Search This Blog

Thursday, January 26, 2012

PREMIER LEAGUE: TOP 5 GOALKEEPER IN PREMIER LEAGUE







Msimu mpya wa Epl umefikia katikati sasa na mapambano ya kugombea ubingwa yakiwa yanazidi kupamba moto. Wachezaji wengi wameibuka na kucheza vizuri katika kuzisaidia timu zao kufanya vizuri katika michuano hii.

Hivyo basi, leo hii tutajaribu kuangalia wachezaji ambao wamekuwa katika kiwango cha juu tangu mwanzoni mwa msimu mwezi August 2011 mpaka hivi karibuni.

Kwa kuanzia tuangalie magolikipa watano bora mpaka kufikia katikati mwa ligi.

MICHEL VORM

Team: Swansea

Umri: 28

Utaifa: Uholanzi

Vorm amekuwa outstanding tangu mwanzoni mwa msimu, japokuwa anachezea katika klabu ndogo, ambayo ndio imepanga katika ligi kuu.

Swansea kwa sasa wapo katika nafasi ya 13, wakiwa wameruhusu nyavu zao kuguswa mara 27 huku Vorm akiwa ndio nguzo imara ya timu hiyo.

Uwezo binafsi wake wa kuokoa michomo ndio unaomfanya awemo katika listi ya magolikipa bora wa Premier league,huku akizivutia klabu za Chelsea na Manchester United.

BRAD FRIEDEL

Team: Tottenham Hotspurs

Umri: 40

Utaifa: Marekani

Kipindi Friedel alipojiunga na Spurs wengi walitabiri kwamba Blackburn Rover’s keeper angekuwa chaguo la pili nyuma ya Gomez ambaye ndiye alikuwa mtu wa mwisho mbele ya milingoti ya Spurs.

Lakini Harry Redknapp alikuwa na mawazo mengine, mawazo ambayo yameonekana kuwa na faida mpaka sasa.

Friedel ametumia kila aina ya uzoefu wake katika kuisadia Spurs kuwa moja ya timu zinazowania ubingwa na kutoa ushindani kwa timu za jiji la Manchester.

Spurs mpaka sasa wameruhusu nyavu zao kuguswa mara 24 tu, ushahidi tosha namna uzoefu Friedel ulivyo muhimu katika safu ya ulinzi ya timu hiyo.

JOE HART

Team: Manchester City

Taifa: England

Rekodi ya ulinzi ya Manchester City inaongea yenyewe. Wakiruhusu magoli 18 katika michezo 22 inaonyesha ni jinsi gani ukuta wao ulivyoundwa vizuri, huku Hart akiwa makini hakuna kinachopita na kuingia nyuma yake.

Manchester City wamekuwa waki-improve kila kukicha tangu timu yao inunuliwe na matajiri wa kiarabu, Roberto Mancini amechukua tahadhari kubwa katika kuhakikisha anakuwa ukuta imara, tabia ipendwayo na makocha wa kiitaliano.

Lakini Hart bora zaidi hata katika uwezo binafsi na kuwa nguzo imara katika mafanikio ya City msimu huu.

TIM HOWARD

Team: Everton

Umri: 32

Taifa: Marekani

Sio mara nyingi kuwaona wamerakani katika listi moja ya wanasoka, wall huyu hapa ni golikipa wa kimarekani wa pili katika listi ya magolikipa waliofanya vizuri katika EPL, na kiukweli wanastahili.

Everton wanaweza kuwa hawapo katika nafasi nzuri, kwa sasa wapo katika nafasi ya 14 wakiwa wameruhusu nyavu za kutikiswa kwa mara 26, lakini hilo haliwezi kumnyima Howard nafasi yake katika listi hii, amekuwa ndio key ya mafanikio ya Everton hivi karibuni, na kama isingekuwa mmarekani huyu then ni dhahiri Everton wangekuwa kwenye nafasi mbaya zaidi.

PEPE REINA

Team: Liverpool

Umri: 28

Taifa: Spain

Liverpool inaweza ikawa haijafanya vizuri sana msimu huu lakini kamwe hauwezi kutoa credit kwa uwezo mkubwa alionao kiongozi huyu safu ya ulinzi ya watoto wa Anfield.

Mpaka sasa Liverpool wakiwa na ulinzi wa Reina kwenye milingoti mitatu wameruhusu nyavu zao kutikiswa mara 21, sawa na vijana wa Sir Alex Ferguson ambao wanashika nafasi ya pili.

No comments:

Post a Comment