Search This Blog

Tuesday, January 10, 2012

AZAM YAENDELEZA UBABE KWA VIGOGO: YAITANDIKA SIMBA 2-0 NA KUIVUA UBINGWA


Timu ya Azam FC imekuwa zaidi ya shule kwa timu za Simba na Yanga katika michuano ya Mapinduzi Cup, kufuatia kuifundisha Yanga kucheza mpira na kisha kuwapa somo Simba kutumia nafasi wanazopata.

Washambuliaji wawili wasio kubalika nchini Gaudence Mwaikimba na John Raphael Bocco ndio waliopeleka kilio kwa Simba hii leo, ambapo Simba walitengeneza nafasi za kutosha na kushindwa kuzitumia.

Mchezo ulitulia kati huku viungo wa Simba wakitawala eneo hilo katika kipindi cha kwanza na kutengeneza nafasi lukuki ambazo ziliishia kupotea huku Azam FC wakitumia vyema nafasi ya dakika 10 kujipatia goli la kuongoza lililo fungwa na John Raphael Bocco.

Simba ambao walionekana kuwa nadhamira ya kusawazisha goli hilo bila mafanikio, walipigiwa msumari wa pili na mtokea bench Gaudence Mwaikimba aliyechukua nafasi ya Kipre Tchetche katika dakika ya 85 na katika dakika ya 90 alitupia goli la pili.

Mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Amani Zanzibar ulishuhudiwa na mashabiki lukuki, huku mchezo ukiwa ni wakasi na ushindani Mkubwa.

Kwa matokeo hayo ya goli 2-0 walio upata Azam FC, una wavua ubingwa Simba na hivyo Azam kutinga fainali ambayo itachezwa january 12 katika uwanja wa Amani, wakati mpinzani wake akitarajiwa kujulikana Kesho pale Mafunzo watakapo chuana na Jamhuri ya Pemba katika nusu fainali ya pili.

ABOODMSUNI

2 comments:

  1. Mimi ni shabiki wa ukweli wa Simba but nashukuru tumefungwa na Azam,imefika wakati viongozi wetu waache siasa kwenye mpira kwani kuna nyakati nashindwa kuelewa wanataka waendeshe soka katika mkondo upi,Wamekua wakwanza kuilalamikia TFF kuhusu ligi kuendeshwa na kampuni na kuachana na kamati kwa madai ya kukuza pato na ku adopt soka la kiuweledi,wakati ndani ya timu zao hakuna uweledi hata kidogo,kwanza hawana mpango mkakati na kama upo hautekelezwi kama unabisha we muulize rage au nchunga malengo yao ya miaka mitano kisoka wanataka wa achieve nini hawezi kukwambia na hili utalijua kutokana na namna wanavyotafuta makocha na mikataba wanayo ingia na hawa makocha,ivi kweli kama mna mpango wa atleast miaka mitano mnaweza kuingia mkataba wa mwaka mmoja na kocha?Na kwanini basi wasiweke vigezo vya wazi vya hizo kazi za ukocha kuliko kuleta siasa na matokeo yake kuleta makocha ambao kumbe hata vyeti hawana kama Basena?halafu angalia usajili wao,simba imekua na tatizo la washambuliaji baada ya Mgosi kushuka kiwango na kuamua kumuacha aende motema pembe,badala ya kutatua tatizo in a longrun wamemleta sunzu ambae anasema ana miaka 30,ukijumlisha na aliodanganya unaweza kukuta kamzidi Gigs,huyu hawezi kua suluhisho hata kidogo,nashauri wawape makocha mikataba ya muda mrefu ambayo itaangalia mpango mkakati wao na kocha afanye kazi kufikia malengo yaliyomo kwenye mpango mkakati huku akipewa ushirikiano na facility zote anazohitaji kama kocha na benchi lake la ufundi,na kama hatafikia malengo ndani ya hiyo timeframe then atakua ka vunja mkataba kuliko ilivyo sasa.Jiulize hivi,Simba waliunda kamati ya ushindi dhidi ya Azam wakawakutanisha hadi washabiki huko zanzibar ili kuunganisha nguvu sidhani kama azam alikua na kamati hii special kwaajili ya Simba na yaliyotokea ndio haya,viongozi wabadili ideology zao kuhusu soka na ukampuni uanzie ndani ya vilabu ndo twende kwenye ligi otherwise hiyo kampuni ya ligi itaingia migogoro mikubwa kama watu wenyewe wanawaza kupanga matokeo.
    Ni hayo tu,Chela wa dom

    ReplyDelete
  2. kaka mbona hiyo link haifunguki maana kunawengine hatukubahatika kuangalia game.

    ReplyDelete