Search This Blog

Thursday, November 24, 2011

MKWASA NA JULIO WATANGAZA WACHEZAJI 20 WALIOPITA KATIKA CHUJIO LA KILI STARS

Kocha Mkuu wa timu ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars), Charles Boniface Mkwasa ametaja kikosi cha mwisho cha wachezaji 20 kwa ajili ya michuano hiyo inayoanza kesho.


Wachezaji waliobaki kati ya 28 waliokuwa wameitwa awali ni Juma Kaseja (Simba), Shabani Kado (Yanga), Shomari Kapombe (Simba), Godfrey Taita (Yanga), Juma Jabu (Simba), Ibrahim Mwaipopo (Azam) na Juma Nyoso (Simba), Said Murad (Azam), Erasto Nyoni (Azam) na Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Nurdin Bakari (Yanga), Haruna Moshi (Simba) na Mwinyi Kazimoto (Simba).


Wengine ni Said Maulid (Angola), Musa Mgosi (DC Motema Pembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC), Mrisho Ngassa (Azam), Ramadhan Chombo (Azam), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC) na Rashid Yusuf (Coastal Union).


Kilimanjaro Stars itacheza mechi yake ya kwanza Novembe 26 mwaka huu dhidi ya Rwanda.

6 comments:

  1. tupe kikosi kipya basi

    ReplyDelete
  2. mbona simuoni Mwaikimba au ndo mchezaji wa Julio na sio wa Mkwasa?..

    ReplyDelete
  3. Hivi Boban amechaguliwa kwa kigezo gani wakati mazoezi hajafanya.
    wako
    James

    ReplyDelete
  4. Kombe ni ndoto, nahisi kama ni mseto wa Simba na Azam tupu.

    ReplyDelete
  5. Hakuna jipya wachezaj walewale bt kiuzalendo zaid tutafika.By Gedluv B.M wa SAUT Mwnza.

    ReplyDelete