Search This Blog

Wednesday, December 28, 2011

COUNTDOWN : MATUKIO YA MICHEZO MWAKA 2011:



4. NAFASI YA NNE INAKWENDA KWA MWAMUZI ALIYETOA KALI YA KARNE KAMA SI YA MWAKA .SIKU ZOTE MCHEZO UNAPOKUWA MGUMU MASHABIKI NA WACHAMBUZI WA SOKA HUSEMA KUWA PAMBANO AU MECHI IMEMSHINDA MWAMUZI LAKINI SI MWAMUZI HUYU ALIYECHEZESHA MCHEZO WA LIGI DARAJA LA TANO NCHINI ARGENTINA.

DAMIEN RUBINO ALIONYESHA KUWA MECHI ZA KIHUNI SI LOLOTE WALA CHOCHOTE KWAKE KWANI ALITOA KADI NYEKUNDU 36 KWENYE MECHI KATI YA CLAYPOLE NA VICTORIANO ARENAS .

KWA MAHESABU SAHIHI MWAMUZI HUYU ALITOA KADI KWA WACHEZAJI KUMI NA MOJA WA TIMU ZOTE ZILIZOANZA YAANI KADI 22 NA KISHA AKAFUATIA KWA KUTOA KADI NYEKUNDU KWA WACHEZAJI 14 WA AKIBA TOKA TIMU ZOTE MBILI.

KWA KIFUPI REFA HUYU ALIMALIZA PAMBANO KWANI BAADA YA HAPA HALIKUWEZA KUENDELEA LAKINI ALITOA ADHABU HII KWA WACHEZAJI WOTE WAKOSE MECHI ZINAZOFUATA NA KUWALAZIMU KUSIMAMISHA MICHEZO YAO KWA KUKOSA WACHEZAJI WA KUCHEZA.


5. SIKU ZOTE SI MARA NYINGI UNAWEZA KUKUTA MWAMUZI WA MCHEZO AKIFANYA JAMBO LA KUKUMBUKWA NA MASHABIKI. LAKINI HII SI KWA MWAMUZI TOKA MEXICO MARCO RODRIGUEZ AMBAYE ANAONEKANA KULIELEWA SOMO LA FIZIKI KULIKO WAAMUZI WENGI WA MCHEZO WA SOKA.


KATIKA MCHEZO WA LIGI DARAJA LA PILI HUKO MEXICO , MWAMUZI HUYU ALIPATA MTIHANI WA UFITI WA MWILI WAKE KWA KUWA MCHEZO ULIKUWA WA KASI KUBWA .


KATIKA MCHEZO HUO , MWAMUZI HUYU ALILAZIMIKA KUTOA KADI TATU NYEKUNDU NA SABA ZA NJANO KUTOKANA NA MCHEZO MBAYA WALIOKUWA WANAONYESHA WACHEZAJI WA TIMU ZOTE.


REFA HUYU ALITOA KALI PALE ALIPOKUWA NA KADI MBILI MBILI YAANI NJANO MBILI NA NYEKUNDU MBILI , HIVYO ALIKUWA AKITOA KADI MBILI KWA WACHEZAJI WAWILI KWA MPIGO BADALA YA KUTOA KADI MOJA NA KUGEUKA KUTOA KWA MTU MWINGINE.

6. WAKATI TIMU YA RIVER PLATE ILIPOSHUKA DARAJA KWA MARA YA KWANZA NDANI YA HISTORIA YAKE YA ZAIDI YA MIAKA 100 MASHABIKI HAWAKUFURAHISHWA NA TUKIO HILI.MUDA MFUPI BAADA YA MCHEZO MASHABIKI WA RIVER WALIANZA MAANDAMANO JIJINI BUENOS AIRES HUKU WAKIFANYA VURUGU KUBWA , TUKIO HILI NI MOJA YA MATUKIO YA KUKUMBUKWA KWA MWAKA HUU.

No comments:

Post a Comment