Search This Blog

Sunday, November 6, 2011

BOMU FC WAIFUNGA ASHANTI UTD KATIKA ILALA DERBY


Mpambano wa watani wa jadi wa Ilala Bom FC na Ashanti United ulipigwa leo katika uwanja wa shule ya sekondari Benjamin Mkapa.

Mchezo huo wa Ngao ya jamii unaoashiria kuanza kwa ligi ya mkoa wakisoka Ilala ulizishuhudia timu hizo zikimaliza dakika 90 bila kufungana huku mchezo ukiwa na burudani ya kipekee, kwa mashabiki waliojitokeza.

Changamoto za Mikwaju ya Penati ndiyo iliyoamua matokeo ya leo, ambapo Bom FC waliibuka kidedea kwa mikwaju 4 dhidi ya 3 ya Ashanti United.

No comments:

Post a Comment