Search This Blog

Monday, August 27, 2012

BHAAAAASI: SERENGETI FIESTA BONANZA YATINGISHA JIJI LA MAHABA TANGA - WEMA SEPETU NA WENZIE WA BONGO MOVIE WATISHA

Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego pichani kati mwenye kipaza sauti akisoma namba za washindi waliojinyakulia piki piki mbili zilizotolewa na kampuni ya Push Mobile, wa tatu kulia ni Meneja Masoko wa kampuni ya Push Mobile,Rugambo Rodney na mwisho kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Clouds Media Group,Joseph Kusaga,na nyuma kabisa ni Mkurugenzi wa utafiti Clouds Media Group, Ruge Mutahaba pamoja na Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti,Ephrahim Mafuru wakishuhudia tukio hilo usiku huu kwenye uwanja wa Mkwakwani ambako tamasha la Serengeti Fiesta 2012 linafanyika.
Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Clouds Media Group, Joseph Kusaga usiku huu mara baada ya kuwataja washindi waliojishindia piki piki mara baada ya kuchezeshwa bahati nasibu,wakati tamasha la Serengeti Fiesta 2012 likiendelea,pichani kati ni Afisa Mahusiano wa Clouds Media Group, Simon Simalenga.
Steve Nyerere & Shilole kazi ipo.......
Shilole & JB
FA & Linah ni Yalait au kunamengine??? LOL!
Wema,Aunt & Shilole....Mmmmmmh! Hapa sitii neno
Bhaaaasss!  Mchomvu akitema cheche.....
Dj-Zero Babyyyyyyyyyyyyyyy
Rachael.....
Rais wa Masharobaro Bob Junior akishambulia jukwaa....
CMB Prezzo 4rom Kenya Bhaaasss!
Mwana FA ndani.....
Shetta wa Darstamina kwa steji akidanganywadanganywa... Hahahaha!

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Nuru akitumbuiza jukwaani usiku huu na shabiki wake mbele ya wakazi wa jiji la Tanga wanaondelea kutiririka ndani ya uwanja wa Mkwakwani ambako tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
Msanii kutoka THT,ajae kwa kasi katika anga ya muziki wa bongofleva aitwaye Rachel akiimba jukwaani usiku huu.
Msanii kutoka THT,ajae kwa kasi katika anga ya muziki wa bongofleva aitwaye Rachel akiimba jukwaani usiku huu.
Pichani shoto ni Mkurugenzi wa Masoko, Ephrahim Mafuru, Mkuu wa Vipindi Clouds FM,Sebastian Maganga sambamba na Meneja wa bia ya Serengeti,Allan Chonjo wakiwa katika picha ya pamoja ndani ya uwanja wa Mkwakwani wakati tamasha la Serengeti Fiesta likiendelea kurindima.
Dj Zero kutoka Clouds FM akikamua.
Sehemu ya umati wa wakazi wa Tanga wakifuatilia kwa makini makamuzi ya Fiesta usiku huu.
Moja ya zao la Supa Nyota kutoka Mkoani Mbeya akiimba jukwaani.
 Mambo ya Fiesta Serengeti 2012 ndani ya Jiji La Tanga.
 Show Love.
 Mkuu wa vipindi wa Clouds Fm Sebastian Maganga akitoa maelezo machache kwa Mtangazaji Millard Ayo wakati wakirusha matangazo live ndani ya Tanga.
 The Dream Team ya Clouds Fm.
 Mtangazaji Millard Ayo akifanya mahojiano na Sam Baruti.
 Mtangazaji Millard Ayo akiongea na wakazi wa Tanga.
 Mwanadada Loveness Love akiongea machache na wakazi wa Tanga.
 ...wakazi wa Tanga walijishindia zawadi mbali mbali ikiwemo t-shirt na tiketi za bure.
 Kwenye moja na mbili toka ndani ya viwanja vya Tangamano.
 
 
PICHA NA http://www.kajunason.blogspot.com/

GOLI LA SIKU: OSVALDO NA GOLI LA KUSAWAZISHA LA AS ROMA


ROMA - Catania (OSVALDO SUPERGOAL) by asroma-ks

REAL MADRID YAPIGWA NA GETAFE - WAPITWA POINTI 5 NA BARCA


Getafe - Real Madrid footyroom.com by footyroom

LIONEL MESSI APIGA GOLI MBILI NA KUIPA BARCA USHINDI MGUMU DHIDI YA OSASUNA


Osasuna - Barcelona footyroom.com by footyroom

ROBERTO MANCINI ASEMA ANFIELD SIO MAHALA PAZURI KWENDA - MAN CITY IKIOKOKA KUFUNGWA NA LIVERPOOL


L-M footyroom.com by footyroom

Sunday, August 26, 2012

NO RVP & STILL NO GOALS: ARSENAL WASHINDWA KUFUNGA BAO KATIKA MECHI YA PILI: YATOKA SARE NA STOKE


S0-0A www.fasthighlights.com by fasthighlights-2012

SABABU 5 KWANINI LIGI KUU YA ENGLAND NDIO BORA DUNIANI




Inapewa sifa kuliko inavyostahili? Labda. Lakini kuna sababu kwanini English Premier League inaonekana kwa upana zaidi kama ligi bora kabisa ya ndani ya nchi duniani kote.

Huku ikiwa na miaka 20 tangu kuanza kwake, Premier league imekuwa chombo kilichobadilishwa namna soka inavyoangaliwa, mpaka inavyochezwa.

Premier league ilizaliwa mwaka 1992 kutokana na matamanio ya vilabu vikubwa vya England kupata faida kubwa kutokana na haki za matangazo ya Televison.

Ulikuwa ni muda ambao soka la England lilikuwa linatoka kwenye muda ambao ulikuwa ni giza la uhuni, ukosefu wa mashabiki viwanjani na ukosefu wa mvuto.

Huku kukiwa na uwepo wa fedha nyingi, utangazwaji na hamu ya kutaka kuiteka dunia, Premier league inaendelea kuitawala tasnia ya soka duniani leo hii.

Hizi ndio sababu 5  kwanini Premier League ndio ligi bora duniani.


WINGI WA UPINZANI WA VILABU VYA NDANI

 
England ndio nchi inayoongoza kwa kuwa na vilabu vya juu, ambavyo vinatoa utajiri wa wingi wa upinzani wa vilabu vya ndani.

Kuna kipute cha upinzani cha London ya kaskazini, kipute cha upinzani wa mji Birmigham na vipute vingine kibao vya ndani ya nchi hiyo....OK, kati ya mechi hizi hakuna inayoweza kuifikia utamu wa kipute kati ya Real Madrid dhidi ya Barcelona, au Boca Juniors dhidi ya River Plate - lakini kikubwa zaidi kuna mechi mbili tu kwa msimu zinazohusisha upinzani mkubwa, tofauti na England ambapo kila wiki kuna uwezekano wa kuangalia mechi ya upinzani wa juu.

 MECHI KUTOKUTABIRIKA

 
Moja ya sababu kubwa nyingine inayoipa ubora ligi kuu ya England ni kutokutabirika kwa mechi.

Japokuwa ni ukweli kwamba ni vigumu kwa timu kama Southmpton kuwa mabingwa bila msaada wa matajiri wenye za kutupa kama akina Shekhe Mansour , lakini premier league bado inatoa level ya juu ya suhindani kutofautisha na ligi nyingine duniani.

Imekuwa kitu cha kawaida sana kuona Manchester United ikifungwa na timu ndogo au ikipata shida sana kupata japo sare. Tofauti na Spain ambapo inapocheza Barelona na Recreativo Huelva unajua leo Lionel Messi anatupia hat trick ngapi, lakini ni vigumu kufikiri hivyo inapocheza Chelsea na Reading au Manchester City na QPR.



Ikumbukwe moja ya mechi zilizosababisha Manchester United kukosa ubingwa kwenye dakika za mwisho ilikuwa dhidi ya timu iliyokuwa ikipambana kushuka daraja Wigan, - Ni vigumu kuona Real Madrid wanafungwa na timu inayoshika mkia kwenye la liga.

UPINZANI WA VILABU VIKUBWA

 
Mbali wa upinzani mkubwa timu zinazotoka sehemu moja: mfano Aston Villa vs Birmigham. Pia kuna wingi wa upinzani wa vilabu vikubwa.

England kuna utamu wa Mechi mbili za Manchester United dhidi ya Man City, Liverpool vs United, Arsenal vs Chelsea, Tottenham vs United, Arsenal vs Tottenham, United vs Chelsea,Tottenham vs City, Arsenal vs United, City vs ARsenal na nyingine kibao.

Mechi za namna hii ni vigumu kupata kwenye ligi nyinginezo duniani.


 USHINDANI

 
Moja ya hoja wanazotoa wapinzani wa Premier league ni ukosefu wa ushindani, hoja ambayo inakuja kutokana na ligi kuu ya England tangu uanzishwa kwake Manchester United imechukua ubingwa mara 12 kati ya 20.

Lakini hao hao United wamekuwa sio watawala wa ligi kuu ya England wamekuwa wakifanya vizuri sana kwenye mashindano ya kimataifa. Katika cha miaka mitano iliopita United wamecheza fainali 3 za champions league. Hii inaonyesha ni kiasi gani England inatoa bingwa sahihi.

Premier league pia imekuwa ikitoa nyingi kwenye mashindano ya kimataifa ambazo zimekuwa zikifanya vizuri.

Mwaka jana Manchester City ilikuwa ni klabu ya tano kushinda ubingwa wa EPL. Mabingwa watano tofauti kwenye kipindi cha miaka 20. Huu ni uwiano mzuri wa ushindani. Sasa Angalia ligi ya Spain, kwenye kipindi cha miaka 20 iliyopita imetoa mabingwa wanne, huku katika katika historia ya ligi hiyo tangu kuanzishwa kwake miaka 90 iliyopita imetoa mabingwa tisa tu.

MAFANIKIO YA ULAYA

 
Moja ya sababu kubwa ya kufanya mapinduzi ya kuileta Premier League ilikuwa ni kuleta upinzani mkubwa  ambao ungetosha kuwafanya kuitawala soka la bara la ulaya.

Ilichukua miaka kadhaa, lakini kwa sasa inaonekana wamefanikiwa vizuri sana.

Makombe manne kati ya 20 ya champions league yamechukuliwa na vilabu vya Premier League, matatu kati ya hayo ndani ya miaka 10 iliyopita. Fainali tano za champions league zilizopita zimekuwa zikihusisha vilabu vya England - United na Chelsea.

Kama, wengi wanavyosema kwamba Champions league ndio roho ya ubora wa soka, basi Premier league inastahili kuitwa ligi bora duniani.

By Aidan Seif Charlie

PHOTOS: SIMBA WATEMBELEA KIWANDA CHA TBL ARUSHA

Mratibu wa Usalama na Afya wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kassena Heavy, akiwaeleza jambo wachezaji na viongozi wa klabu ya Simba waliotembelea kiwanda cha TBL kilichopo Arusha mwishoni mwa wiki ili kujionea uzalishaji wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager ambayo ndio mdhamini wao mkuu.

Meneja wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe akiongea na wachezaji na viongozi wa klabu ya Simba waliotembelea kiwanda cha TBL kilichopo Arusha mwishoni mwa wiki ili kujionea uzalishaji wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager ambayo ndio mdhamini wao mkuu.

Meneja wa Mauzo wa Kanda ya Kaskazini wa kampuni ya bia Tanzania (TBL), Kasiro Msangi akiongea na wachezaji na viongozi wa klabu ya Simba waliotembelea kiwanda cha TBL kilichopo Arusha mwishoni mwa wiki ili kujionea uzalishaji wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager ambayo ndio mdhamini wao mkuu.

Wachezaji na viongozi wa klabu ya Simba wakitembelea kiwanda cha TBL kilichopo Arusha mwishoni mwa wiki ili kujionea uzalishaji wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager ambayo ndio mdhamini wao mkuu.

Mratibu wa Usalama na Afya wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kassena Heavy, akiwaeleza jambo wachezaji na viongozi wa klabu ya Simba waliotembelea kiwanda cha TBL kilichopo Arusha mwishoni mwa wiki ili kujionea uzalishaji wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager ambayo ndio mdhamini wao mkuu.

Kocha Mkuu wa Simba, Profesa Milovan Cirkovic akiongea na Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe kwenye hafla iliyofanyika baada ya wachezaji na viongozi wa klabu ya Simba kutembelea kiwanda cha TBL kilichopo Arusha mwishoni mwa wiki ili kujionea uzalishaji wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager ambayo ndio mdhamini wao mkuu.

Wachezaji na viongozi wa klabu ya Simba wakitembelea kiwanda cha TBL kilichopo Arusha mwishoni mwa wiki ili kujionea uzalishaji wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager ambayo ndio mdhamini wao mkuu.

Mshambuliaji hatari wa Simba, Mrisho Ngassa akisalimia wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL)

Wechezaji wa klabu ya Simba wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kilichopo Arusha mwishoni mwa wiki ili kujionea uzalishaji wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager

Kocha Mkuu wa Simba, Profesa Milovan Cirkovic akitoa neon la shukrani baada ya wachezaji na viongozi wa klabu ya Simba kutembelea kiwanda cha TBL kilichopo Arusha

Wechezaji wa klabu ya Simba wakiwa katika picha ya pamoja na viongozii wa kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kilichopo Arusha

  1. Wechezaji wa klabu ya Simba wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kilichopo Arusha mwishoni mwa wiki ili kujionea uzalishaji wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager ambayo ndio mdhamini wao mkuu. (Picha: Executive Solutions)


LIVERPOOL YAIPIGA BAO ARSENAL: YAMTWAA NURI SAHIN, ATAMBULISHWA RASMI




ANGALIA VIDEO ZINAZOONYESHA UWEZO WA KIJANA HUYU WA KITURUKI

HAZARD AZIDI KUTISHA - TORRES AWEKA KAMBANI TENA, CHELSEA IKIUA NEWCASTLE 2-0