Search This Blog

Friday, June 24, 2011

GASPERINI KOCHA MPYA WA INTER MILAN


INTER MILAN wamemthibitisha Gian Gasperini kuwa kocha wao mpya.
Gasperini, 53, bado hajamaliza hatua za mwisho za kukamilisha mkataba wa miaka miwili lakini Inter wamethibitisha kuwa ndiye mrithi wa Leonardo.
Akiongea na vyombo vya habari Raisi wa Inter Massimo Moratti alisema: "Nimeridhika na uteuz wa Gasperini, namtakia kazi njema katika kuiwezesha Inter kuwa mabingwa wa dunia."
Gasperini ambaye alikuwa kocha wa zamani wa Genoa, aliiwezesha timu hiyo kurudi katika Seria A na kuiwezesha timu hiyo kupata nafasi ya katika EUROPA Cup kabla hajafukuzwa November mwaka jana.

No comments:

Post a Comment