Search This Blog

Friday, December 16, 2011

SEMINA YA KUVUMBUA VIPAJI (GRASSROOTS)

Semina ya mafunzo ya kuhamasisha watoto kucheza mpira wa miguu na kuvumbua vipaji (Grassroots) inamalizika kesho (Desemba 17 mwaka huu) kwa tamasha (festival) litakalofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Tamasha hilo litakaloshirikisha watoto 1,200 wa Mkoa wa Dar es Salaam wenye umri kati ya miaka 6-12 litaanza saa 3 asubuhi na kumalizika saa 6 mchana kwa mkutano na waandishi wa habari. Mzungumzaji mkuu katika mkutano huo atakuwa Rais wa TFF, Leodegar Tenga ambapo mbali ya grassroots, pia atazungumzia masuala mengine ya mpira wa miguu ikiwemo kujibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari.

No comments:

Post a Comment