Search This Blog

Sunday, July 17, 2011

WAKALA: BARCA NAO WANAMTAKA NEYMAR


Wakala wa mchezaji wa kimataifa wa Brazil Neymar amesema kuwa mahasimu wa Real Madrid, Barcelona nao wameingia katika vita ya kutaka huduma za kinda hilo Santos.
Neymar ambaye pia amekuwa akisakwa na vilabu tajiri vya EPL, Chelsea na Man City lakini wakala Wagner Ribeiro anasisitiza Madrid wana nafasi kubwa ingawa Barca ndio sehemu inayomvutia zaidi mchezaji husika.
Ribeiro anasema Barca wapo tayari kusubiri mpaka mabingwa wa Copa Libertadores Santos wamalize kushiriki katika Club World Cup mwezi December, kitu ambacho kitamruhusu raisi wa Santos Luis Alvaro De Oliveira kutimiza ndoto yake ya kuona Neymar anaiongoza Santos katika mashindano ya dunia kabla hajahamia Ulaya.

No comments:

Post a Comment