Search This Blog

Friday, December 30, 2011

GARY CAHIL NJIANI KUELEKEA DARAJANI KUUNDA UKUTA NA TERRY


Owen Coyle amethibitisha Bolton wamekubali kumuuza Gary Cahil kwenda Chelsea.

The England defender, ambaye anamaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu, anatarajiwa kujiunga na Chelsea kwa ada ya inayotajwa kufikia £7million.

Manager Andre Villas Boas amekuwa katika harakati kuimarisha safu yake ya ulinzi baada ya kumwambia Alec anaweza kutafuta klabu nyingine ya kuitumikia.

Akiongea juu ya mchezo unaofutia dhidi ya Wolves, Coyle alisema: “Hali ilivyo ndani ya klabu kwa sasa, Bolton Wanderers na Chelsea wameshakubaliana juu ya ada ya Gary Cahil.

“Sasa ni juu ya wawikilishi wa Gary kuongea na Chelsea. Nimeshaongea na Gary na kumwambia aendelee ku-focus kucheza soka akiwa bado mchezaji wa Bolton mambo yake ya usajili awaachie wawikilishi wake.

Cahil ambaye alijiunga na Bolton in 2008 kutoka Aston Villa, ikiwa atafanikiwa kujiunga na Chelsea atakwenda kuuunda ukuta imara kwa pamoja na mchezaji mwenzie wa timu ya taifa ya England John Terry, ambaye kwapamoja wameonekana kucheza vizuri kwa pamoja ndani ya kikosi cha Three Lions.

No comments:

Post a Comment