Mechi namba 58 ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Yanga na Kagera Sugar iliyochezwa Oktoba 14 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam iliingiza sh. 42,810,000. Watazamaji waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo walikuwa 11,559.
Watazamaji 11,787 walikata tiketi kushuhudia mechi namba 62 ya ligi hiyo kati ya Simba na African Lyon iliyochezwa Oktoba 16 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mechi hiyo iliingiza sh. 41,800,000.
Nayo mechi namba 60 kati ya JKT Ruvu na Azam iliyochezwa Oktoba 15 mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam Chamazi iliingiza sh. 909,000 kutokana na watazamaji 303 waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo.
hongera kaka,ila uache ushabiki. usiweke taarifa za soka kwenye blog, kwa upendeleo.habar nyingi ni za simba,za yanga ni chache.mfano mechi ya jana hakuna ulichokiandika.kwa tabia hiyo hatuwezi kufika
ReplyDelete