uliofanyika November 23 mwaka jana baada ya Vancouver Whitecaps kumpeleka Philadelphia siku moja kabla. Kuachwa kwa Nizar kunaacha wazi nafasi moja ya mchezaji wa kimataifa kwenye timu hiyo huku ikisaliwa na wachezaji saba tu wa kimataifa kati ya nafasi tisa zinazoruhusiwa na MLS kwa wachezaji wa kimataifa toka nchi nyingine .
Khalfan ambaye ni mzaliwa wa Mtwara , aliichezea Vancouver mechi 22 za msimu wa Ligi ya marekaniikiwemo michezo 9 ambayo alikuwemo kwenye kikosi cha kwanza . Katika muda wa dakika       1, 066, kiungo huyu mwenye umri wa miaka 23 alifanikiwa kufunga bao moja huku akitoa pasi nne za mwisho . Khalfan Alijiunga na Vancouver mwaka 2009 wakati timu hiyo ilipokuwa kwenye ligi daraja la kwanza ambapo alicheza michezo 58 ambayo ni sawa na dakika 3,029.
Taarifa ambazo nimezipata hivi punde Nizar huenda asije nchini kujiunga na kambi ya Taifa Stars inayojiandaa kucheza na Msumbiji.
Nizar yupo bize akitafuta timu ya kujiunga nayo kabla ya ligi kuu ya Marekani maarufu kama MLS kuanza hapo mnamo mwanzoni mwa mwezi wa tatu.

1 comment:

  1. shaffi sijaelewa umesema nizar ana miaka 23? haaa haaa haaa jamani wabongo hivi mpaka lini tutakua tunadanganya umri?mi nakua namkuta nizar mara leo nakua nimemzidi umri kweli jamani?Nizar ana miaka 31 namjua vyema
    chela

    ReplyDelete