Search This Blog

Tuesday, September 27, 2011

NGASSA: DAKIKA 531 BILA GOLI NI KITU CHA KAWAIDA KWENYE SOKA.


Mrisho Ngassa amesema kutofunga kwake mabao katika Ligi Kuu bara sio kwamba kiwango chake kimeshuka isipokuwa ni hali ya mchezo inayoweza ikamtokea yeyote yule.
Winga huyo wa zamani Kagera Sugar, Yanga amecheza dakika 531 bila kufunga bao lolote katika michezo sita aliyoshuka dimbani ikiwa pambano la Yanga alifanyiwa mabadiliko dakika ya 81 na nafasi yake kuchukuliwa na mlinzi, Ibrahim Shikanda.
Ngassa ambaye msimu uliopita wa Ligi Kuu bara alikuwa mfungaji bora baada ya kufunga mabao 16, alisema kutofunga kwake hakumpi presha kwani hali hiyo inaweza ikamtokea yeyote yule.

"Nafikiri mfano mzuri wa hili ni kwa mshambuliaji wa Hispania na Chelsea, Fernando Torres," alisema Ngassa."Hali hii hutokea na kupotea, kiwango changu hakijashuka, naamini hivyo, ipo siku utamsoma tu 'Anko' (Ngassa)," alisisitiza

Alisema hauwezi kusema kwamba kutofunga kwa Torres kiwango chake kimeshuka isipokuwa ni hali ya kisoka na huweza kumkumba mwanamichezo yeyote kwa kipindi fulani.Pia, alisema hali hiyo anaichukulia kama changamoto kwake na kuongeza mapambano katika kuhakikisha anarudia kwenye hali yake ya msimu uliopita na kucheka na nyavu.

Katika hatua nyingine Ngasa alikiri kuwa ligi ya msimu huu ni ngumu kuliko uliopita kutokana na kila timu kufanya usajili mzuri.

No comments:

Post a Comment