Search This Blog

Saturday, June 18, 2011

VILLARREAL YAKATAA OFA YA BARCA KWA ROSSI


Villarreal wamekataa ofa ya kutoka Barcelona kwa ajili ya kumsajili Giusseppe Rossi.

Wakala wa Rossi Federico Pastorello amesema kuwa ofa ya Barca ilikuwa ndogo ukilinganisha na bei ya mwanzo iliyotajwa na Villarreal.

"Nafahamu juu ya Barca kupeleka ofa kwa ajili ya Giusseppe, lakini tumeambia ofa yao ilikuwa haijitoshelezi. Hatujaongea na timu yoyote ndani ya wiki hii.Pia nafahamu kuwa Catalunya bado wanajadiliana na Villarreal, hivyo kikubwa tunachofanya sasa ni kusubiri matokeo ya majadiliano hayo." alisema wakala wa Rossi.

No comments:

Post a Comment