Kwa upande wa Kikapu nimekua mpenzi mkubwa sana wa ligi ya NBA,usiku wa kuamkia leo Draft za NBA zimefanyika, kwa mtazamo wangu nimetengeneza top 10 drafts of all time.
1.Ervin ‘magic’ Johnson, LA LAKERS .1979. Magic anaaminika kuwa mtu aliyeubadilisha mchezo wa kikapu kwa upande wa biashara . Hii ni kutokana na upinzani wake na nyota mwingine Larry Bird , upinzani ambao ulikuwa sawa na upinzani wa kanda ya mashariki na kanda ya magharibi . Upinzani huu uliipa ligi ya NBA umaarufu mkubwa kama kampuni ya kibiashara .
2.Bill Russell,Boston Celtics,1956.Bill Russell ni moja kati ya draft bora za miaka yote kwenye NBA . Sababu kubwa ni jinsi alivyoweza kuunganisha juhudi ,kipaji na uwezo binafsi sambamba na majukumu ya uongozi kwenye timu yake ya Boston Celtics . Chini ya Russell Celtics waliweza kutwaa taji la NBA mara 11 kwenye misimu 13 .
3.Michael ‘mj’ Jordan ,CHICAGO BULLS ,1984. Hakuna anayejua kwanini timu ya Portland Trail Blazers ambayo ilikuwa na nafasi ya kumchagua Jordan iliamua kuachana naye na kumchagua mtu mwingine Sam Bowie kwenye nafasi ya pili waliyokuwa nayo ya kuchagua mchezaji mwaka 84,Houston Rockets walimchagua Hakeem Olajuwon mwaka huo huo kwenye nafasi ya kwanza . Kimsingi walichokosa Blazers kilikuwa faida ya bulls kwani chini ya Jordan Bulls waliweza kutengeneza historian a Jordan mwenyewe alijiwekea historia yake binafsi si tu kama mchezaji wa NBA bali mwanamichezo maarufu kuliko wote ulimwenguni.
4. David Cowens,Boston Celtics ,1970. Huyu ni mmoja wa wachezaji waliojishindia tuzo lukuki wakati wake kwenye NBA , Cowens aliweza kurithi vyema nafasi ya Bill Russell kwenye timu ya Boston Celtics akiwaongoza kutwaa mataji mawili ya NBA .
5. Kevin Garnett,MINESOTTA TIMBERWOLVES ,1995. Minesotta walionekana kama wanafanya mchezo wa hatari kumsajili mtu ambaye hana uzoefu wa mashindano ya vyuo NCAA , lakini mwishowe haikuwa hivyo kwani Garnett au KG kama mashabiki wa kikapu wanavyomuita aliiishia kuwa mmoja wa wachezaji bora wa nafasi yake , Garnett alikuja kutwaa ubingwa wa NBA kwa mara ya kwanza akiwa na Boston Celtics mwaka 2008.

7.Dirk Nowitzki,Milwaukee Bucks , 1998. Dirk Nowitzki alichaguliwa na timu ya Milwaukee Bucks lakini kwenye siku hiyo hiyo ya Draft Dallas walimbadili na Robert Taylor waliyemchagua kwenye nafasi ya Sita na kumchukua Nowitzki . Uwezo mkubwa alio nao Dirk wa kutupa mitupo ya point tatu ulibadili kabisa mtazamo wa NBA na mchezo wa kikapu kwa ujumla kwa nafasi ya power forward . Dirk aliiongoza Dallas kufika fainali ya NBA mwaka 2006 ambapo alichaguliwa kuwa MVP kwa mwaka uliofuata na mwaka huu kwa msimu ulioisha aliiongoza Dallas Mavericks kutwaa ubingwa wa NBA huku akichaguliwa tena kuwa MVP .

9.Reggie Miller,INDIANA PACERS ,1987.Reggie Miller ni mmoja kati ya watupa 3 pointers bora wa miaka yote na alikuwemo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya marekani Dream Team kwa miaka mingi na alikuwa anachezeshwa kwa jukumu la kufunga 3 pointers tu .
10.Jullius ‘dr J’ Erving , Milwaukee Bucks ,1972.Dr J angeweza kuwa timu moja na gwiji Kareem Abdul Jabar lakini mwishowe aliishia kuwa Philadelphia 76ers ambako aliweza kutwaa ubingwa wa NBA pamoja na tuzo ya MVP.

No comments:
Post a Comment