Search This Blog

Thursday, May 3, 2012

LIONEL MESSI AVUNJA REKODI YA GERD MULLER - AFUNGA MAGOLI 68 NDANI YA MSIMU MMOJA


Barcelona vs Malaga 4-1 Full Match Highlights... by kofiswag

Lionel Messi kwa mara nyingine tena amefunga mabao matatu peke yake, Barcelona ikishinda 4-1 dhidi ya Malaga Uwanja wa Camp Nou usiku huu.

Carles Puyol alifunga bao la kwanza kabla ya Messi kufunga mfululizo.
Messi sasa ametimiza mabao 68 katika mashindano yote msimu huu na kuvunja rekodi ya Mjerumani Gerd Muller ya kufunga mabao mengi msimu mmoja katika Ligi kubwa Ulaya.

ITSSSSSSSSSSSSSSSS PAPISS DEMBA CISSE - CHELSEA HALI YAZIDI KUWA MBAYA EPL - WATANDIKWA 2-0 NA NEWCASTLE


Chelsea vs Newcastle 0:2 GOALS HIGHLIGHTS by maidb7abc

TOTTENHAM WARUDI KWENYE MSTARI - WAIPIGILIA BOLTON 4-1 HUKU MUAMBA AKITOKWA NA MACHOZI

Emotional: Muamba at the Reebok
Fabirce Muamba akisalimia mashabiki huku machozi yakimtoka kabla ya mechi kati ya Bolton na Tottenham.





Tearful: Muamba shows his emotion
Thank you: Muamba acknowledged the fans for their support



Bolton vs Tottenham 1:4 GOALS HIGHLIGHTS by maidb7abc

REAL MADRID MABINGWA WA LA LIGA BAADA YA UTAWALA WA MIAKA MINNE YA BARCELONA





Real Madrid Title Celebration At Final whistle... by kofiswag


Athletic Bilbao vs Real Madrid 0-3 All goals and... by kofiswag

Wednesday, May 2, 2012

6-0 ZA 1977 DONDA NDUGU YANGA




Kikosi hatari cha Simba kilichoipiga Yanga 6-0, wa tatu kutoka kulia waliosimama  ni King Kibadeni aliyepiga hat trick, rekodi ambayo haijavunjwa hadi leo kwenye mechi za watani

MGOGORO wa mwaka 1976 ulioibuka na kuigawa Yanga hadi kuzaliwa Pan African, ulisababisha athari nyingine kadhaa za kihistoria kwenye klabu hiyo, zaidi ya mgawanyiko huo.
Baada ya mgogoro wa Yanga Kandambili na Yanga Raizoni, rasilimali nyingi za klabu hiyo, yakiwemo mabasi ziliteketea. Lakini pengine hilo inawezekana lisiwaumize sana wana Yanga, kuliko kipigo kutoka kwa watani wao wa jadi, Simba, cha mabao 6-0.
Baada ya mgogoro huo, kwa sababu wachezaji wote walimfuata mzee Tarbu Mangara aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu hiyo, Yanga walilazimika kuunda upya timu yao, wakisajili wachezaji wapya. Tangu mwaka 1977, Yanga walikuwa vibonde wa Simba hadi mwaka 1981, walipojikomboa.
Tangu kuanzishwa kwa Ligi ya Tanzania, mwaka 1965 hadi mwaka 1976 Yanga inakutwa na mgogoro huo, ilikuwa imekutana na watani wao wa jadi, Simba kwenye mechi 10. Katika mechi hizo, Yanga walishinda saba, Simba waliibuka kidedea mara mbili na mara moja ilikuwa ni sare. 
Kati ya mara saba ambazo Yanga iliifunga Simba, ndani yake kuna kipigo cha mabao 5-0, Juni Mosi mwaka 1968, enzi hizo Simba bado ikiitwa Sunderland.
Siku hiyo, mabao ya Yanga yalitiwa kimiani na Maulid Dilunga dakika za 18 kwa penalti na 43, wakati mengine yalifungwa na Salehe Zimbwe dakika za 54 na 89 na kuhitimisha karamu ya mabao, lilifungwa na Kitwana Manara 'Popat' dakika ya 86.
Kwa homa ya kipigo hicho, kwenye mchezo uliofuata Machi 3, mwaka 1969, Simba waliishia njiani maeneo ya Chang'ombe na kurejea klabuni kwao, wakihofia kutandikwa zaidi, hivyo watani wao wa jadi, kupewa pointi za chee.
Baada ya hapo, timu hazikukutana hadi Juni 4, mwaka 1972, Simba wakiwa madhubuti tayari kuweza kuhimili vishindo vya Yanga. Katika mchezo huo, timu hizo zilitoka sare ya 1-1, tena Sunderland ikitangulia kupata bao kupitia mshambuliaji wake, Willy Mwaijibe, dakika ya 11, kabla ya Kitwana Manara kusawazisha dakika nane baadaye.
Juni 18, mwaka huo huo 1972, timu hizo zilikutana tena na bao pekee la Leonard Chitete (sasa marehemu) lilitosha kuendeleza ubabe wa Yanga kwa Simba.
Haidari Abeid 'Muchacho' alikomesha tabia ya Simba kufungwafungwa na Yanga, katika mechi baina ya watani hao wa jadi, Juni 23, mwaka 1973, akifunga bao pekee lililowalaza mapema wana Jangwani, dakika ya 68.
Wakati Simba ikiamini imekwishapata dawa ya Yanga, Agosti 10, mwaka 1974 katika mchezo uliowakutanisha watani hao wa jadi nje ya Dar es Salaam, kwa mara ya kwanza, Uwanja wa Nyamagana mjini Mwanza, Wekundu wa Msimbazi walikiona cha moto.
Wekundu wa Msimbazi walianza vizuri kwa kuwatungua Yanga bao la mapema dakika ya 16 tu ya mchezo, mfungaji akiwa ni Adamu Sabu. Lakini zikiwa zimesalia dakika tatu mchezo kumalizika, mjini Dar es Salaam, mashabiki wa Simba wakiwa wamekwishajikusanya kuanza misafara ya kuelekea makao makuu ya klabu hiyo, Mtaa wa Msimbazi kushangilia ushindi, walikuwa wanyonge ghafla baada ya mtangazaji wa Radio Tanzania (RTD), Ahmad Jongo kutangaza bao la kusawazisha la Gibson Sembuli (sasa marehemu).
Kwa bao hilo, mchezo huo kwa sababu ulikuwa wa kuamua bingwa, ilibidi uhamie kwenye dakika 30 za nyongeza. Dakika ya saba Sunday Manara aliwainua vitini mashabiki wa Yanga waliokuwa Nyamagana kwa kufunga bao la pili. Naam, huo ulikuwa ushindi wa mwisho wa Yanga kwa Simba, kwani baada ya hapo, mgogoro wa Yanga Kandambili na Yanga Raizoni uliitafuna klabu hiyo.
Hatimaye ikawadia siku chungu zaidi katika maisha ya Yanga kwenye utani wao na Simba, ilikuwa ni Julai 19, mwaka 1977 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, enzi hizo Simba ikinolewa na Mbulgaria, Dimitar Samsarov.
Simba ikiwa na 'mziki' wake ule ule uliokuwa ukichuana na Yanga tangu mwaka 1974, ilikutana na Yanga mpya kabisa iliyoundwa na wachezaji kama kipa aliyekuwa Mwadui ya Shinyanga, Bernard Madale.
Yanga walishindwa kuimudu kasi ya Simba na kujikuta wakitandikwa mabao 6-0, mabao ya Wekundu wa Msimbazi yakitiwa kimiani na Abdallah Kibadeni katika dakika za 10, 42 na 89, Jumanne Hassan 'Masimenti' dakika za 60 na 73, wakati Selemani Sanga alijifunga mwenyewe dakika ya 20. Kipigo hicho kilikuwa sababu tosha ya kipa Madale kutupiwa virago Jangwani.
Lakini Yanga iliendelea kuchezea vipigo tu walipokutana na Simba, japokuwa Oktoba 7, mwaka 1979 walipunguziwa dozi kwa kiwango cha nusu nzima, kutoka bao sita hadi tatu.
Yanga ilichapwa 3-1 siku hiyo, mabao ya Simba yakifungwa na Nico Njohole dakika ya tatu, Mohammed Bakari 'Tall' dakika ya 38 na Abbas Dilunga dakika ya 72, wakati lile la kufutia machozi la Yanga lilifungwa na Rashidi Hanzuruni dakika ya nne.
Oktoba 4, mwaka 1980, Yanga ilipigwa tena 'nusu dozi' ya 6-0, mabao ya wana Msimbazi yakitiwa kimiani na Abdallah Mwinyimkuu dakika ya 29, Thuwein Ally dakika ya 82 na Nico Njohole dakika ya 83.
Hatimaye saa ya ukombozi iliwadia Jangwani, Juma Hassan Mkambi akiitwa 'Jenerali' enzi zake alikomesha uteja wa Yanga kwa Simba, Septemba 5, mwaka 1981, kwa bao lake pekee dakika ya 42. Siku hiyo, mabeki wa Yanga walifanya kazi kubwa ya kulinda bao hadi dakika 90 zilipotimia, wana Jangwani wanainua mwali wao.
Naam, Mkambi alifuta uteja wa Yanga kwa Simba na kuanzisha rasmi enzi za Jangwani kuwanyima raha wana Msimbazi, kwani katika mechi iliyofuata, Aprili 29, mwaka 1982, bao la Rashid Hanzuruni dakika ya pili tu ya mchezo liliifanya Simba ilale tena 1-0.
Hiyo ilikuwa mechi ya kwanza kuwakutanisha watani wa jadi, tangu kuanza kwa Ligi ya Bara kutoka Klabu Bingwa ya Taifa na katika mchezo wa marudiano, Simba walikiona tena cha moto, walitandikwa 3-0, Septemba 18, mwaka huo, 1982.
Mabao ya Yanga siku hiyo yalitiwa kimiani na Omar Hussein 'Keegan'
katika dakika ya pili na ya 85, wakati lingine lilifungwa na Makumbi Juma 'Homa ya Jiji' au 'Bonga Bonga' dakika ya 62.
Tangu hapo, Yanga iliitesa Simba kwa miaka sita mfululizo, hadi ilipokuja kujikomboa Agosti 23, mwaka 1986 kwa ushindi wa mabao 2-1, wafungaji wakiwa ni marehemu Edward Chumila, dakika ya tisa na Malota Soma dakika ya 51. Siku hiyo Omar Hussein alitangulia kuifungia Yanga bao dakika ya 5.
Februari 10, mwaka 1983, timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana na kwenye mchezo wa marudiano, Aprili 16, mwaka huo, Yanga ilishinda 3-1, mabao yake yakitiwa kimiani na Charles Boniface Mkwasa dakika ya 21, Makumbi Juma dakika ya 38 na Omar Hussein dakika ya 84, wakati la kufutia machozi la Simba lilifungwa na marehemu 'Super' Kihwelo Mussa dakika ya 14.
Septemba 10, mwaka 1983, Yanga iliichapa Simba 2-0, wafungaji wakiwa ni Lila Shomari aliyejifunga dakika ya 72, kabla ya Ahmad Amasha kufunga la pili dakika ya 89, wakati kwenye mechi ya marudiano, Septemba 25, mwaka huo, timu hizo zilitoka sare ya 1-1. Sunday Juma 'Pikipiki' alitangulia kuifungia Simba bao dakika ya 72, kabla ya Makumbi Juma kusawazisha dakika tatu baadaye, dakika ya 75.
Machi 10, mwaka 1984, timu hizo zilitoka 1-1 tena, kipa Iddi Pazi 'Father' akitangulia kuifungia Simba bao kwa mkwaju wa penalti dakika ya 20, kabla ya Omar Hussein kusawazisha dakika ya 72.
Julai 14, mwaka 1984, mdudu wa sare aliendelea kutawala kwa watani wa jadi, kwani zilitoka 1-1 tena, Zamoyoni Mogella 'Golden Boy' akitangulia kuifungia Simba dakika ya 17, kabla ya Abeid Mziba 'Tekero' kusawazisha dakika ya 39.
Mei 19, mwaka 1985 mchezo ulimalizika kwa sare ya 1-1 tena, Omar Hussein akianza kuifungia Yanga dakika ya sita kabla ya Mohammed Bob Chopa kuisawazishia Simba dakika ya 30.
Yanga ilirejesha enzi za ubabe Agosti 10, mwaka 1985, ilipopewa pointi za chee, baada ya Simba kutoroka uwanjani ikigomea adhabu ya penalti, wakati Machi 15, mwaka 1986 zilitoka sare ya 1-1 tena, John Hassan Douglas akitangulia kuifungia Simba dakika ya 20, kabla ya Abeid Mziba kusawazisha dakika ya 44.
Katika mchezo wa marudiano, Agosti 23, 1986 ndiyo Chumila na Malota walizima ubabe wa Yanga kwa Simba rasmi.
Baada ya hapo, timu hizo zilikuwa zikifungana kwa zamu, ingawa kipigo kikali zaidi kilikwenda kwa Yanga, Julai 2, mwaka 1994, wakati Simba waliposhinda 4-1.
Hata hivyo, baada ya mchezo huo, Yanga ilivunja tena kikosi kutokana na tuhuma za kuhujumiwa na wachezaji wake, safari hiyo ikidaiwa aliyekuwa mfadhili mmoja wa klabu hiyo mwenye asili ya Kiasia, aliwapa fedha wachezaji wafungwe ili kuwakomoa viongozi katika vita iliyokuwa inaendelea baina yao.
Baadhi ya wachezaji waliobakishwa kikosini walikuwa ni Kenneth Mkapa, Constantine Kimanda, Sekilojo Chambua, Sanifu Lazaro ‘Tingisha’ na Mohammed Hussein ‘Mmachinga’, wengine wote walitimuliwa kwa tuhuma hizo.
Baada ya hapo, Yanga iliundwa na wachezaji waliokuwa wakiandaliwa na Tambwe Leya (sasa marehemu) katika kikosi cha pili, ambao ni pamoja na Godwin Mashoto (sasa marehemu), Mzee Abdallah, Anwar Awadh, Maalim Saleh ‘Romario’, Nonda Shaaban na wengineo, waliosajiliwa kutoka timu mbalimbali kuimarisha kikosi kama Bakari Malima, Reuben Mgaza waliotoka Pan African.
Baada ya hapo, Simba ilirejesha utemi wake kwa Yanga kwa kuifunga mfululizo tangu mwaka 2004 hadi ilipojikomboa Oktoba 26, mwaka 2008, kwa bao pekee la Ben Mwalala dakika ya 15 ya mchezo huo, Uwanja mpya wa Taifa, Dar es Salaam.
Yanga ilikuwa imeifunga Simba kwa mara ya mwisho katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Aprili 20, mwaka 2003, Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza, mabao 3-0 yaliyotiwa kimiani na Heri Morris, Salum Athumani na Kudra Omar.
Katika Ligi Kuu, Yanga ilikuwa imeifunga Simba kwa mara ya mwisho Agosti 5, mwaka 2000, mabao 2-0 yote yakifungwa na Iddi Moshi Shaaban, anayechezea Villa Squad kwa sasa.
Moshi, aliyekuwa anacheza kwa mara ya kwanza tangu ametoka kwenye fungate la ndoa yake, alifunga mabao hayo katika dakika za 37 na 47, wakati kwenye mechi iliyofuata Septemba 1, mwaka 2001, bao pekee la Joseph Kaniki 'Golota' katika dakika ya 76 liliinyima raha Yanga siku hiyo.
Sekilojo Chambua, ambaye kwa sasa ni kocha, aliinusuru Yanga kulala tena mbele ya Simba Septemba 30, mwaka 2001, baada ya kuifungia bao la kusawazisha dakika ya 86, kufuatia Kaniki tena kutangulia kufunga dakika ya 65 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Agosti 18, mwaka 2002, Chambua tena aliinusuru Yanga kulala, baada ya mwamuzi Victor Mwandike kuipa timu hiyo penalti dakika ya 89 na kiungo huyo wa zamani kuukwamisha mpira kimiani.
Awali ya hapo, mkongwe Madaraka Suleiman 'Mzee wa Kiminyio', alitangulia kuifungia Simba bao dakika ya 65, wakati mechi ya marudiano Novemba 10, mwaka huo, timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana.
Septemba 28, mwaka 2003, mabao ya Kudra Omary dakika ya 42 na Heri Morris dakika ya 55, yaliinusuru Yanga kulala 2-0 mbele ya Simba, kufuatia Emanuel Gabriel kufunga mapema katika dakika za 27 na 36, wakati kwenye mchezo wa marudiano Novemba 2, mwaka huo, timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana.
Agosti 7, mwaka 2004, Shaaban Kisiga alitangulia kuifungia Simba dakika ya 64, kabla ya Pitchou Kongo kusawazisha dakika tatu tangu kuanza kipindi cha pili na Ulimboka Mwakingwe kufunga bao la ushindi dakika ya 76.
Bao pekee la Athumani Machuppa katika dakika ya 82, liliipa ushindi wa 1-0 Simba dhidi ya Yanga Septemba 18, mwaka 2004, wakati Aprili 17, mwaka 2005 kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, Aaron Mwinura Nyanda alitangulia kuifungia Yanga dakika ya 39, kabla ya Nurdin Msiga kuisawazishia Simba dakika ya 44 na Machuppa kufunga la pili dakika ya 64.
Kwenye mchezo wa marudiano, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha uliofanyika Agosti 21, mwaka 2005, Nicodemus Nyagawa aliibuka nyota wa mchezo baada ya kufunga mabao yote mawili yaliyoipa Simba ushindi wa 2-0 dhidi ya Yanga, dakika za 22 na 56.
Machi 26, mwaka 2006, baada ya Yanga kuimarisha kidogo kikosi chake, ilianza kugoma kufungwa kwa kulazimisha sare ya bila kufungana na Simba kama ilivyokuwa kwenye mchezo wa marudiano Oktoba 29, mwaka huo, mechi zote zikichezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Julai 8, mwaka 2007 katika fainali ya Ligi ndogo ya Bara, Moses Odhiambo alitangulia kuifungia Simba kwa mkwaju wa penalti dakika ya pili tu ya mchezo, kabla ya Said Maulid 'SMG' kufunga la kusawazisha dakika ya 55.
Mchezo huo ulihamia kwenye mikwaju ya penalti na Simba ilishinda kwa mikwaju ya penalti 5-4 baada ya sare hiyo.
Oktoba 24 mwaka 2008, kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, Simba wakicheza 10 baada ya Henry Joseph kutolewa kwa kadi nyekundu mapema tu dakika ya sita, iliibuka na ushindi wa bao 1-0, lililotiwa kimiani na Ulimboka Mwakingwe dakika ya 23.
Aprili 27 mwaka 2009 katika mchezo wa marudiano wa Ligi Kuu, timu zilitoka sare ya bila kufungana na Oktoba 26, mwaka 2008, Ben Mwalala alifunga bao dakika ya 15, ambalo lilidumu hadi mwisho wa mchezo, hivyo kuifutia Yanga uteja uliodumu tangu mwaka 2004.
Bao la Mwalala lilikuwa la kishujaa na la kihistoria kama ilivyokuwa kwa Jenerali Mkambi, Septemba 5, mwaka 1981.
Katika mchezo wa marudiano kwenye Ligi hiyo, baina ya watani hao wa jadi, Aprili 19, mwaka 2009 Yanga ilinusurika kulala 2-1, kama si bao la Jerry Tegete dakika ya 90.
Ramadhan Chombo 'Redondo' alitangulia kuifungia Simba kwa kichwa dakika ya 23, kabla ya Mwalala kusawazisha dakika ya 48 kwa shuti lililowababatiza mabeki na kutinga nyavuni. Haruna Moshi 'Boban' aliifungia Simba bao lililoelekea kuwa la ushindi dakika ya 62, kabla ya Tegete kuzima shangwe za wana Msimbazi, tena ndani ya dakika za lala salama.
Oktoba 31, mwaka 2009, bao pekee la Mussa Hassa Mgosi katika dakika ya 26, lilitosha kuipa Simba ushindi wa 1-0 dhidi ya Yanga, Uwanja mpya wa Taifa, Dar es Salaam, wakati Aprili 18, mwaka 2010 ilikuwa funga nikufunge kabla ya Weikundu wa Msimbazi kutoka kifua mbele kwa ushindi wa 4-3.
Mabao ya Simba yalifungwa na Uhuru Suleiman dakika ya tatu, Mgosi dakika ya 53 na 74 na Mkenya Hillary Echesa dakika ya 90 na ushehe, wakati wa Yanga yaolifungwa na Athumani Iddi dakika ya 30 na Jerry Tegete dakika za 69 na 89.
Baada ya mechi hiyo, kipa Mzungu wa Yanga, Obren Curkovic kutoka Serbia aliondoka moja kwa moja kwenye klabu hiyo, kwa aibu ya kufungwa mabao mengi na ya kuzembe, hasa la nne lililotiwa kimiani na Mkenya Echesa kwa umbali wa zaidi ya mita 40.
Msimu uliofuata katika mechi ya kwanza ya Ligi Kuu mjini Mwanza, Yanga ililipa kisasi Oktoba 16, mwaka 2010 kwa bao la Jerry Tegete dakika ya 70. Ikumbukwe mapema katika kuuzindua msimu huo, Simba na Yanga zilikutana katika mechi ya Ngao ya Jamii Agosti 18, mwaka 2010 na dakika 90 zilimalizika timu hizo zikiwa hazijafungana.
Mchezo ukahamia kwenye mikwaju ya penalti na Yanga ikashinda kwa penalti 3-1. Geoffrey Bonny, Stefano Mwasyika na Isaac Bokaye walimtungua kipa wa Simba siku hiyo, Ally Mustafa ‘Barthez’ wakati Mghana Ernest Boakye alikosa. Mohamed Banka ndiye mchezaji pekee wa Simba aliyemtungua kipa wa Yanga, Mghana Yaw Berko siku hiyo, wakati Emanuel Okwi, Uhuru Suleiman na Juma Nyosso walipoteza penalti zao.
Wababe hao katika soka ya Tanzania, walikutana tena katika mchezo wa marudiano wa Ligi Kuu Machi 5, mwaka 2010 na dakika 90 zilimalizika timu hizo zikiwa zimefungana bao 1-1, Yanga wakitangulia kupata bao dakika ya 59 kwa penalti mfungaji Stefano Asangalwisye Mwasyika.
Penalti hiyo ilitolewa baada ya mchezaji wa Kizambia wa Yanga, Davies Robby Mwape kuangushwa kwenye eneo la hatari na Juma Said Nyosso na refa Orden Mbaga akaamuru pigo hilo, ingawa watu walistaajabu kwa nini hakutoa kadi nyekundu kwa beki wa Simba.
Mussa Hassan Mgosi Mgunya aliisawazishia Simba dakika ya 73, akiuwahi mpira uliotemwa na Yaw Berko, kufuatia shuti la mpira wa adhabu kutoka nje kidogo ya eneo la mita 18 lililopigwa na Mganda Emmanuel Okwi.
Refa Orden Mbaga alizua tafrani uwanjani, kwanza kwa kulikataa bao la kusawazisha la Simba, kisha akalikubali baada ya kujadiliana na msaidia wake namba moja.
Mechi iliyopita, mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu, Yanga ilishinda 1-0 bao pekee la Mzambia Mwape.
Lakini kipindi chote hicho Yanga imeshindwa kulipa kisasi cha mabao 6-0 na kwa mwenendo ulivyo, hakuna dalili za kisasi hicho kulipwa leo au kesho. Simba ilifungwa 4-1 na Toto Afrika ya Mwanza, lakini ilikuwa madhubuti ilipocheza na Yanga Dar es Salaam msimu huo huo. Kipigo cha 6-0 bado kinaendelea kutonesha donda la wana Yanga miaka nenda rudi. 
Wakati timu hizo zinakutana tena katika mechi ya marudiano Jumamosi, bado 6-0 ni donda ndugu kwa Yanga. Simba ya sasa iko sawa, imetoka kumpiga Al Ahly Shandy 3-0 katika mechi ya kwanza hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho na inaongoza ligi, zaidi inahitaji kushinda mechi hiyo ya mwisho ili kujihakikishia ubingwa. Je, wana Yanga waendelee kusubiri iko siku watafuta aibu hiyo auj hilo ndilo wamelala nalo?  
 
source: bongostaz

BREAKING NEWS! MCHEZO WA AZAM NA MTIBWA KURUDIWA!


TAARIFA NILIZOZIPATA HIVI PUNDE KAMATI YA TIBAIGANA IMEAMURU MCHEZO BAINA YA AZAM VS MTIBWA URUDIWE ,

TAARIFA KAMILI BAADAE!

PLAY OF THE DAY!

EXCLUSIVE: AZAM KWENYE MAZUNGUMZO NA MKENYA ANAYECHEZA DENMARK.

Odhiambo mwenye jezi nyeupe.
Mchezaji wa zamani wa Randers FC George Blackberry Odhiambo ameondoka leo jijini Nairobi  kuja Tanzania ambapo anategemewa kufanya mazungumzo na klabu ya Azam ambayo imeonyesha nia ya kumsajili.

George Odhiambo alirudi Kenya wiki iliyopita kutoka Denmark baada ya mkataba wake wa miaka minne na klabu ya kidenish kuvunjwa kwa makubaliano baina ya timu hiyo na mchezaji mwenyewe.

Odhiambo pia amekuwa akihusishwa na kusajiliwa na klabu yake ya zamani ya Gor Mahia lakini hii ilikuwa inategemea na uamuzi wa kocha Logarusic  ambaye ndio anahusika na kusajili na kuruhus wachezaji kuondoka au kuuzwa. Jana jumanne kocha huyo alitangaza kuwaacha wachezaji tisa katika kile kilichoitwa kuipa uhai mpya klabu hiyo.

CRISTIANO RONALDO, BENZEMA NA HIGUAIN WAVUNJA REKODI YA LIGI YA HISPANIA KWA MAGOLI




Cristiano Ronaldo, Benzema na Higuain wametengeneza historia mpya kwenye La Liga baada ya kila mmoja magoli 20 au zaidi katika ligi hiyo ndani ya msimu mmoja. Haijawahi kutokea katika historia ya ligi hiyo kwa wachezaji wa timu moja kufanikiwa kufanya hivi.


GOALS THIS SEASON
PLAYER LA LIGA UCL COPA S. S. CUP TOTAL
Ronaldo 43 10 3 1  57
Benzema 20  7 3 1  31
Higuain 21  3 1 -  25
TOTAL 84 20 7 2 113

Washambuliaji hawa watatu ndio wanatengeneza safu kali ya ushambuliaji kwenye La Liga wakiwa wamefunga mabao 113 katika msimu mmoja, Ronaldo akiwa akafunga mabao 57 - magoli mengi zaidi katika kalbu hiyo.

TOP SCORING REAL MADRID ATTACKING TRIOS
Season Players (goals) Total
2011/12 Cristiano (57), Benzema (31), Higuain (25) 113
1959/60 Puskas (49), Di Stefano (24), Pepillo (22) 95
2010/11 Cristiano (53), Benzema (26), Higuain (13) 92
1960/61 Puskas (41), Di Stefano (29), Del Sol (18) 88
1961/62 Puskas (40), Di Stefano (22), Tejada (20) 82
1932/33 Olivares (39), Regueiro (24), Hilario (19) 82
1956/57 Di Stefano (43), Joseito (17), Mateos (17) 77
1988/89 H. Sanchez (37), Butragueño (22), Michel (15) 74
1957/58 Di Stefano (36), Rial (22), Marsal (15) 73
1958/59 Di Stefano (34), Puskas (25), Rial (13) 72

JUVENTUS WAGOMA KUTOA MKATABA MPYA: DEL PIERO ATANGAZA KUONDOKA KWA KIBIBI KIZEE CHA TURIN

Kwaherini.

Baada ya kukaa kwa misimu 19 akiwa na Kibibi Kizee cha Turin hatimaye mfalme wa Turin Alessandro del Piero ametangaza ataondoka katika klabu hiyo mwishoni wa msimu huu., huku Juventus wakikaribia kutwaa kombe la Scudetto tangu waliporudi kwa ligi ya Serie A.

Juve wanaweza kuchukua kombe la Coppa Italia  mwishoni mwa msimu ambapo watacheza dhidi ya Napoli: mchezo ambao utakuwa wa mwisho kwa Del Piero katika jezi maarufu za rangi nyeusi  na nyeupe.

Del Piero anamaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu, na mpaka sasa hajapewa mkataba mpya wa kuongeza muda wake wa kukaa Turin kwa msimu wa 20.

"Kwa sasa kama mambo yalivyo, mechi ya fainali ya Coppa Italia dhidi ya Napoli mwezi huu tarehe 20 ndio utakuwa mchezo wa mwisho kuitumikia Juventus kwa sababu mkataba wangu unamalizika mwezi June," Del Piero aliliambia La Gazzetta dello Sport.

"Lakini kwa sasa napenda kufikiria kuhusu wakati huu. Mapenzi waliyonionyesha mashabiki kila siku niliyokuwepo hapa ni makubwa. Hivyo kama la kutokea litatokea.






Huku siku zake za kukaa na Juventus zikiwa zinakaribia kuisha - ebu tukumbuke career ya Del Piero kwa namba.

702
Del Piero amecheza mechi 702 akiwa na Juventus - hii ni idadi kubwa kuliko mchezaji yoyote katika historia ya klabu hiyo.
 Del Piero alifunga bao lake la kwanza katika mechi dhidi ya Biaconeri  ikiwa ndio mechi yake ya pili na Juventus.

4
Del Piero amecheza mara nne fainali ya Champions League akiwa na Juventus - ingawa walifanikiwa kushinda mara moja na kupoteza mara 3.

7

Del Piero ameshinda kikombe cha Scudetto mara 7 akiwa na Juventus - kombe la kwanza akishinda katika msimu wake wa pili tu tangu aanze kucheza kikosi cha wakubwa cha Juventus.

289
Akiwa na magoli 289 katika mechi 702 na Juventus - Del Piero ndio mfungaji bora wa muda wote katika historia ya klabu hiyo.

32
Msimu ambao Del Piero alitisha zaidi ni msimu wa 1997-98 ambapo alifunga magoli 32 katika mashindano yote na kuiwezesha Juventus kuchukua kombe la Scudetto na kufika fainali ya Champions league.

ZANTEL YAZINDUA OFA MBILI MPYA- UHURU KWA TANZANIA BARA NA UMOJA KWA TANZANIA VISIWANI

Mkurugenzi wa Biashara wa Zantel Zanzibar Mohammed Mussa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na viwango vya Umoja ambavyo vinawawezesha wateja wetu walio visiwa vya Zanzibar kuongea kwa robo shilingi kuanzia saa nne usiku hadi saa moja asubuhi. Pembeni mwake ni Afisa Mkuu Biashara wa Zantel Ahmed Mokhles.
Afisa Mkuu Biashara wa Zantel Ahmed Mokhles (katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wakati wa uzinduzi wa ofa ya Isiyo na Kifani inayowawezesha wateja wa Zantel kupiga simu kwa nusu shilingi kwa masaa 24 na kwenda mitandao mingine kwa TSH 2 kwa sekunde siku nzima. Kulia ni Mkurugenzi wa Biashara wa Zantel Zanzibar Mohammed Mussa na aliyeketi kushoto ni Chief Mwakibete Mkurugenzi wa Bigtone LTD wakala mkuu wa Zantel.

ZANTEL YAZINDUA OFA MBILI MPYA- UHURU KWA TANZANIA BARA NA UMOJA KWA TANZANIA VISIWANI

Dar es Salaam, Jumatano 2 Mei, 2012: Kampuni ya simu za mikononi ya Zantel, imezindua ofa mbili mpya za kipekee kwa wateja wake wa Tanzania bara na visiwani zitakazoifanya kuwa mtandao nafuu zaidi nchini. Wateja wa Zantel Bara watafaidika na ofa ya UHURU ambayo itawawezesha kupiga simu kwa nusu shilingi (0.5) kwa sekunde muda wote. Ofa hii ya Uhuru itawawezesha pia kupiga mitandao yote nchini kwa shilingi 2 tu kwa sekunde. Zaidi ya hayo, ofa ya Uhuru itamuwezesha mteja kupiga kwenda nchi tano (Kenya, India, Pakistan, UAE and China) kwa shilingi 4 tu kwa sekunde siku nzima.
Wakati huo huo, wateja wa Zantel Zanzibar watafaidika na ofa ya UMOJA ambayo itawawezesha kupiga simu kwa shilingi moja kwa sekunde saa 2 asubuhi hadi saa 11 jioni, na baada ya hapo kupiga kwa robo shilingi (0.25) kila baada ya dakika ya tatu ya maongezi. Ofa hii ya Umoja pia itawawezesha wateja wa Zantel Zanzibar kupiga mitandao yote kwa shilingi 2.50 kwa sekunde muda wote.
Kujiunga na ofa hizi, wateja wa Zantel wanatakiwa kupiga *148*06#, wakati wateja wapya wataunganishwa moja kwa moja wakiongeza muda wa maongezi wa shilingi 500, na moja kwa moja watapata meseji 1000 pamoja na mlio wa simu kwa kutumia mwezi mzima.
Akizungumzia ofa hizo, ya Uhuru na Umoja, Afsa masoko mkuu wa Zantel, Bwana Ahmed Mokhles anasema:
“Ofa hizi zote zinalenga kuwapa wateja wetu thamani ya pesa zao wakiwa wanawasiliana na ndugu zao, marafiki pamoja na wafanya biashara wenzao wakitumia mtandao wa Zantel.”
Katika kuonyesha pia Zantel ni mtandao unaowajali wateja wake, imeamua pia kuongeza muda wa promosheni yake ya TickTock na Ushinde baada ya kupata shuhuda toka kwa wateja wake namna ilivyoweza kuwasaidia kimaisha.
Wakati baadhi wameweza kuwalipia ada ya shule watoto wao, wengine wameweza kufungua biashara zao wenyewe”anasema Bwana Mokhles.

Ticktock na ushinde ni promosheni ya kipekee iliyoanzishwa na Zantel kuanzia tarehe 1 mwezi wanne ambapo kila siku mshindi mmoja wa shilingi milioni moja na wengine 24 walikuwa wakijishindia simu za mkononi kila siku kwa kuongeza muda wa maongezi wa shilingi elfu moja au zaidi. “Tunafuraha kubwa kuongeza muda wa promosheni hii, ili tuwafikie wateja wengi Zaidi” anasisitiza Mokhles.
Sambamba na ofa hizo, Zantel pia itakuwa na ofa katika maduka yao na ofisi za huduma kwa wateja katika vituo  vya Vuga, Chake Chake, Pemba na katika makao makuu ya Zantel , Dar es salaam, ambapo zawadi zaidi zitatolewa kwa wateja watakaoenda kuweka muda wa maongezi kupitia maduka ya Zantel au kupitia Mimina.
 Kwa shilingi 1,000 au zaidi wateja wetu wana nafasi ya kushinda zawadi za papo kwa papo kama miavuli, peni, tisheti na nyingine nyingi” anasema mkurugenzi wa Masoko wa Zantel-Zanzibar Bwana Mohamed Mussa.
Huduma hizi zote ni sehemu ya ahadi za Zantel kuwa kampuni ya simu inayompa mteja wake huduma bora kwa gharama nafuu kabisa.
-MWISHO-


SHOMARI KAPOMBE NA FELIX SUNZU WATAKIWA TP MAZEMBE

SIKU mbili baada ya kuonyesha kiwango cha juu katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika, kiraka wa Simba, Shomari Kapombe na mshambuliaji wa timu hiyo, Felix Sunzu wameanza kupigiwa hesabu na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Habari ambazo zimekuwa zikizagaa na kuripotiwa na vyombo vya habari, zinadai kuwa klabu hiyo inayoshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika ilituma mawakala wake kwa ajili ya kuangalia soka ya wachezaji hao ambao ni vipenzi vya mashabiki wa Simba kwa sasa.

Katika mchezo wa Jumapili, Kapombe 'alivalishwa viatu' vya Juma Nyoso aliyekuwa nje kwa kadi nyekundu na kuimudu kikamilifu nafasi hiyo katika mchezo huo uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa.

Chanzo cha habari kilipasha kuwa ujumbe wa watu wawili ulitumwa kwa ajili ya kuwaona pamoja na kufanya mazungumzo ya awali na wachezaji hao kwa ajili ya kujiunga na timu yao.

Habari zilizopatikana baadaye zilisema kuwa Kapombe anabanwa na mkataba na hata hivyo imeelezwa kuwa Simba haiwezi kumwachia kwa sasa wakati Sunzu amekataa kuondoka na lengo lake ni kuona Simba inatwaa ubingwa wa Bara na Kombe la Shirikisho.

"Unajua wale mabwana walikuwa wanawataka hawa wawili, lakini Sunzu amekataa ila Kapombe hajawa muwazi, sasa sifahamu msimamo wake, lakini inawezekana anabanwa na mkataba," kilisema chanzo hicho ndani ya Simba.
 
 Kapombe alipotafutwa kuzungumzia suala hilo,  ambapo alisema mpaka sasa hana taarifa zozote za jamaa hao wa TP Mazembe.

"Kaka sina taarifa zozote za hao jamaa, wala hajanifuata ila wakinifuata mimi nipo tayari kuzungumza nao, kwa sababu ni mazungumzo,"alisema Kapombe.

Klabu ya TP Mazembe tayari imeishawachukua wachezaji wawili kutoka Simba ambao ni Mbwana Samata na Patrick Ochan, pia timu hiyo imemchukua mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Vijana ya Tanzania, Thomas Ulimwengu.

NSA JOB AITOSA VILLA - AENDA SWEDEN KUJARIBU ZALI

MSHAMBULIAJI wa Villa Squad, Nsa Job, amepata ulaji wa kwenda kufanya majaribio Sweden kutokana na kiwango chake kuwa juu kwa sasa.
 Mwenyekiti wa Villa, Uledi Ramadhani, alisema Nsa alimwambia kuwa anatarajia kuondoka nchini mara baada ya ligi kumalizika kwenda kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa.
Alisema awali Nsa alimwambia anaenda Ulaya bila kuwatajia sehemu aendayo lakini watu wake wa karibu wakamwambia anakwenda Sweden ambako ametafutiwa timu na wakala wake.
“Nsa aliniambia anatarajia kwenda Ulaya kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa mara baada ya ligi kumalizika ingawa hakuniambia ni nchi gani anaenda, ila wenzake waliniambia amepata timu Sweden.
“Binafsi namuunga mkono kwa hilo kwa kuwa sisi tunapenda maendeleo, hivyo tutafurahi tukiona amefanikiwa kwa kuwa ni njia mojawapo ya kuitangaza Villa,” alisema Uledi.
Nsa alipotafutwa kuzungumzia mpango huo alikiri: “Kweli naondoka kati ya tarehe sita au saba mwezi wa tano, nakwenda Sweden kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa.”
Nsa aliyejiunga na Villa Julai, mwaka jana akitokea Yanga, amefanikiwa kuonyesha uwezo mkubwa katika michezo ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Bara akiwa amefunga mabao kumi mpaka sasa.


EDEN HAZARD AZIANGALIA UNITED NA CITY ZIKICHUANA - MASAA 24 BAADA YA KUIADHIBU PSG

Eden Hazard alikuwa mmoja ya watu maarufu walioenda kuangalia mechi katika ya mahasimu wawili wa jiji la Manchester.

Timu hizi mbili zote zimekuwa zikihusishwa na kumsajili kinda huyo mwenye kipaji cha hatari akiwa na miaka 21,  hivyo kusababisha vita nyingine baina ya rivals hawa.

Roberto Mancini wikiendi iliyopita aliongeza joto la vita hiyo kwa kumwambia Hazard kwamba City ndio mahala panapomfaa.

Boss wa United Sir Alex Ferguson pia amethibitisha kuwa anavutiwa na Hazard na alienda kumuangalia nchini Ufaransa.

Arsenal na Tottenham wote nao wapo katika kuwinda saini ya kinda hilo.

Hazard alienda nchini Uingereza jijini Manchester kwa ajili ya kuangalia derby masaa 24 baada ya kufunga goli moja na kutengeneza lingine katika ushindi wa Lille wa 2-1 dhidi ya Pars Saint Germain.



Katika mchezo huo aliangaliwa na bosi wa kituo cha maendeleo cha City Patrick Vieira na skauti wa United Martin Ferguson.

KOCHA MPYA WA ENGLAND: NITAONGEA NA RIO NA TERRY, ROONEY ATAKUWEMO KATIKA KIKOSI CHANGU - SHEARER ATAJWA KUWA MSAIDIZI WAKE



Kocha mpya wa England
Kocha mpya wa England Roy Hodgson ataongea na John Terry na Rio Ferdinand kwa matumaini ya kuwachukua wachezaji wote wawili katika michuano ya EURO 2012.

Kazi kubwa ya kwanza kwa Hodgson ni kunitibu majeraha ya uhusiano mbovu uliopo baina ya wachezaji  katika chumba cha kubadilishia nguo uliotokea baada ya Terry kutuhumiwa kumtolea maneno ya kibaguzi Antoni Ferdinand - ambaye ni mdogo wake Rio. mwezi October mwaka jana.

Terry na Ferdinand wanabakia kuwa mabeki wenye ushirikiano mzuri katika timu ya taifa na wakati akitangazwa rasmi katika uwanja wa Wembley, Roy alikaririwa akisema: "Itabidi niongee na John na Rio, natumaini tutakutana uso kwa uso, na kujua nini suluhisho.

"Kwa sasa siwezi kusema chochote  mpaka nitakapogundua kiundani mahusiano yao yapoje - na nafikiri sitoongeea na wao tu, nitaongea na wachezaji wote wakubwa ndani ya kikosi."

Hodgson, ambaye amesema kwamba atamchagua Wayne Rooney katika kikosi cha wachezaji 23 - ambacho atakitangaza muda mfupi baada ya msimu kuisha - bado hajaamua kuhusu wasaidizi wake.

Lakini inaaminika atamchagua msaidizi mmoja, ingawa bado hajaongea na kocha wa England chini ya miaka 21 na kocha wa timu ya Uingereza ya Olympic Staurt Pearce kuhusu jinsi ya kuhusika kwake katika EURO 2012.
Alan Shearer

Mtu anayetajwa sana kuweza kuchaguliwa kama msaidizi wa Roy ni Alan Shearer ambaye anatajwa kuwa na mahusiano ya karibu sana na Hodgson.

ASAMOAH GYAN KUONDOKA RASMI SUNDERLAND - APEWA DILI LA £200,000 BILA VAT

Asamoah Gyan anakaribia kukamilisha uhamisho rasmi wa £10million kujiunga na Al-Ain ya Uarabuni mwezi huu.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ghana, ambaye alitumia muda mrefu wa msimu kwa kucheza dili la mkopo la kulipwa £200,000 kwa wiki bila kodi - akitokea Sunderland ya England.

WASIKILIZE HAPA WAZEE WA YANGA



SIMBA VS AL ALHLY WAINGIZA 216


WAKATI mchezo wa Kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF) baina ya Simba na Al Ahly Shandy ya Sudan ukiingiza shilingi milioni 216,kikosi cha Simba kinaendelea na maandalizi yake ya mchezo  wake wa mwisho wa ligi kuu soka Tanzania Bara dhidi ya Yanga utakaopigwa jumamosi hii kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza kwa simu kutoka Visiwani Zanzibar  ambapo timu imepiga kambi, msemaji wa Simba Ezeckiel Kamwaga  alisema kwamba kikosi chao ambacho kimepiga kambi eneo la Mbweni kipo katika hali nzuri na kinafanya mazoezi katika uwanja wa Fuoni.
Aliongeza kuwa wamepania kushinda mchezo huo ili kulipiza kisasi cha kufungwa bao 1-0 na mahasimu hao katika mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo ambayo Simba inaongoza kwa pouinti 59 ikifuatiwa na Azam Fc yenye pointi 56 na Yanga inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 46.

USHINDI WA MANCHESTER CITY JANA WASABABISHA KIFO NAIROBI KENYA: AMUUA NDUGU YAKE BAADA YA UNITED KUFUNGWA.

Shabiki wa soka ameripotiwa kuchomwa kisu mpaka kufariki baada ya kutokea majibizano juu ya matokeo ya mechi ya jana usiku ya premier league kati Man City and United iliyofanyika kwenye uwanja wa Etihad Stadium.

Mr.Stephen Ochieng Olouch, 24, ambaye ni mfanyabiashara wa biashara za kutembeza katika soko la Muthurwa, Nairobi, alichomwa kisu na ndugu yake baada ya kutokea kwa majibizano makali  baada tu ya Manchester City kuibuka na ushindi wa 1-0.

Kwa mujibu wa mdogo wa Ochieng Mercel Omondi, 22, ni kwamba kaka yake na ndugu yao walikuwa wanangalia mechi katika ukumbi wa Mbotela usiku wa jana na wakaanza kujibizana huku kila mmoja akitetea upande wa timu aliyokuwa akiishabikia.

Shahidi aliyeshuhudia tukio hilo amesema kwamba, "Wawili wale walikuwa wanakaa pamoja katika chumba cha kupanga - jana muuaji aliwahi kurudi kabla ya marehemu na kujifungua ndani. Marehemu Stephen aliporudi akagonga mlango kwa fujo huku akisema afunguliwe - alipofunguliwa mlango na mwenzie wakaanza tena kujibizana kitu ambacho kilipelekea wawili wale kushikana na kuanza kupigana kabla ya mtuhuiwa kuchukua kisu na kumchoma mwenzie kichwani."

Majirani hawakustuka kutokana na kelele za ugomvi ule kwa sababu wale jamaa kupigana  na jambo la kawaida .

Mpaka sasa mtuhumiwa hajakamatwa na polisi wanaendelea kumtafuta.

Tuesday, May 1, 2012

WAZEE WA YANGA WAMCHARUKIA NCHUNGA

BARAZA la wazee la klabu ya Yanga limesikitishwa na kauli za kejeli na zenye kuwadhalilisha  alizozitoa mwenyekiti wa klabu hiyo Lloyd Nchunga juzi, hivyo kuanzia sasa wamemwachia aendelee na timu hiyo.
Hatua hiyo inafuatia Nchunga kudai kuwa wazee hao walikurupuka na hawezi kukabidhi kwa wahuni, pia sehemu ambapo hana uhakika na usalama, huku akihofu timu hiyo kuhudumiwa na wauza dawa za kulevya.
Wakizungumza na mamapipiro blog leo asubuhi wazee hao wakiongozwa na katibu wao Ibrahim Akilimali walisema kwamba hawakukupupuka kutangaza kuichukua timu bali walikubaliana na Nchunga, lakini wanashangaa baadaye kuwageuka.
“Hatukukurupuka kuongea vile, ilikuwa ni ridhaa ya Nchunga, tulikuwa sahihi kutokana na mapenzi yetu na timu, pamoja na kuwa uongozi ndio una haki tuliikubaliana kuichukua timu kwa lengo la kuhakikisha inaifunga Simba, tunafanya usajili wa uhakika na kurejesha nidhamu,”alisema.
“Ni ajabu kwa Nchunga kututamkia sisi wauza unga, inamaana mama Fatma Karume, Francis Kifukwe, Seif Ahmed, Abdallah Binkleb na Yusuf Manji ni wauza unga?
...hivi Nchunga anajua umuhimu wa hawa watu ndani ya Yanga,tena kwa mshangao mkubwa amediriki hata kutuma watu wamzuie kuingia klabuni mzee Kitundu  (Jabir)ambaye alishiriki kuijenga klabu,”alisema Mzee Akilimali.
Naye mjumbe wa baraza hilo, Yussuf Mzimba pamoja kusikitishwa na kauli za Nchunga, alisema Yanga ina wenyewe na kwamba ukifuga kuku wengi lazima utapata aliye kisirani ambao wanajifanya wanajua kumbe si lolote.
“Tunataka serikali iangali watu kama hawa, Nchunga hawezi kutukana watu kama kina mama Karume, inaonekana klabu imemshinda kwani aliingia madarakani kwa bahati tu na matokeo yake kaleta mgawanyiko badala ya umoja”,alisema mzee Bilal Chakupewa.
Aidha Mzee Chakupewa aliongeza kwamba hata kama wakiifunga Simba jumamosi Nchunga ni lazima aondolewe madarakani kutokana na udhaifu aliouonyesha kwenye uongozi wake na kuifikisha Yanga mahala pabaya

SIMBA WAFUATA UBANI WA KUIREHEMU YANGA ZANZIBAR - MILAOVAN AFURAHISHWA NA USHINDI DHIDI AL ALHLY

SIMBA jana ilienda Zanzibar kwa ajili ya kujiandaa na mechi ya mwisho ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya mtani wake Yanga itakayofanyika Jumamosi wiki hii.

Vinara hao wa Ligi Kuu wamefunga safari hiyo ikiwa siku moja baada ya kuifunga Al Ahly Shandy ya Sudan mabao 3-0 katika mechi ya kwanza ya raundi ya tatu ya michuano ya Kombe la Shirikisho na hivyo kujiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu hatua inayofuata katika mechi ya marudiano wiki mbili zijazo.


Habari za uhakika kutoka ndani ya Simba zilizopatikana jana zilisema uongozi wa timu hiyo umeamua kuipeleka Zanzibar kwa siku zilizosalia ili kujiandaa na mechi hiyo. Mechi dhidi ya Yanga ndio itaamua hatima ya ubingwa wa Simba, inahitaji ushindi au sare ili kutangaza ubingwa.


Simba ina pointi 59 na Azam inayoshika nafasi ya pili ina pointi 56, hivyo Simba ikifungwa na Yanga na Azam kushinda mechi yake ya mwisho zitalingana pointi na hivyo bingwa kuamuliwa kwa tofauti ya mabao.


“Tuko njiani tunakwenda Zanzibar kwa ajili ya kambi kujiandaa na mechi ya Yanga, nadhani tutarudi Ijumaa jioni,”alisema mchezaji mmoja alipozungumza na mwandishi wetu kwa simu jana.


Wakati huohuo Kocha Mkuu wa Simba Milovan Cirkovic ameelezea kufurahishwa na kiwango kilichooneshwa na wachezaji wa timu hiyo kwenye ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Al Ahly kwenye Uwanja wa Taifa juzi.


Akizungumza mara baada ya mchezo huo Milovan alisema kuwa ushindi huo unaiweka timu yake kwenye nafasi nzuri ya kusonga kwa hatua inayofuata.


Alisema kuwa timu yake ilicheza vizuri hasa kipindi cha pili na ndio maana waliweza kupata mabao hayo na kuongeza kuwa bado wanakabiliwa na kazi ngumu kuiondoa timu hiyo katika mashindano.


“Ni kama tumemaliza nusu ya kwanza ya mchezo, nusu ya pili itakuwa nyumbani kwao hivyo bado tuna kazi ya kuhakikisha tunaitoa na kusonga mbele,” alisema Milovan.


Maneno ya Milovan yaliungwa mkono na nahodha wa timu hiyo Juma Kaseja aliyesema bado wana kazi ngumu kuitoa timu hiyo mashindanoni watakaporudiana wiki mbili zinazokuja huko Kartoum Sudan.


“Kwanini tuone kama tumeitoa, hapana bado tunakabiliwa na mechi ngumu ya marudiano kama mlivyoiona ni timu nzuri, hivyo kazi haijaisha,”alisema Kaseja.

HAYA WAJUZI WA MAMBO TUSAIDIANE KIDOGO: HUYU NI NANI AKIWA NA FAMILIA YAKE?


BREAKING NEWS: AFRICAN LYON WAKATA RUFAA DHIDI YA MAAMUZI YA KAMATI YA NIDHAMU NA USULUHISHI KUHUSU MTIBWA SUGAR

5th Floor

Barclays House

P.O. Box 11133

Dar es Salaam

Tanzania

­­
REF No: ALFC/VOL.11/21/021
MWENYEKITI WA KAMATI YA NIDHAMU NA USULUHISHI ­TFF
S.L.P 1574
DAR ES SALAAM
TANZANIA

YAH: KUKATA RUFAA KWA TIMU YETU YA AFRICAN LYON FC DHIDI YA
KUCHEZA NA TIMU BATILI YA MTIBWA SUGAR LIGI KUU YA VODACOM
MCHEZO NO 174

Husika na somo la hapo juu kwa mujibu wa kanuni za ligi .KANUNI YA 15(1)
tunakata rufaa katika kamati yako kupinga kuendelea kwa uwepo wa timu ya
MTIBWA SUGAR katika ligi kuu Tanzania.

Sababu kubwa ya kukata rufaa hii ni kutokana na kamati ya ligi ya mashindano kutoa
maamuzi ya kutatanisha na yasiyozingatia kanuni dhidi ya mchezo AZAM FC VS
MTIBWA uwanja wa Chamanzi tarehe 22/4/2012.

Kamati ya ligi na mashindano katika maamuzi ya mchezo huo imepindisha KANUNI
MAKUSUDI kwa lengo la kutoa MAAMUZI KWA KUTUMIA KANUNI NA
TARATIBU KWA NJIA CHAFU ZISIZOKUBALIKA (KANUNI ZA LIGI
UTANGULIZI PARA YA MWISHO)

Sababu za kukata rufaa hii ni kama ifuatavyo:-
1. Kamati ya ligi na mashindano haikuzingatia kanuni no. 22. ( kifungu kidogo cha
kwanza), Ambayo ndio inayobeba dhana nzima ya KUVURUGA MCHEZO.

2. KANUNI NO.22 kifungu kidogo cha 1­6 ZINAELEZEA MCHAKATO MZIMA
WA KUVURUGA MCHEZO na adhabu zake, hivyo kamati kutumia kipengele
no 3 kuhusu muda wa mwamuzi kusubiria ni kitendo cha kutaka kuyumbisha
kanuni kwa makusudi.
Tafsiri halisi ya 22.(3) ni kuwa kuna tamko linalompa mwamuzi muda (nukuu)
‘’MWAMUZI ATASUBIRI KWA DAKIKA ZISIZOPUNGUA 15’’ Hivyo
mwamuzi anayo mamlaka ya kuona muda unaofaa kati ya dakika 1 hadi 15.
Kamati imelipotosha hili kwani mwamuzi alizingatia muda wa KIKANUNI.

3. Tunapinga pia kamati kutumia kipengele cha kanuni no. 5 na 6 kwani Tafsiri yake
halisi hata kama timu iliyo kwisha kuabidhiwa kwa kanuni no 22.(1)bado

4. itashushwa daraja na kutekeleza kanuni 22. Kifungu kidogo cha 4,5na 6. Kamati
hili nalo ilipotosha na kuyumbisha kanuni kwa maslahi binafsi.

Kamati ya ligi
5. Kunukuu kanuni za FIFA katika kutoa adhabu bado kanuni inaelekeza jukumu la
Tafsiri ya kanuni na chombo kinachopaswa kuelekeza kanuni za FIFA na CAF
(KANUNI ZA LIGI IBARA YA 69).

29/4/2012

6. Hoja yetu nyingine ni kuwa kamati ya ligi na mashindano maamuzi yake
yanaonekana wazi ni ya kimaslahi zaidi kuzingatia uhalisia wa kanuni
Mfano hai:
a. Mwenyekiti wa kamati : WALLACE KARIA ni mjumbe kutoka klabu ya
Mtibwa hivyo ana maslahi na timu ya Mtibwa fc.

b. Makamu mwenyekiti

c. Mjumbe wa kamat

: Kamati ya ligi SAID MOHAMED ni mwenyekiti wa
Klabu ya Azam Fc ambayo ina maslahi na mchezo huo.

:

GODFREY NYANGE KABURU ni makamu

mwenyeki Simba maamuzi halali ya KANUNI
yanaiathiri klabuyake ya Simba kuelekea mbio za
ubingwa

d. Mjumbe wa kamati

:

YAHAYA AHMED ni mfanyakazi wa kiwanda
cha mtibwa sugar­ hatatenda haki kwa kuwa ana
maslahi na mtibwa.

e. Mjumbe wa kamati

:

Damas Ndumbaro
Ni mwenyekiti kamati ya uchaguzi Simba ana
maslahi na Simba. Pia kisheria haruhusiwi
kuwepo kwenye kamati ya ligi kwa kuwa ni
WAKALA WA FIFA. Na FIFA imelikataza hilo
la mwakala wake kua kwenye kamati zozote za
shirikisho la mpira wa miguu.

Hivyo basi kwa kuwa wajumbe hawa niliowataja hapo juu walikuwa na maslahi
binafsi na uamuzi wowote ndani ya kikao hicho ni dhahiri maamuzi hayakuwa ya
haki na iwapo kama kamati ya ligi ilizingatia hoja hizi. Basi KORAM isingeweza
kutimia na kikao kilikuwa ni BATILI.

7. Sisi African Lyon tunashaka hata utekelezaji wa adhabu kabla ya mchezo wetu
no 174 dhidi ya mtibwa haikutekelezwa. Kanuni ya 22 kifungu no.6 (Adhabu ya
faini tunaomba kamati yako ijiridhishe na uhakiki wa hilo)

8. Kanuni bado hazizingatiwi hasa ukiangalia swala la mchezaji Salum Swed
aliyecheza mchezo no. 174 huku akiwa na adhabu kwa kumpiga mwamuzi
mchezo Azam vs Mtibwa.

MAJUMUISHO
Iwapo kama kweli kamati ya ligi na mashindano ingetaka kutoa maamuzi ya haki kwa
sababu ilizotoa basi maamuzi ya kamati yasingeegemea upande mmoja wa maamuzi
yenye utata. Kwakua wajumbe wengi wana maslahi na maamuzi ya kikanuni hivyo
basi ilipelekea wao kuangalia maslahi yao binafsi.

Kamati yako tukufu tuna imani itazingatia taarifa za mchezo husika na pia itazingatia
kanuni no.24 kifungu cha (i) na kuitolea tafsiri halisi ya kanuni no.22. (1 –6) ili haki
itendeke.

Tunatanguliza shukrani zetu za awali tukiwa na IMANI KUBWA NA KAMATI
YAKO KUWA ITATENDA HAKI KATIKA KUSIMAMIA KANUNI ZA LIGI NA
KUTOA MAAMUZI YA HAKI KWA MUJIBU WA KANUNI ZA LIGI KUU ZA
2011/12 AMBAZO ZILIZOPITISHWA NA KAMATI YA UTENDAJI 20 JULAI
2009.

AHSANTE

……………………………………
Rahim Kangezi
CEO/OWNER AFRICAN LYON FC
Mob: +255 784 255614
Email: Kangezi@gmail.com

Na ambatanisha na ada ya rufaa shilingi laki tatu (300,000/=)

www.africalyon.com

KALI YA LEO: CHEKA NI MCHAWI - ALINIROGA NA KIFO CHA DEREVA PIKIPIKI ALIYEMGONGA KILIBIDI KIWE CHANGU




Mada Maugo.
Baada ya pambano la juzi kati ya mabondia Francis Cheka na Mada Maugo, stori kubwa kwenye midomo ya watu ni kuhusu lile gari alilozawadiwa Francis Cheka kwenye hilo pambano ambapo usiku ule ule jumamosi hilo gari lilipata ajali na linadaiwa kugonga mtu na kumuua.
Bondia Mada Maugo amekubali kuamplfy kwenye millardayo.com baadhi ya vitu ambavyo hakuvizungumza kokote, ikiwemo stori ya yeye kudai kwamba alikua amelogwa na cheka ndio maana alipigwa kwenye hilo pambano.
Amesema “mimi mambo ya ushirikina sitaki sana kuongelea japo hata kina matumla walishawahi kusema kwamba Cheka amewaloga, kingine ni kwamba najua round ya tano, ya sita kwenye pambano nilipokaa kwenye kiti niliamua nisirudi tena kwa sababu nilikua sioni, simuoni mtu ninaepigana nae ni giza kabisa mbele yangu”

.
Maugo amesema hana neno na Cheka japo kuna kauli mbaya Cheka aliitoa kwake kwamba ndio alitakiwa kufa na sio yule aliekufa baada ya kugongwa na gari ambalo Cheka alizawadiwa usiku baada ya kushinda pambano kitu ambacho ni ishara ya ushirikina.
Maugo Ameamplfy kwamba “alipogonga mtu usiku ule na kumuua nilikwenda kumuona pale polisi Osterbay nikamuona kiubinadamu na nikaongea nae lakini nilishtuka sana baada ya yeye kuniambia kwa mdomo wake kwamba kama nisingeacha kupigana nae ningekufa, akasema bahati yako nzuri amekufa dereva wa pikipiki… baada ya hapo aliniambia nimfate hotelini kwake Magomeni lakini kutokana na kauli yake sikuweza kumfata tena, yeye bado yuko Magomeni baada ya kuwekewa dhamana kutokana na kifo cha huyo dereva wa pikipiki”

kutoka: http://millardayo.com/

DIAMOND AKIWA KWENYE HELKOPTA AKIWAPAGAWISHA MASHABIKI DAR LIVE

JE MBIO ZA UBINGWA NCHINI ENGLAND NDIO ZIMEISHIA HAPA? ANGALIA CITY WALIVYOIADHIBU UNITED


Manchester City 1-0 Manchester United by goalsarena2012-3

LIONEL MESSI VS CRISTIANO RONALDO - MWEZI WA 4

TAKWIMU ZA APRIL
         

470 DK. WALIZOCHEZA 469
7 MAGOLI 6
2 PENATI 1
5 ASSISTS 1
27 / 10 (37%) MASHUTI / YALIYOLENGA 39 / 13 (33.3%)
338 / 295 (87.3%) PASI / ZILIZOFIKA 185 / 145 (78.4%)
7.4 WASTANI 7.9
43 2011-12 LA LIGA GOALS 43
65 (56) 2011-12 COMPETITIVE GOALS (APPEARANCES) 57 (52)
http://i1.goal.com/files/images/stats/goal/team-logos/1/451_48x48.jpg

SIMBA WAENDELEA KUFANYA USAJILI: WAMNYAKUA KIUNGO WA DC MOTEMA PEMBE

Kanu Mbiyavanga

DR CongoDR Congo | 23 years | Midfielder


7

PROFILE
NamePatrick Nkanu Mbiyavanga
NationalityDR Congo DR Congo
Born1989-03-15 (23 years)
City of BirthKinshasa - Zaire Zaire
PositionMidfielder
Height171 cm
Weight70 kg
Web
Social network
Club-

KIUNGO wa kimataifa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Patrick Kanu Mbiyavanga ameanza mazoezi rasmi na Simba juzi Alhamisi kwenye Uwanja wa TCC

Chang'ombe jijini Dar es Salaam na ameahidi kufanya kazi nzuri kuhakikisha kikosi hicho kinafikia malengo.

Mbiyavanga aliivutia Simba baada ya kumwona akiwa na kikosi cha DC Motema Pembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kwenye Kombe la Shirikisho msimu uliopita.

Kiungo huyo ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili na alishawahi kuichezea klabu ya GD Inter Luanda inayoshiriki Ligi Kuu Angola, alisema kuwa amejiunga Simba kwa sababu anaipenda na tayari amesaini mkataba wa miaka miwili.

"Tulikubaliana na viongozi na malengo yangu ni kufanya kila niwezalo kuona naisaidia Simba kufikia malengo yao," alieleza Mbiyavanga.
Kocha wa Simba, Milovan Corkovic alisema hajamwona Mbiyanga akicheza mechi lakini anaamini ni mchezaji mzuri.

Kimsingi Mbiyavanga alivutwa na aliyekuwa kocha wa zamani wa Simba, Moses Basena.
Basena alivutiwa na mchezaji huyo baada ya mechi kati ya Simba na Motema Pembe, mwaka jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Basena aliweka wazi alikuwa amevutiwa naye mbele ya waandishi wa Mwanaspoti na ndilo lilikuwa gazeti la kwanza kuripoti kuwa mchezaji huyo atajiunga na Simba.
Katika hatua nyingine, kiungo huyo juzi Alhamisi alionja joto ya jiwe mbele ya kocha Milovan Cirkovic baada ya kuleta maringo mazoezini.

Aliingia uwanjani hapo na kuwakuta wachezaji wote wa Simba wameshaanza mazoezi, lakini alitakiwa kuanza kukimbia kuzunguka uwanja.

Alitii amri hiyo lakini alikuwa anakimbia huku akiwa ameshusha kaptula yake kwa mtindo wa 'mlegezo.
Baada ya kukimbia raundi mbili, uvumilivu ulimshinda Cirkovic na mchezaji huyo alipofika karibu yake alimuita na kumtaka kupandisha kaptula yake huku akimkaripia kuwa hataki tabia za kihuni.

�Pandisha kaptula hiyo, alisikika Cirkovic na mchezaji huyo alipandisha kidogo na kuendelea kukimbia, lakini kocha huyo akamwamuru arudi na kumtaka kupandisha vizuri hadi juu ndipo aendelee kukimbia, kitu alichokitekeleza na kisha kuendelea na mazoezi na kuwaacha watu wakiangua kicheko.

NIYONZIMA: SIONDOKI YANGA

KIUNGO mahiri wa Yanga, Haruna Niyonzima Fabregas, amewahakikishia mashabiki kwamba ana mwaka mwingine mmoja (siku 365) wa kuvaa jezi katika timu hiyo ya Mtaa wa Jangwani kama asipopata timu nje ya nchi na wala vuguvugu la watu kujiuzulu halimhusu.

Hata hivyo Mnyarwanda huyo amekiri kwamba mambo yalikwenda ndivyo sivyo msimu huu wa Ligi Kuu Bara, lakini wataing'ang'ania Simba Jumamosi ijayo kulinda heshima yao kama wachezaji na hadhi ya klabu.

Haruna amekuwa akihusishwa na kuondoka Yanga hasa baada ya mwanachama aliyemnunua Rwanda, Bin Kleb, kujiuzulu kwenye nafasi zote za uongozi na kukaa kando.

Sababu nyingine inayotajwa kutaka kumkimbiza mchezaji huyo Yanga ni ukweli kuwa klabu hiyo imekosa nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa barani Afrika mwakani.

"Siwezi kuondoka Yanga kienyeji, nina mkataba nao, kitakachotokea ni kwamba kama nitapata timu nje ndipo nitaondoka, lakini vinginevyo nitakuwa hapa kwa msimu mwingine tena," alisema.

"Hayo mambo mengine ya viongozi wamejiuzulu mimi kama mchezaji hayanihusu, kazi yangu mimi ni uwanjani na kutekeleza mkataba wangu."

Akizungumzia mechi ya Simba, alisema: "Tutaing'ang'ania Simba na tutaifunga kutunza heshima yetu kwa vile hatuna cha kupoteza na msimu umeshaharibika kwa upande wetu.

"Tunataka ushindi tu, hakuna cha ziada na tutafanya kazi kwelikweli uwanjani, ndicho kitu pekee tunachoweza kuwalipa mashabiki wetu kwa sasa.".

source:mwanaspoti