Search This Blog

Saturday, June 18, 2011

SIMBA WAPEWA BASI NA CHAKULA KIBOVU LAKINI BASSENA ASEMA TUTASHINDA




KOCHA Mkuu ya Simba Mganda Moses Bassena amesema licha ya kupata ushindi kiduchu katika mchezo uliopita ana imani kikosi chake kitajituma na kupata ushindi katika mchezo wao wa leo dhidi ya Motema Pembe utakafanyika kwenye Uwanja wa Stade de Martyrs kiswaili ni Uwanja wa mashujaa.

Akizungumza Bassena alisema ana imani kubwa na kikosi chake katika mchezo leo ambapo Simba ikishinda itakuwa imeingia hatua ya makundi .

Bassena alisema kwa muda uliobaki atautumia kurekebisha machache ambayo yalijitokeza katika mchezo ule .

"Nina Imani kubwa na kikosi changu kitaisambaratisha Motema Pembe kesho kwa kuifunga nyumbani kwao"- Bassena.

Naye Nahodha wa Simba nico Nyagawa, amewataka watanzania kuiombea dua timu yao iweze kufanya vizuri katika mchezo huo.



Aidha uongozi wa Simba jana ulibadilisha gari na kuamua kukodi basi lao wenyewe baada ya viongozi wa matoma Pembe kuwapa basi chakavu .

Licha kudibalisha gari uongozi wa Simba umeamua kuitafutia hoteli maalum kwa ajili ya kupata chakula kizuri cha wachezaji baada hoteli wanayokaa kuwapa chakula kkibovu .

No comments:

Post a Comment