Search This Blog

Sunday, June 5, 2011

NAONDOKA WEST HAM - SCOT PARKER


Scott Parker amethibitisha kuwa atamwambia Sam Allardyce kuwa anataka kuondoka West Ham ili aendelee kupata nafasi katika kikosi cha England baada ya kurudi mapumzikoni.

Parker amesema ataongea kocha huyo mpya wa wagonga nyundo London kuongelea mstakabali wake katika timu hiyo, mazungumzo ambayo anaamini yatakuwa katika muelekeo wa kurudi kwenye ligi kuu kama anataka kuitunza nafasi yake katika cha Three Lions.

"Kwenye EPL ndio kila mchezaji angependa kucheza na sipo tofauti, najua Big Sam atanipigia simu na tutaongea, nataka kuendelea kupigania nafasi yangu katika England lakini siwezi kufanya hivyo kama sitocheza EPL msimu ujao."

Parker ambaye ndiye Footballer of the Year wa England anatakiwa na timu za Tottenham, Liverpool na Arsenal.



No comments:

Post a Comment