Search This Blog

Saturday, August 20, 2011

Arsenal 0-2 Liverpool: Kutolewa kwa Frimpong na Mabadiliko ya Liverpool yalibadilisha mchezo.



VIKOSI VYA KWANZA
Bao la kujifunga la Aaron Ramsay na lingine rahisi la Luis Suarez yalitosha kuipa Liverpool ushindi wao wa kwanza wa msimu na ushindi wao wa kwanza dhidi ya Arsenal kwenye uwanja wa Emirates .
Arsene Wenger alilazimika kumchezesha Samir Nasri pamoja na ‘issue’ yake ya kuhamia Man City . Emmanuel Frimpong alichukua nafasi ya Alex Song anayetumikia adhabu na majeraha ya wachezaji wengine yalimaanisha kuwa Arsenal ilimuanzisha Carl Jenkinson kwenye upande wa kulia wa ‘defense’ na kwa mshangao wa wengi akamchezesha Bacary Sagna kwenye nafasi ya beki wa kushoto.
Kenny Dalglish hakumwanzisha Luis Suarez kwa kuwa bado hana ‘match fitness’ kwa hiyo akampanga Dirk Kuyt kwenye upande wa kulia wa ‘midfield’ huku Martin Kelly akicheza nyuma yake .
Kwa ujumla hii ni mechi ambayo ilikosa vitu vingi kiufundi kwa pande zote mbili za Liverpool na Arsenal –Nafasi nyingi za wazi zilitokana na makosa pamoja na mashuti ya mbali na hakukuwa na ufundi wala ujanja wowote kwa timu hizi mbili na Liverpool walipata nafasi ya kuufungua mchezo baada ya mchezaji wa Arsenal Emmanuel Frimpong kuonyeshwa kadi nyekundu kinyume na hapo ilikuwa inaonekana kama sare nyingine ya 0-0 ingetokea.

SARE YA MWANZONI.
Dalglish alikuwa na wepesi wa kuweza kutumia mifumo kati ya 4-4-2 na 4-3-3 kutegemea na ambavyo viungo Jordan Henderson na Dirk Kuyt walivyojipanga kuendana na ‘move’.Dalglish alimpendelea zaidi Kuyt kwa mtindo wake wa uchezaji ambapo hachoki na anakimbia muda wote na hii ikaonekana kama Liverpool wanatumia 4-2-3-1 dhidi ya 4-3-3 ya Arsenal, huku Frimpong akimiliki mpira mara nyingi.

Kwa mchezo dhidi ya Liverpool Frimpong alikuwa mchezaji bora na ndiyo sababu kuu ya Arsenal kufungwa kwa Arsenal , alitolewa kwa kadi nyekundu kwa rafu ya kijinga ambayo hakuwa na sababu ya kuicheza kwa Lucas na akatolewa kwenye dakika ya 70 baada ya kupewa kadi ya njano ya kizembe kwenye dakika ya 7.
Hatari za kiungo mkabaji kuonyeshwa kadi ya njano mapema zimezungumzwa sana na kutolewa kwa Frimpong kuliigharimu Arsenal na ishara za kutolewa kwake zilionekana tangu mapema .
Frimpong alimiliki mpira vizuri sana .

Huku Henderson akikabana na Ramsay kwa muda mrefu kwenye mchezo na Charlie Adam akilazimika kurudi nyuma ili kuwa karibu na Lucas , Frimpong alikuwa na nafasi kubwa sana kwenye eneo la katikati mwa uwanja na alitumia uhuru alioupata kupandisha timu mbele na kuanzisha mashambulizi kuliko kupiga pasi za ‘square’ pembeni mwa uwanja .
Mara nyingi alipiga pasi zilizoelekea mbele na alikaribia hata kufunga kwa shuti la mbali .
PRESSING YA LIVERPOOL’.
‘Pressing’ ya Liverpool iliisaidia Arsenal kwa kiasi Fulani kwa sababu upigaji wao wa pasi kuanzia nyuma mpaka mbele kwa washambuliaji haukutofautiana sana na ule wa kwenye mchezo dhidi ya Newcastle , ulikuwa wa kasi ndogo mno .

Tatizo la majeraha ambayo yamekuwa yakiwakumba wachezaji wa Arsenal halikuwasaidia . Bacary Sagna alikuwa anapata tabu sana kupandisha mipira upande wa kushoto na tatizo hilo pia lilionekana kwa Vermalaen pale ambapo alilazimika kuhamia upande wa kulia baada ya kutoka kwa Laureant Koscielny.Huku Sagna na Vermalaen wakicheza sehemu ambazo si sehemu zao za kawaida , na wachezaji kama Miquel na Jenkinson wakiwa kwenye mechi yao ya kwanza jambo ambalo liliwafanya wacheze kwa woga , pasi za Arsenal kuanzia nyuma zilikuwa mbaya mno kwa kuwa hazikuwa kwenye kasi ya Arsenal iliyozoeleka .
Liverpool wanapaswa kupongezwa kwa aina yao ya ‘pressing’ . Kuyt , Henderson na Stewart Downing waliwatia mabeki na Viungo wa Arsenal presha ya hali ya juu ukizingatia kuwa Charlie Adam kwa kawaida hana kasi na hana ‘movement’ nyingi awapo uwanjani japo kwa mchezo dhidi ya Arsenal alijitahidi sana hasa pale alipokuwa hana mpira , akifanya ‘tackling’ karibu tano ambazo zilifanikiwa na alifanya ‘interceptions’ tatu za uhakika .
Liverpool walimiliki mpira zaidi ya Arsenal pia kitu ambacho si cha kawaida kwa Arsenal ambao humiliki mpira zaidi na Liverpool ambao mpira wao ni wa kasi na moja kwa moja zaidi usiozingatia sana kumiliki mpira kwa muda mrefu.

Waliomiliki mpira kwa kiasi kikubwa walikuwa mabeki wa pembeni japo kulikuwa hakuna mpango wowote wa kutafuta bao mapema tofauti na ule wa kumtumia Andy Caroll wa kumlisha mipira ya juu kwa kutegemea urefu wake . Mabeki wa kati wa Arsenal wanapswa kupongezwa pia kwa jinsi walivyoweza kummudu Caroll na urefu wake huku ‘combinationa ya Downing na Caroll ikionekana kufanya kazi vyema japo hadi sasa hakuna krosi yoyote ya Dwoning ambayo imekutana na kichwa cha Caroll na kuzalisha bao .
Jose Enrique alikuwa mchezaji bora kwa Liverpool kwenye na Theo Walcott hakuwa na jinsi ya kumzidi ujanja , Enrique ana kasi kuliko Walcott na ana nguvu na’positioning’ yake ni nzuri kiasi cha kutokuwa na tatizo lolote akiwa anamkaba na Walcot kwa upande wake hakuwa na mchango mkubwa kwenye mchezo .Walcott na Arshavin wanahitaji kuingia ndani na kutafuta mabao wakati mpira uko kwenye winga nyingine –Walcott anasema kuwa anapenda kuchezeshwa kati kama mshambuliaji lakini kuna ‘move’ kwenye dakika ya 28 ambapo Walcott alibaki kwenye winga ya kulia wakati kama angekimbia kuingia kati angeweza kupata bao rahisi.

DAKIKA YA 70

Mchezo ulikuwa sare hadi dakika ya 70 ambapo mambo mawili yalitokea . Kwanza Frimpong alitolewa kwa kadi nyekundu na pili Raul Mereles aliingia kuchukua nafasi ya Jordan Henderson na Andy Caroll alitoka na nafasi yake kuchukuliwa na Luis Suarez.
Mambo haya yalitokea kwa kufuatana na ni vigumu kusema ni tukio gani lilikuwa na ‘impact’kwenye mchezo kuliko linguine lakini yote yalikuwa na ‘impact’ kubwa .
Liverpool walifaidika na kuwa na mtu mmoja zaidi uwanjani kwani walimiliki mpira .

Mpaka kufikia dakika ya 70 Arsenal walikuwa wamepiga pasi 322 na Liverpool walikuwa wamepiga 281 –lakini kuanzia dakika ya 71 kwenda mbele hadi mwisho Arsenal walipiga pasi 105 na Liverpool walipiga 141 .Faida ilikuwa upande wa Liverpool.
Hapa ndipo msingi wa ushindi wa Liverpool ulipojengewa na ‘move’ nyingi zilianzia kipindi hiki huku Meireles na Suarez wakitengeneza nyingi zaidi .

Kutoka kwa Frimpong kulimaanisha kuwa Arsenal ililazimika kutumia mfumo wa 4-4-1, hii ilimpa Meireles nafasi kubwa katikati ya wachezaji wa Arsenal na aliweza kupeana pasi na wenzie .
Kuingia kwa Suarez kuliongeza ‘movement’ za kijanja zaidi ya zile zilizokuwepo wakati Caroll akiwa uwanjani . Mabao yote mawili yalianza na pasi za Meireles kwa Caroll . La kwanza ilikuwa bahati mbaya kwa Aron Ramsay kujifunga nala pili lilikuwa ‘move’ nzuri ambayo ilimkuta Suarez akiwa mwenyewe na kumaliza .


Mwisho.
Mchezo haukuwa wa kusisimua kama ilivyotarajiwa na ulipata uhai kwenye dakika 20 za mwisho –nidhamu mbaya iliwagharimu Arsenal , lakini mbinu za Dalglish zilifanya kazi na kufanikiwa .

Alitoka sawa na Arsenal wakiwa 11 v 11 , na akaingiza wachezaji ambao walikuwa wajanja kuyafanyia kazi mashimo yalionekana nyuma baada ya Arsenal kubaki 10. Arsenal bado hawajawa na ushinda uliozoeleka toka kwao .
Walikosa uzoefu kwenye wachezaji wanaocheza nafsi muhimu kama nyuma na pia walikosa ubunifu mbele mara nyingi Robin Van Persie akipiga miayo mwenyewe, hakuna anayejua nini kitawakuta wiki ijayo watakapokutana na Man United .















2 comments:

  1. thanx kwa uchambuzi mzuri sikugundua mambo mengine zaidi yako hata baada ya mechi kumalizika. Takwimu nzuri nimepata za mechi. Sub za liverpool dakika ya 70 zilikua ni ametoka Dirk kuyt akaingia Raul meithanx kwa uchambuzi mzuri sikugundua mambo mengine zaidi yako hata baada ya mechi kumalizika. Takwimu nzuri nimepata za mechi. Sub za liverpool dakika ya 70 zilikua ni ametoka Dirk kuyt akaingia Raul meireles na akatoka Andy caroll akaingia Luis suarez, ila jordan henderson alimaliza mpaka kipenga cha mwisho. Thanx again.Thanx again.

    ReplyDelete
  2. gud, kazi nzur, nxt wk 2taona mbinu za kibabu fergie!gud, kazi nzur, nxt wk 2taona mbinu za kibabu fergie!

    ReplyDelete