Search This Blog

Saturday, August 13, 2011

Preview ya England Premier League: Newcastle vs Arsenal

Ligi ya England hatimaye imeanza na leo mechi kubwa itakuwa baina ya Newcastle United watakaokuwa wenyeji wa Arsenal kwenye uwanja wa St James Park .

Mara ya mwisho mechi hii ilimalizika kwa mabao nane kwenye sare ya 4-4 huku Newcastle wakishinda mchezo wa awali 1-0 . Kama kuna chochote kitakachojirudia kwenye mchezo wa leo basi hakika mchezo huu utakuwa mkali na wa kutegemewa kwa mengi.

Arsenal wamekuwa na bahati mbaya ya kuwa na majeruhi kwenye timu yao, hasa kwenye michezo ya pre-season ambapo Jack Wilshere,Theo Walcott, na Kieran Gibbs waliumia vibaya japo si vibaya sana lakini watakosa mchezo dhidi ya Newcastle ila Thomas Vermalen na Robin Van Persie watakuwa fiti kuanza .

Kitu ambacho kinakuja kama habari mbaya kwa Arsenal ni kukosekana kwa Samir Nasri na Cesc Fabregas ambao wako mbioni kuihama Arsenal .

Unaweza kushangazwa na jinsi kukosekana kwa watu hawa kunavyochukuliwa kuwa habari mbaya . Fabregas alitarajiwa kuondoka hilo halina ubishi ,

tatizo linakuja kwa kukosekana kwa wale waliokuwa wanatazamwa kama watu wanaokuja kuziba pengo lake , Samir Nasri na Jack Wilshere na hapo ndio unapoweza kuona shimo ambalo linaweza kuwagharimu Arsenal kwenye eneo la katikati ya kiwanja .

Ukiacha hayo kuna sababu ya furaha kwa wanaarsenal kwani nyota wao mpya Gervais Yao Kone atakuwepo na kila mmoja anajua uwezo wake . Akiwa sambamba na Robin Van persie ni dhahiri wataipa makali yanayohitajika safu ya ushambuliaji ya Arsenal .

Upande wa midfield Arsenal watalazimika kumtumia Aron Ramsay kama mbadala wa Jack Wilshere huku akisaidiwa na yoyote kati ya Abou Diaby na Alex Song huku Tomas Rosicky naye akiwemo kwenye orodha ya viungo walioko fiti kucheza . Wapo pia kina Andriy Arshavin , Riyo Miyachi na Alex Oxlade Chamberlain .

Golini atakuwepo Wojciech Szczesny huku akilindwa na Armand traore upande wa kushoto ambaye anakuja kuziba pengo la Kieran Gibbs aliyeumia , huku Bacary Sagna akiwa kwenye nafasi yake ya kawaida kwenye eneo la kulia kwenye safu ya ulinzi.

Mmojawapo kati ya Laureant Koscielny au Johan Djorou atakuwa pamoja na Thomas Vermalean kwenye moyo wa defence . Uwepo wa Thomas Vermalaen utaisaidia sana Arsenal ambayo imekuwa kwenye wakati mgumu kwenye eneo hilo hasa ukizingatia kuwa Newcastle itakuwa na watu wenye vimo virefu kwenye safu yao ya ushambuliaji Shola Ameobi na Demba Ba .

Swali gumu litakuwa nani atayecheza kama msaidizi wa Vermalen. Djorou alijitahidi sana msimu uliopita lakini Koscielny amecheza vizuri kwenye michezo ya Pre-seaon akionyesha uwezo mkubwa wa kuusoma mchezo na kukatiza pasi hatari za maadui na imani kubwa ya Arsene Wenger itakuwa kwake .

Kwa upande wa Newcastle , mchezo huu utakuwa mgumu kwao ukizingatia kuwa wameondokewa na wachezaji wengi muhimu waliokuwepo msimu uliopita . Newcastle ya sasa inawakosa kina Kevin Nolan , Andy Caroll na Jose Enrique ambaye hivi majuzi tu amemfuata Caroll Merseyside. Kuna utata juu ya uwepo wa Joey Barton ambaye pamoja na kuwa fiti na uwezo mkubwa aliounyesha msimu uliopita atakosekana kutokana na uhusiano mbovu alio nao na viongozi wa timu hususan mmiliki Mike Ashley na kocha Allan Pardew.

Bado Hatem Ben Arfa hajawa fiti kwa asilimia 100 na haya yote yanapunguza makali yalikuwepo Newcastle msimu uliopita kwa kiasi kikubwa sana . Ukiaachana na hayo bado Newcastle ni timu yenye uwezo wa kuiletea Arsenal matatizo . Demba Ba akishirikiana na Shola Ameobi ni watu wenye uwezo wa kufunga .

Kiungo kitakuwa chini ya Ismael Cheikh Tiote ambaye alifanya vizuri mno msimu uliopita . Atakuwepo pia kijana mpya toka Ufaransa Yoan Cabaye sambamba na wachezaji waliokuwepo msimu uliopita kama Jonas Guttierez na nahodha mpya Fabricio Coloccini.

Newcastle pia wana matatizo kwenye majeruhi ambapo watamkosa kipa Steven Harper na beki Noel Perch huku Dan Guthrie naye akikosekana.
Kama ilivyokuwa kwa michezo ya msimu uliopita , mchezo huu utakuwa mkali kwa kuwa timu zote zitautazama kama mchezo ambao matokeo yake yatakuwa mwelekeo wa msimu mzima .

Timu zinatarajiwa kuwa kama ifuatavyo.
NEWCASTLE UNITED

Krul
Simpson, Coloccini, S Taylor, R Taylor
Gutierrez, Barton, Cabaye, Tiote
Ameobi, Ba


ARSENAL

Szczesny
Sagna, Djourou, Vermaelen, Traore
Song, Ramsey, Rosicky
Gervinho, Walcott
Van Persie


No comments:

Post a Comment