Search This Blog

Monday, August 29, 2011

BARCLAYS PREMIER LEAGUE KWENYE NAMBA


0 – Swansea City ndio timu pekee ambayo bado haijafunga bao kwenye EPL msimu huu.The Swans wametoka sare ya 0-0 dhidi ya Sunderland na Wigan Athletic baada ya kupokea kichapo cha 4-0 kutoka kwa Manchester City katika wiki ya ufunguzi.

3 – Ashley Young na Samir Nasri wote wameshatoa assist 3 katika mechi zao walizocheza kwenye EPL Jumapili.Ni mchezaji mmoja alifanikiwa kufanya hivyo msimu uliopita.

3.33 – Baada ya kufungwa 8-2 na United, Arsenal sasa wamefungwa wastani wa 3.33 wa magoli kwa kila mchezo ndani ya EPL msimu huu.

6 – Jumla ya magoli yaliyofungwa na Edin Dzeko katika Epl, akiwa ndio top scorer.

21 – Kufungwa kwao 0-1 na Everton, Blackburn Rovers walipata attempts on goal 21.

34 – Ilimchukua dakika 34 akitokea benchi Juan Mata kufunga bao katika mchezo wake wa kwanza, Chelsea wakishinda 3-1 dhidi ya Norwich.

115 – Mara ya mwisho Arsenal kuruhusu wavu kutikisika mara nane ilikuwa miaka 115 iliyopita, baada ya kufungwa na Loughborough Town in 1896.

1 comment:

  1. Number 8: Man Utd Vs Arsenal ilichezwa tarehe 28, mwezi wa 8, na Arsenal ilifungwa magoli 8.

    ReplyDelete