Search This Blog

Tuesday, November 15, 2011

KELVIN YONDAN AWASILISHA UTETEZI WAKE SIMBA, KUJUA HATMA YAKE LEO.


Mlinzi wa kati klabu ya wa Simba, Kelvin Yondan amewasilisha utetezi wake kwa uongozi wa klabu hiyo baada ya kutakiwa kufanya hivyo kutokana na kuondoka kambini bila taarifa yoyote.

Beki huyo ambaye ana mkataba wa mwaka mmoja na klabu ya Simba, hivi karibuni alitoweka kambini bila taarifa yoyote kwa uongozi kitu kilichosababisha kukosa michezo kadhaa ya Ligi Kuu raundi ya kwanza.

Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga alithibitisha uongozi kupokea barua hiyo ya utetezi kutoka kwa mchezaji huyo lakini akasema kuwa wataweka wazi kila kitu siku ya leo.

''Ni kweli mchezaji huyo ametuandikia barua baada ya kukaa kimya muda mrefu pamoja na uongozi kumtaka kujitete kwa barua lakini kiutendaji ni lazima Mwenyekiti aipitie barua hiyo ndipo nami niitangaze,'' alisema Kamwaga.

Uongozi wa klabu hiyo ulimpa nafasi mbili mchezaji kuandika barua ya kujitetea au kukatisha mkataba kama hatakuwa hataki kuitumikia klabu hiyo..

No comments:

Post a Comment