Search This Blog

Wednesday, August 17, 2011

LIVE MATCH CENTRE: FULL TIME: SIMBA 2 VS YANGA 0.

MPAMBANO WA NGAO YA HISANI KATI YA YANGA NA SIMBA PUNDE UNAANZA.

SIMBA NDIYO INAANZA KUKANYAGA MPIRA.

DK 1: OKWI AMECHEZEWA FAULO,SIMBA WAMEPIGA ,YANGA WAMEOKOA INAPIGWA KONA.

DK 2: KONA ILIYOPIGWA NA SALUM MACHAKU IMEOKOLEWA NA MABEKI WA YANGA.

DK 5: SALUM MACHAKU ANAKOSA BAO,PASI TOKA KWA HARUNA MOSHI.

dk 9: emmanuel okwi anakosa tena bao la wazi,golikipa Shabani Kado ameokoa.

dk 10. HARUNA NIYONZIMA AMEPIGA SHUTI KALI LIMETOKA JUU YA LANGO LA
SIMBA
DK 11: CHACHA MARWA ANAPEWA KADI YA NJANO BAADA YA KUCHEZEA MADHAMBI FELIX SUNZU.

UWANJA UNAONEKANA KUWASUMBUA WACHEZAJI KWANI INAVYOONEKANA UMEMWAGILIWA MAJI JIONI YA LEO, WACHEZAJI HASA WANAOCHEZA KWENYE KIUNGO WANAPATA SANA SHIDA KU-CONYROL MPIRA.

DK:15: GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO,
HARUNA MOSHI ANAIPATIA SIMBA BAO LA KUONGOZA BAADA YA KUUNGANISHA PASI YA FELIX SUNZU.

DK 17: SALUM MACHAKU ANAPATA KADI YA NJANO,WAKATI HUO HUO GODFREY TAITA ANAENDA KUPIGA KONA KUELEKEA LANGO LA SIMBA.

DK 21: HARUNA MOSHI KACHEZEWA RAFU NA JUMA SEIF ,BOBAN AMETOLEWA NJE KWA MACHELA BADO YUPO NJE ANATIBIWA WAKATI HUO HUO KAGO GERVAIS ANAPASHA.

DK 24: SAID NASSOR BEKI WA KULIA WA SIMBA AMEPEWA KADI YA NJANO WAKATI HUO HUO BOBAN ANAREJEA UWANJANI.

DK 27: GODFREY TAITA AMEPIGA KONA AMBAYO IMEOKOLEWA NA MABEKI WA SIMBA.

SO FAR HARUNA NIYONZIMA ANACHEZA VIZURI SANA UPANDE WA KULIA WA YANGA, WAKATI HUO HUO AMIR MAFTAH AMEMCHEZEA FAULO TAITA,NSAJIGWA AMEPIGA VICTOR COSTA ANAOKOA.

DK 35: SIMBA WANAPATA PENALTY BAADA YA BOBAN KUANGUSHWA NA NADIR HAROUB.

DK 37: GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO,FELIX SUNZU ANAIPATIA SIMBA BAO LA PILI

DK 41: KWA MTAZAMO WANGU YANGA WALISTAHILI KUPEWA PENALTY BAADA YA KEN ASAMOAH KUANGUSHWA KWENYE ENEO LA HATARI.

DK 45: SIMBA ANAONGOZA MABAO MAWILI KWA BILA WAKATI HUO HUO DAKIKA MBILI ZIMEONGEZWA, SIMBA WAMEPATA KONA IMEPIGWA NA AMIR MAFTAH SAIDI CHOLLO KAPAISHA.


HALF TIME SIMBA 2 YANGA 0

DK 46: KIPINDI CHA PILI KIMEANZA HAKUNA MABADILIKO KWENYE VIKOSI VYA TIMU ZOTE MBILI.

DK: 48 YANGA WANAPATA FAULO NJE YA 18, NIYOZIMA ANAPAISHA

DK 49: YANGA WANAKOSA BAO LA WAZI

DK 50: HAMIS KIIZA ANATAKA KUINGIA

DK 51: KIGI MAKASI ANATOKA HAMIS KIIZA ANAINGIA KWA UPANDE WA YANGA

DK 53: KADI YA MAJANO KWA GODFREY TAITA KWA KUMCHEZEA FAULO EMMANUEL OKWI

DK 56: CHACHA MARWA ANAPIGA SHUTI KALI KASEJA ANADAKA VIZURI

DK 57: YANGA WANAPATA KONA INAOKOLEWA.

DK: 60: SIMBA WANAFANYA MABADILIKO WANAINGIA AMRI KIEMBA NA GERVAIS KAGO ,WANATOKA SALUM MACHAKU NA HARUNA MOSHI

DK 64: YANGA WAMEPATA KONA AMBAYO IMESINDWA KUZAA MATUNDA.

DK 66: YANGA WANAFANYA MABADILIKO ANATOKA KEN ASAMOAH ANAINGIA RASHID GUMBO.

DK 70: EMMANUEL OKWI AMEUMIA NA NAFASI YAKE ANAICHUKUA SHOMARI KAPOMBE

DK 85: BADO SIMBA INAONGOZA MABAO 2-0 ILA YANGA WANACHEZA VIZURI SANA .

DK 86: YANGA WANAPATA KONA,AMEPIGA HARUNA NIYONZIMA NYOSO AKAOKOA,

DK 89: GERVAIS KAGO ANAPIGA SHUTI GOLIKIPA SHABANI KADO ANAOKOA.

DK 90: DAKIKA 90 ZIMEMALIZIKA NA MWAMUZI WA AKIBA ANAONYESHA DAKIKA 3 ZA NYONGEZA. WAKATI HUO HUO SIMBA WANAPATA KONA.

FULL TIME: YANGA 0 SIMBA 2

4 comments:

  1. Huyu Kijiko amezidi kucheza rafu, alimuumizaga Kazimoto hivi hivi

    ReplyDelete
  2. Shaffih asante sana hasa kwa mimi nipo mbali nanyumbani isitoshe siwezi kuzipata game za home online so umenisaidia sana bro JAH! bless.

    ReplyDelete
  3. Yanga mwaka huu walie tu hawatukuti tena.
    Mzimbiri,M.K. Uyole,Mbeya

    ReplyDelete