Search This Blog

Sunday, June 19, 2011

CHELSEA HATARINI KUKATWA POINTI


Chelsea wapo katika hatari ya kukatwa pointi ikiwa watapatikana na hatia ya kumshawishi Luka Modric kujiunga nao isivyo halali.

Akiwa amekasirika mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy amesema anajiandaa kuiripoti Chelsea kwa wasimamizi wa Premier League.Amesema ameshawaonya The Blues kwa maandishi kuacha kumshawishi Modric na sasa anawashutumu Chelsea kutangaza ofa hadharani ili kumchanganya Luka.

Chelsea ambao wana kashfa za kufanya mipango ya usajili isivyo halali, mwaka 2005 walipigwa faini ya paundi 300000 na wakapewa adhabu ya kukatwa pointi 3 na kamati ya Premier League baada ya kufanya mazungumzo kinyume na sheria ya kutaka kumsaini Ashley Cole.

Pia waliwahi kukutwa na hatia na FIFA kwa kufanya makubaliano kinyume na sheria na Gael Kakuta na wakapewa adhabu ya kutokufanya usajili wa kimataifa kwa miaka 3 lakini baadae adhabu hiyo ilifutwa.

Spurs wanatarajiwa kupeleka mashtaka kwa kamati ya ligi kuu, na matokeo ya mashtaka hayo yanaweza kuwa mabaya kwa Chelsea kutokana na rekodi yao chafu.

Modric jana alijitokeza na kusema anataka kuondoka Spurs mahali ambapo bado ana mkataba wa miaka 5 akiwa analipwa paundi 42000 kwa wiki.

Inaaminika kuwa ikiwa Chelsea wakifanikiwa kumsaini mchezaji huyo basi atakuwa anaweka kibindono paundi 150,000 kwa wiki.



1 comment:

  1. shaffhi embu tupe habari za arsenal kuna mwingine yoyote aliye sajiliwa

    ReplyDelete