Search This Blog

Wednesday, September 7, 2011

Mtwa Kiwhelu Akitaja kikosi chake Bora cha Yanga.





Steven Nemes
Alikuwa kipa mahiri na aliyetisha langoni. Hakuwa mtu aliyetaka masikhara uwanjani.

Mtwa Kihwelo
Mimi mwenyewe nilikuwa sitaki mzaha katika upande wa kulia na nilicheza kama beki wa kupanda na kushuka.

Ken Mkapa
Beki mrefu aliyekuwa katika fomu enzi zake na ambaye alikuwa roho ya Yanga upande wa kushoto. Alicheza soka la uhakika la kupanda na kushuka.

Willy Mtendamema
Alikuwa mahiri katika safu ya ulinzi na muda wote alionekana kuwakumbusha wenzake majukumu yao vema.

Issa Athuman
Marehemu kwa sasa. Alikuwa mchezaji tegemeo katika safu ya ulinzi. Namkumbuka kwa kuwa mkali sana kama ukifanya makosa ya kijinga.

Method Mogella
Marehemu kwa sasa. Alikuwa kiungo mtaratibu uwanjani huku akicheza sana soka la akili. Atakumbukwa na wengi kutokana na kipaji chake murua.

Zamoyoni Mogella
Alikuwa hana mfano uwanjani na alikuwa roho ya timu. Vile vile alikuwa mshauri mzuri kwa wachezaji wengine.

Steven Mussa
Marehemu kwa sasa. Alikuwa mchezaji mtaratibu lakini mshindani uwanjani. Alikuwa kiungo maridadi sana na aliweza kuunganisha timu muda wote bila ya kuchoka.

Said Mwamba
Marehemu kwa sasa. Wengi wanakifahamu kipaji cha Said. Alikuwa bora sana uwanjani na asiye na mzaha kama utafanya makosa ya kijinga.

Mohamed Hussein
Alikuwa mfungaji hodari wakati huo. Asingeweza kupoteza nafasi mbili za wazi kama washambuliaji wa kileo.

Edibily Lunyamila
Wote tunafahamu sifa za Edibily. Ndiye aliyekuwa nyota wa michuano ile. Alikuwa fiti sana Eddy na alitubeba kwa kiasi kikubwa.

No comments:

Post a Comment