Search This Blog

Monday, August 15, 2011

BARCLAYS PREMIER LEAGUE NUMBERS


0 – Kwa mara ya kwanza, hakuna timu mwenyeji iliyoshinda katika mchezo wa kwanza wa Barclays Premier League tangu katika msimu wa 1994/95

1 – Kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2011 uanze, Robin Van Persie hajaweza kufunga katika mechi ya ugenini kwenye EPL, baada ya Arsenal kutoa suluhu ya 0-0 dhidi ya Newcastle.Alikuwa amefunga mabao katika kila mechi ugenini ndani ya mechi tisa zilizopita.

4 – Ushindi wa Bolton Wenderers wa 4-0 dhidi ya QPR ulikuwa ndio ushindi wao mkubwa katika EPL tangu wawafunge Everton mwaka 2005, huku ukiwa ndio ushindi wao mkubwa katika historia ya Barclays Premier league ukiufutia ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Leicester City katika msimu wa 2001/02.

5 – Steven Reid alikuwa mchezaji wa 5 wa West Bromwich Albion kujifunga bao katika mwaka 2011, hakuna klabu nyingine iliyozidisha wachezaji watatu.

6 – Fulham wametoa droo 6 za bila kufungana katika Barclays Premier League mwaka 2011, mbili zaidi ya klabu yoyote ile.

7 – Kiungo asiyekuwa na bahati Kieron Dyer alidumu kwa dakika 7 katika mchezo wa kwanza kwa timu yake ya Queens Park Rangers kabla ya kuumia enka.

8 – Manchester United wameshinda mechi 8 za ugenini mfululizo katika Barclays Premier League, wakiifikia all time top flight record.

8 – Penalty iliyokoswa na Luis Suarez kwa Liverpool dhidi ya Sunderland ilikuwa ndio ya kwanza katika michezo ya ufunguzi katika miaka 8 iliyopita.

9 – Droo ya 0-0 ya Fulham kwenye uwanja wa nyumbani dhidi ya Aston Villa inaamanisha kwamba timu hizo zimetoshana nguvu mara 9 katika michezo 14 waliyokutana katika Barclays premier league.

19 – Mchezaji wa Arsenal Gervinho alikuwa mchezaji wa 19 kupewa kadi nyekundu katika mchezo wake wa kwanza wa premier league.

21 – Aston Villa waliweka rekodi ya kutoruhusu bao katika michezo 21 tangu ushindi wao dhidi ya Hull City mwezi aprill 2010 baada ya kudroo 0-0 kwenye uwanja wa Craven Cottage.

46 – Ushindi wa Wolverhampton Wanderers wa 2-1 kwenye uwanja wa Ewood Park ulikuwa ndio ushindi wao wa kwanza dhidi ya Blackburn Rovers katika miaka 46.

No comments:

Post a Comment