Search This Blog

Thursday, June 9, 2011

MKATABA KATI YA PUMA NA SAFA UWE CHANGAMOTO KWA TFF YETU.

HII NI JEZI YA TAIFA STARS IKIWA BILA YA NEMBO YA.
MDHAMINI


JEZI HII INA NEMBO YA KAMPUNI YA UHLSPORT JE,KUNA CHOCHOTE
TFF WANANUFAIKA KWA KUITANGAZA HII BRAND?






HUU NI MFANO WA TSHIRT AMBAZO TFF WANGEWEZA KUZIUZA




NA KUTENGENEZA PESA YA KUMWAGA.








HII NDIYO JEZI MPYA YA BAFANA BAFANA BAADA YA SAFA




KUINGIA MKATABA WA MIAKA 7 NA KAMPUNI YA PUMA WENYE THAMANI YA




DOLA MILIONI 2 KWA MWAKA.

Na SHAFFIH DAUDA
CHAMA CHA SOKA NCHINI AFRIKA YA KUSINI KIMEINGIA MKATABA NA KAMPUNI YA VIFAA VYA MICHEZO YA PUMA KWA AJILI YA KUSAMBAZA VIFAA VYA MICHEZO KWA TIMU ZA TAIFA ZA AFRIKA YA KUSINI. NI MKATABA WA MIAKA SABA WENYE THAMANI YA DOLA ZA KIMAREKANI MILIONI MBILI KWA MWAKA ($2M) ZAIDI YA TSH BILIONI 3 ZA KITANZANIA KWA MWAKA.


BAADA YA KUPATA TAARIFA HII IMENIFANYA NIKIFIKIRIE CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU NCHINI TANZANIA TFF, KWA JINSI AMBAVYO KIMEKUWA KIKISHINDWA KUTAMBUA KWAMBA TIMU YA TAIFA NI BIDHAA. LAITI KAMA KINGEKUA NA MIPANGO MATHUBUTI JUU YA MAENDELEO YA SOKA, KINGEWEZA KUPATA PESA AMBAZO ZINGEKIPUNGUZIA GHARAMA NYINGI ZA UENDESHAJI WA TIMU ZA TAIFA, NA MATOKEO YAKE KWA VIPINDI TOFAUTI, TIMU ZA TAIFA ZIMEKUWA ZIKIVAA JEZI ZENYE NEMBO ZA MAKAMPUNI MBALIMBALI YANAYOTENGENEZA VIFAA VYA MICHEZO PASIPO NA KUWA NA MIKATABA NAYO, NA HIVYO KUTONUFAIKA KABISA KWA KUVAA NA KUZITANGAZA NEMBO HIZO.


HIVI KARIBUNI KATIKA KILE KILICHOONEKANA KANA KWAMBA NI KUJIVUA GAMBA KWA TAASISI HIYO NGURI YA USIMAMIZI WA MCHEZO WA SOKA NCHINI, IKIWAAMINISHA WADAU WA SOKA KWAMBA IMEAZIMIA KULETA MAGEUZI NA MABORESHO YA KIUTENDAJI NA TIJA NDANI YA TAASISI, TFF ILIANZISHA KITENGO KIPYA CHA MASOKO KWA ZINGATIO LA KUZIUZA BIDHAA ZINAZOHODHIWA NA TAASISI HIYO.

LAKINI PAMOJA NA KITENGO HICHO KUANZISHWA CHINI YA MKURUGENZI WA KITENGO HICHO JIMMY KABWE, BADO HAKUNA MABADILIKO YA AINA YOYOTE YA KIUTENDAJI HUSUSANI KATIKA IDARA HIYO YA MASOKO YALIYOKWISHAONEKANA HADI SASA.

LENGO LANGU KUBWA HASA LA KUANDIKA WALAKA HUU NI KUTAKA KUELEZEA NAMNA AMBAVYO VYAMA VYA SOKA VYA NCHI MBALI MBALI ULIMWENGUNI VINAVYONUFAIKA KWA KUINGIA MIKATABA MINONO NA HAYA MAKAMPUNI YA KUTENGENEZA VIFAA VYA MICHEZO ,

NI KWELI MAKAMPUNI HAYA HUPENDA KUJIHUSISHA NA VYAMA VYA SOKA VYA NCHI HUSIKA AMBAZO TIMU ZAKE ZA TAIFA ZINAFANYA VIZURI.
KWA MFANO KIASI CHA PESA AMBACHO KAMPUNI YA NIKE INALIPA KWA TIMU YA TAIFA YA BRAZIL KUVAA VIFAA VYENYE NEMBO YAKE NI TOFAUTI KABISA NA KIASI WANACHOLIPWA NIGERIA KWA KUVAA VIFAA HIVYO HIVYO VYA NIKE.

KUTOKANA NA HALI YA USHINDANI MKUBWA WA KIBIASHARA ILIVYO DUNIANI HIVI SASA, KAMPUNI YA KUTENGENEZA VIFAA VYA MICHEZO YA PUMA IMEAMUA KUVAMIA SOKO LA AFRIKA AMBAPO AFRIKA YA KUSINI IMEKUA NCHI YA 11 KUINGIA MKATABA NA KAMPUNI HIYO BARANI AFRIKA, ZIKIWEMO PIA BAADHI YA NCHI KAMA IVORY COAST, CAMEROON, MISRI NA MALAWI.
UKISIKIA PUMA INAKILIPA SAFA KIASI HICHO CHA DOLA MILIONI 2 KWA MWAKA UNAWEZA KUDHANI WANALIPA PESA TASLIMU.
HILO PIA LINAWEZEKANA MAANA HATUJUI VIPENGELE VILIVYOMO NDANI YA MKATABA WAO.

LAKINI PIA KUNA UWEZEKANO NDANI YA HUO MKATABA WA KIASI HICHO CHA DOLA MILIONI 2 KUNA PIA GHARAMA ZA VIFAA AMBAVYO SAFA ITAVITUMIA KWA TIMU ZAKE ZA TAIFA (VIJANA, BANYANA BANYANA NA BAFANA BAFANA).
PIA SAFA INAWEZA KUTENGENEZEWA JEZI Z A MASHABIKI (REPLICA) KWA BEI YA JUMLA NA KUZIUZA KWA FAIDA.

KAMA NINGEKUA MKURUGENZI WA MASOKO WA TFF NINGEIONA FURSA HIYO YA KAMPUNI YA PUMA KUTAKA KUJITANGAZA HASWA KUPITIA MATAIFA YA AFRIKA, NA NINGEWATAFUTA WAHUSIKA AU WAWAKILISHI WA KAMPUNI HIYO BARANI AFRIKA, NA KUWAPA MCHANGANUO KAMA SI MAPENDEKEZO ( PROPOSAL ) YA KUINGIA MKATABA NA TFF WALAU KWA KUANZIA BILA HATA MKATABA MNONO, LAKINI KWENYE MKATABA KUWEPO VIPENGELE KADHAA VYENYE KUIFADISHA TFF.
KWA MFANO, MOJA KATI YA VIPENGELE HIVYO KATIKA MKATABA NI KUTENGENEZEWA JEZI ZA MASHABIKI (REPRICA ) AMBAZO CHAMA CHA SOKA KITAUZIWA KWA BEI YA JUMLA. MATHALANI TFF IKIUZIWA JEZI MOJA YENYE UBORA KWA TSH 5,000/=, HALAFU WENYEWE WAKAUZA KWA TSH 20,000/= KILA JEZI, HEBU PIGA HESABU KWA NCHI YETU YENYE WATU ZAIDI YA MILIONI 40 ANGALAU WAUZE NAKALA 10,000 TU ZA JEZI, NI FAIDA KIASI GANI WANGETENGENEZA? NI KARIBU MILIONI 150 HIVI.

NADHANI WANGEKUA NA MIKAKATI MADHUBUTI YA NAMNA HIYO VIKOSI VYA TIMU ZA VIJANA WA KIKE NA KIUME AMBAVYO KILA SIKU TUNAAMBIWA HAVINA WADHAMINI, VINGEPATA MATUNZO MAZURI LAKINI PIA BENDERA YA TAIFA INGEWEZA KUPEPERUSHWA VYEMA.
ILI KUWEZA KUFANIKISHA HILI, SIYO LAZIMA TFF WAUZE WENYEWE HIZO JEZI, WANAWEZA KUTANGAZA ZABUNI NA WAKAPATA KAMPUNI NA KUINGIA NAYO MKATABA WA KUSAMBAZA JEZI HIZO, HALAFU KAMPUNI HIYO IKAPATA GAWIO KUTOKA KWENYE FAIDA YA THS 15,000 KATIKA KILA JEZI KUTOKANA NA MAKUBALIANO.

HUU MKATABA MNONO BAINA YA CHAMA CHA SOKA NCHINI AFRIKA YA KUSINI ( SAFA ) NA KAMPUNI YA PUMA UWE CHANGAMOTO KWA SHIRIKISHO LETU LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA ( TFF ), UKIZINGATIA HIVI KARIBUNI TULIWEZA KUCHEZA NAO MCHEZO WA KIRAFIKI.
TUSIISHIE HAPO PIA TUJIFUNZE NAMNA WANAVYOENDESHA MAMBO YAO KITAALAMU NA KISAYANSI KATIKA KUENDESHA MCHEZO WA SOKA.

No comments:

Post a Comment