Search This Blog

Saturday, November 10, 2012

LIVE MATCH CENTRE: SIMBA SC 0 - 1 TOTO - AZAM FC 1 - 2 MGAMBO JKT - FULL TIME


DK 90: Simba 0-1 Toto FULL TIME


 DK 83: Simba wanafanya mabadiliko anatoka Kazimoto anaingia Edward Christopher. 

Kutoka Tanga - Azam 1-2 Mgambo JKT 

 DK 74: Toto inapata bao la kuongoza linalofungwa na Mussa Said akiunganisha krosi ya Mohamed Jingo. Simba 0-1 Toto.

 DK 72: Mrisho Ngassa anaenda benchi na nafasi yake inachukuliwa na Haruna Chanongo. Simba 0 - 0 Toto

 DK 84: Issa Kambili anaipatia Mgambo bao la pili dhidi ya Azam

 DK 62: Toto inafanya mabadiliko anatoka Kheri Mohamed anaingia Mohamedi Hussein

 DK 55: Seleman Kibuta wa Toto anakosa bao la wazi baada ya shuti lake kupanguliwa na kipa wa Simba William Mweta.

Kutoka Tanga - DK ya 75 Azam 1-1 Mgambo

DK 50 Mrisho Ngassa anakosa bao la wazi akiwa amebaki na kipa wa Toto.

Kipindi cha pili kinaanza hapa uwanja wa taifa Simba 0-0 Toto
 
Kutoka Tanga hivi ni dakika ya 10 kipindi cha pili Azam 1-1 Mgambo.


 Mpira ni mapumziko Simba 0 - 0 Toto

 Dakika ya 42 milango ya timu zote bado migumu huku timu zikishambuliana kwa zama.

 Dakika ya 28 - Simba 0 - 0 Toto Africa

Kutoka Tanga - Dakika 45 za kipindi cha kwanza zimeisha timu zikitoshana nguvu, Azam 1 - 1 Mgambo JKT .

 Uwanja wa taifa leo upo doro, watu wakiwa wachache sana. Kipindi cha kwanza mpira ni mkali na timu zinashambuliana kwa zamau. Hivi sasa ni dakika ya 15 - Simba 0 - 0 Toto

AZAM 1 -1 MGAMBO - Mabao ya Kipre Balou  kwa Azam, na Issa Kambili aliifungia Mgambo

SIMBA 0 - 0 TOTO AFRICA


EPIQ BSS YAMALIZIKA NA USHINDI WA WALTER CHILAMBO

Mshindi wa shindano la  Epiq Bongo Star Search 2012 (EBSS),Walter Chilambo (Dar) akikabidhiwa sanduku lake lenye kitita cha shilingi milioni 50 ndani ya ukumbi wa Diamond jubilee,katika shindano hilo lililovuta hisia za wengi,mshindi wa pili ameibuka mwanadada Salma Abushiri  (Zanzibar) na watu ni Wababa Mtuka (Dar).

Mshindi wa shindano la  Epiq Bongo Star Search 2012 (EBSS),Walter Chilambo (Dar) akiwashukuru wapenzi na msahabiki wake waliompigia kura na hatimaye kuibuka mshindi wa shindano hilo,lililofanyika ndani ya ukumbi wa Diamond jubilee.

Baadhi ya mashabiki wa mshindi wa shindano hilo la EBSS,Walter Chilambo wakishangilia kwa shangwe na vifijo mara baada kutamkwa yeye ndiye kinara katika kilele cha shindano hilo lililovuta hisia za watu wengi.

Mkurugenzi wa kampuni ya Benchmark Productions Limited, na Jaji Mkuu wa Shindano la  Epiq Bongo Star Search 2012 (EBSS), akiwa amemkumbatia mshindi wa shindano hilo Walter Chilambo ndani ya ukumbi wa Diamond,Chilambo ameibuka na kitita cha shilingi Milioni 50.

Msanii Barnaba akiimba na mmoja wa washiriki wa shindano la Epiq Bongo Star Search 2012 (EBSS).

Mshiriki wa EBSS NshomaNg'hangasamala akiimba moja ya wimbo wake jukwaani.

Mwanadada Salma Albushiri akiimba kwa hisia huku akipiga gitaa mbele ya mashabiki wake waliofika kumshuhudia ndani ya ukumbi wa Diamond.

Mapouda.! majaji hawaishi vituko. Picha kwa Hisani ya Father Kidevu Blog

Friday, November 9, 2012

WAKATI LIGI IKIFIKIA NUSU MSIMU - KAMATI YA LIGI IMELETA MABADILIKO GANI?? - AZAM NA KASUMBA ZA SIASA ZA SOKA - SIMBA UMOJA NDIO UDHAIFU WAO



Jumapili tutashuhudia mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ya Vodacom ukimalizika kwa timu mbalimbali zikijitupa uwanjani, sasa wadau wenzangu sijui tumejifunza nini na kuna tofauti gani na ligi ya mwaka jana au kuongezwa kwa nauli katika mkataba wa Vodacom kwa vilabu vya ligi kuu au kuondolewa kwa nembo ya mdhamini kifuani?


Vilabu vimenufaika na nini au mabadiliko gani yamefanyika kuhakikisha ligi inakuwa na msisimko kulingana na hadhi ya ligi yenyewe?

 Ndio maana mimi tangu mwanzoni sikuwa muumini wa chombo kinachoitwa kamati na sababu ninazo. 

Tumeshuhudia ligi hii inayosimamiwa na kamati imeanza bila ya vilabu kusaini mkataba wa udhamini kutoka Vodacom kitu ambacho kikapelekea African Lyon kusaini mkataba na kampuni ya simu ya Zantel bila ya kujua kwamba katika mkataba wa Vodacom sehemu inayoeleza kuwa vilabu vinaweza kutafuta wadhamini lakini wasiwe washindani wa kibiashara na Vodacom na wana haki katika hilo pale African Lyon waliteleza kwa sababu umeshakubali kuolewa masharti ya ndoa uyafuate. 

Sasa basi sitaki kufika mbali dhamira yangu kwa wadau ni kueleza ni jinsi gani kamati haiwezi kutufikisha pale tulipotarajia kwa sababu ina watu wenye utashi zaidi katika mambo kama ya siasa, na mpira wa siku hizi ni sayansi na biashara sio siasa, sasa kama tutaendelea kuikumbatia kamati ya ligi tutakuwa tunafanya makosa sana nauliza swali kamati hii imefanya nini kuhakikisha vilabu vya ligi daraja la kwanza linachezwa kwa ufanisi?.


Madaraka achieni watu nyie endeleeni na siasa yenu kama kamati lakini pawe na chombo chenye wataalamu wa biashara, madalali wa kutafuta wadhamini mbona mambo yanawezekana lakini sisi tunataka mambo yote tuyafanye sisi eti kwa ajili kiongozi unakuta hapa katika mpira wetu mmoja ni Simba yeye, Yanga yeye, TFF yeye, chama cha mpira labda Rukwa yeye na kwenye kamati yeye, inakuwa unafiki, hivi vyeo vingine peaneni lakini ukweli ubakie palepale ligi yetu inahitaji kusimamiwa na watu wenye taaluma sio uzoefu.


 Kingine tumejifunza nini kwa timu yetu ya Azam nayo imejikita katika siasa, eti inamaliza ligi kwa staili ambayo ni aibu kwa timu kama Azam na siku za hivi karibuni ndio timu pekee niliyokuwa naitarajia itatoa somo matokeo yake ndio hivyo duuuh hii ni hatari jipangeni mmejaaliwa kila kitu hamna sababu ya kushindwa. Yanga nao walianza vibaya wamejipanga na Simba nao walianza vizuri lakini wametoka nje ya mchezo kwa sababu si wamoja.
Viongozi wa Simba SC
Lazima kuna namna, nimejaribu kufanya utafiti na kugundua kwamba uongozi wa samba samba sio collectively yaani wanafanya kazi kwa mafungu wapo kama kambale wote wana sharubu hajulikani jike wala dume yani mpaka mwanachama anaweza kusema Kaseja sio kipa!!!!! tuache uhuni tengenezeni umoja kwanza kwani utengano ni udhaifu, bila Simba imara Soka la kibongo litayumba, angalieni mlipojikwaa basi lakini jibu nimekupeni na mnalijua viongozi sio wamoja.

 Kuna mwandishi mmoja anaitwa J.K. Rowling, katika Harry Potter and the Goblet of Fire aliandika “We are only as strong as we are united, as weak as we are divided.” Mwisho namalizia na ndugu zangu wagombea wa DRFA jamani mkifukuza chizi ondoeni na makopo yake udambwi udambwi wa makato unaenda wapi mimi ndio maana sijachukua form nitaeleza maana yake nini wiki ijayo. 

Idd GodiGodi

BREAKING NEWS! AGGREY MORRIS AONDOLEWA KWENYE KIKOSI CHA AZAM.

Baada ya leo asubuhi kutoa maoni kwa klabu ya AZAM ya kumuondoa kikosini nahodha Aggrey Morris kama kweli alihusika na tuhuma za rushwa,hatimae hivi punde nimepata taarifa kutoka kwenye chanzo cha kuaminika beki huyo na nahodha wa timu hiyo ameondolewa kwenye kikosi na kocha Stewart Hall.
Tayari Morris alikuwa mjini Tanga pamoja na kikosi cha Azam kinachojiandaa na mchezo dhidi ya JKT MGAMBO hapo kesho amerejeshwa jijini Dar Es Salaam,kocha Stewart Hall amemuondoa nahodha huyo kikosini baada ya kuonyeshwa vielelezo vya wachezaji waliohusishwa na tuhuma za kuchukua rushwa ili kuifungisha Azam, kitendo ambacho kimewaudhi sana wachezaji wa Azam.

I SALUTE YOU AZAM KTK HILI!Nawaomba kamwe msirudi nyuma it's time now kwa ajili ya kutokomeza rushwa michezoni hasa mchezo wa soka.

PICHA YA SIKU: TAKWIMU ZA MCHEZO WALIOFUNGWA BARCELONA NA CELTIC


SANTI CAZORLA, JUAN MATA NA MICHU WANUNUA HISA ZA UMILIKI WA TIMU NCHINI HISPANIA

Tumekuwa tukisikia namna wanamichezo wanavyotumia vibaya utajiri wao wanaopata katika fani zao, hasa wanasoka - huku wakiacha majukumu yao ya kurudisha kwa jamii katika kusaidia soka lizidi kupiga mbele zaidi, lakini jambo ambalo nimelisikia sasa limenifurahisha kiasi kujua kwamba kundi la wachezaji wa zamani wa Real Oviedo wamejiunga pamoja kuisadia timu yao inayokabiliwa na ukata mkubwa.

Santi Cazorla, Juan Mata na Michu wote ni wachezaji wa zamani wa Oviedo wakiwa wamekulia na kujifunza soka katika klabu hiyo na tunaambiwa kwamba watatu hao wamenunua hisa katika klabu hiyo ili kuikoa klabu hiyo kukaa vizuri kibiashara. 

Klabu hiyo ya Hispania, ambao kwa sasa wapo katika nafasi ya tano katika daraja la tatu la soka la Spain, ndio klabu ambayo Mata, Michu, na Cazorla wote walianzia maisha yao ya soka la kisasa katika klabu hiyo, Michu kwa kipekee zaidi alitumia muda mrefu zaidi katika klabu hiyo kabla ya kwenda Celta Vigo B.

Mie, Mata na Cazorla wote tumenunua hisa, lakini haitakuwa sawa kwangu mimi kusema ni hisa kiasi gani. Tumejaribu kuisadia klabu yetu ambayo wote tumeichezea," alithibitisha Michu.

Uchumi wa Hispania upo katika hali mbaya sana na klabu inahitaji kiasi kinachokaribia €2m ili kuweza kuendelea. Watu wengi wamenunua hisa  na tumaini letu sasa hali ya uchumi itaimarika kiasi mpaka kufikia mwisho wa ununuzi wa hisa tarehe 17 mwezi huu. 
"Hii ni klabu yangu ya nyumbani, klabu niipendayo, hivyo naamini mchang wetu na watu wengine utatosha kuisadia."

KUMUACHA AGGREY MORRIS KUNDINI KUTAIPELEKA AZAM KUBAYA

Siku mbili zilizopita klabu ya Azam FC ilifanya maamuzi magumu ya kuwasimamisha wachezaji wake watatu kati ya sita waliotuhumiwa kula njama na kupokea rushwa kutoka kwa vilabu vya kulwa na doto wa soka la Tanzania ili LambaLamba ifungwe na vigogo hao wa soka nchini.

Wachezaji wa Azam FC waliotuhumiwa na baadhi kukiri na kuchukua rushwa hiyo ni pamoja na Deo Munishi ‘Dida’ na mabeki Said Mourad na Erasto Nyoni ambao mpaka sasa wameshasimamishwa - huku nahodha Aggrey Morris ambaye nae ameshakiri kupokea mlungura akiachwa bila kuadhibiwa kwa sababu wanazozijua wenyewe Azam. Pia kuna wachezaji wengine wawili viungo wapo katika mkumbo huo lakini bado hawajatajwa.

Sasa ikiwa imepita siku moja baada ya kuibuka kwa mambo hayo ndani ya klabu ya Azam, kuna taarifa za kuaminika kwamba suala la kutoadhibiwa kwa nahodha Aggrey Morris ambaye ameshakiri kushiriki katika zoezi la upokeaji rushwa limeanza kuleta mgawanyiko mkubwa ndani ya kikosi cha Azam FC.

Ripoti kutoka ndani ya chanzo kilichopo karibu na kikosi cha timu hiyo kinasema kundi kubwa la wachezaji wa Azam wamechukizwa sana na kitendo walichofanya wenzao na wamefurahia kusimamishwa kwa Dida, Nyoni na Morad lakini bado wamekataa katukatu kuendelea kuongozwa na mchezaji ambaye amekiri kuchukua mlungura ili timu ifungwe au kucheza vibaya. Hivyo wanahitaji Aggrey Morris nae aadhibiwe na hata ikiwezekana kuporwa unahodha kwa sababu anakosa sifa ya kuwa kiongozi.

Hata hivyo uongozi wa klabu hiyo bado umeshindwa kufanya lolote la kumuadhibu Aggrey Morris, jambo ambalo kwa hakika linaleta mgawanyiko kwenye timu na kuweza kuiharibia Azam FC mipango yake hai ya kutaka kubeba ubingwa wa msimu huu pia kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa ambayo mwaka huu ndio itakuwa mara ya kwanza kwa klabu hiyo kucheza michuano hiyo tangu ilipopanda daraja takribani misimu minne iliyopita.

Kwa maoni yangu ikiwa Azam wantaka timu iwe na umoja na kuweza kuwa na mafanikio ya uwanjani lazima washughulikie suala hili katika namna inayofaa. Kama Aggrey Morris amekiri kuchukua rushwa basi aadhibiwe kama wengine ili kuwatendea haki wote walioadhibiwa na kuleta uwiano ndani ya timu. Endapo watamuacha kama ilivyo sasa bila kumuadhibu wala kuchukua hatua yoyote dhidi yao basi kuna wasiwasi mkubwa sula hilo likaleta ufa ndani ya timu - pia inaweza ikajenga tabia hiyo kwa wachezaji wengine - kwani wote wanajua kama fulani aliachwa kwa kosa kama hili basi hata yeye akifanya ataachwa kutokana labda na nafasi yake ndani ya kikosi cha Azam FC. Nini matokeo ya hali kama hii?

Matokeo yake timu itafanya vibaya na kuendelea kuzama katika siasa za mpira wa Kulwa na Doto, mwishowe matatizo ya vitu kama hivi ndio yanapelekea soka letu nzima kuoza na Tanzania kuwa nyuma kwa maendeleo ya mchezo huu.

Nawasilisha.    

SERGIO RAMOS: BILA MAMA NINGEKUWA NACHEZA MCHEZO WA KUPIGANA NA NG'OMBE NA SIO SOKA

 
Sergio Ramos amevunja ukimya juu ya ushangiliaji wake wa alioufanya wakati akishangilia ubingwa wa ulaya wa Spain mwaka huu.
Mlinzi huyo wa Real Madrid hajawahi kuficha hisia zake alizonanzo juu ya mchezo wa kupigana na ng'ombe ambao ni maarufu huko kwao Spain. Baada ya mafanikio yake ya uwanjani Sergio huonekana akicheza dansi za aina fulani huku akiwa na kitambaa kikubwa, lakini sasa anasema kwamba chaguo lake lilikuwa kucheza mchezo huo badala ya soka kama mama yake asingeingilia kati.
"Unapokuwa mdogo ni muhimu kuwa na ndoto," anaiambia AS.
"Ndoto yangu kubwa siku zote ilikuwa ni kuwa mcheza mchezo wa kupigana na ng'ombe au mwanasoka, lakini mama yangu hakupenda mie nicheze mchezo huo kwa sababu ni hatari, hivyo nikaona bora nicheze soka kwa sababu haukuwa mchezo wa hatari kama wa kupigana na ng'ombe."

TAIFA STARS YAHAIRISHA MECHI YA SIMBA VS TOTO NA NYINGINE NNE - YANGA VS COASTAL YABAKI VILEVILE

Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imefanya mabadiliko madogo ya ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom ili kupitisha mechi ya kirafiki ya kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kati ya Taifa Stars na Kenya (Harambe Stars) itakayochezwa Novemba 14 mwaka huu jijini Mwanza.
Mechi tano za ligi hiyo zilizokuwa zichezwe Novemba 11 mwaka huu, zimerejeshwa nyuma kwa siku moja ambapo sasa zitafanyika Novemba 10 mwaka huu. Mechi hizo ni Simba vs Toto Africans (Uwanja wa Taifa), Kagera Sugar vs Polisi Morogoro (Uwanja wa Kaitaba) na Oljoro JKT vs Ruvu Shooting (Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid).
Nyingine ni Tanzania Prisons vs JKT Ruvu (Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine) na African Lyon vs Mtibwa Sugar (Azam Complex). Mechi ya Mgambo Shooting vs Azam (Azam Complex) yenyewe itachezwa Novemba 10 mwaka huu kama ilivyokuwa imepangwa.
Nayo mechi ya Coastal Union vs Yanga (Uwanja wa Mkwakwani) itabaki Novemba 11 mwaka huu kwa vile Novemba 10 mwaka huu uwanja huo utakuwa na mechi nyingine. TFF imepanga utaratibu wa kuwapata kwa wakati wachezaji wa Yanga walioitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars.
Mabadiliko mengine ni ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ambapo mechi ya Villa Squad vs Transit Camp iliyokuwa ichezwe Novemba 8 mwaka huu sasa inachezwa Novemba 9 mwaka huu, na ile ya Novemba 7 mwaka huu kati ya Burkina Faso na Small Kids inachezwa Novemba 9 mwaka huu. Viwanja ni vilevile.
Kamati ya Ligi imelazimika kufanya mabadiliko hayo kutokana na viwanja husika kuwa na mechi nyingine, na vilevile Small Kids kupata matatizo ya usafiri kutoka mkoani Rukwa kwenda Morogoro.

Thursday, November 8, 2012

THE LEGEND IS BACK DJ JD AT SYNERGY LOUNGE THIS SATURDAY !

CLOUDS MEDIA YAITANDIKA ETIHAD FC 3-2 JANA USIKU


Kikosi cha The Dream Team kutoka Clouds Media kilichoanza katika ya ufunguzi wa uwanja wa Etihad Stadium uliopo mwanayamala B. Katika mechi ya jana iliyochezwa usiku uliisha kwa Clouds FM Dream Team kuitandika Etihad kwa mabao 3-2 yaliyofungwa na Shaffih Dauda, Anatory Kabezi na Kikucha.
Kikosi cha Etihad FC kilichoanza jana usiku dhidi ya Dream Team
Waamuzi wa mchezo wa jana wakiongozwa na Othmani Kazi


Mgeni wa heshima Diwani wa kata ya Makumbusho Mheshimiwa Ali Haroub Mohamed akiikagua timu ya Etihad.
Nahodha wa Dream Team Mbwiga Mbwiguke akisalimiana na mgeni rasmi.



    Mwenyeji wetu Mwalimu Mkuu wa shule ya Mwananyamala B, Bwana Bambaza Odas,Mr Bambaza alitusaidia sana kwenye mchakato mzima wa ukarabati wa uwanja huu,



Ibrahim Masoud Maestro akitoa mawaidha kwa wachezaji wa Dream Team wakati wa mapumziko






KULWA NA DOTO WALETA KIZAZAA AZAM - WATUHUMIWA KUWAPA RUSHWA SAID MORAD, NYONI, NA DIDA ILI WAIFUNGE AZAM

Habari za kuaminika kutoka katika klabu ya Azam ni kwamba imewasimamisha nyota wake watatu wa kikosi cha kwanza kutokana madai ya kuchukua rushwa katika mchezo miwili ambayo timu hiyo ilifungwa na kulwa na doto wa soka la Tanzania.

Wachezaji ambao wametuhumiwa katika kesi wapo sita, lakini Said Morad, kipa Deogratius Munishi 'Dida' na kiungo Erasto Nyoni ndio ambao wamesimamishwa kuichezea Azam.

Chanzo cha kuaminika kutoka Azam kinasema kwamba, kuna wachezaji wengine watatu akiwemo nahodha Aggrey Morris na viungo wa kutumainiwa wawili wa timu hiyo nao wapo katika kesi hiyo, lakini kutokana na umuhimu wao katika timu imekuwa shida kidogo kuweza kuwasimamisha.

"Dida amesimamishwa kwasababu pengo lake litazibwa na Mwadini, wakati Saidi Morad nafasi yake yupo Owino, na pia Nyoni yupo dogo Nuhu. Hao wengine wameepuka adhabu ya kusimamishwa kwa sababu wataidhoofisha timu."  - Kilisema chanzo hicho cha habari.

Wednesday, November 7, 2012

AZAM YAIKUNG'UTA OLJORO NA KUISHUSHA SIMBA MPAKA NAFASI YA 3

Kiungo wa Azam, Kipre Bolou (wa pili kushoto) akimiliki mpira huku akichungwa na wachezaji wa JKT Oljoro wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam leo.
AZAM imeiengua Simba katika nafasi ya pili ya msimamo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kushinda goli 1-0 dhidi ya JKT Oljoro kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam leo.


Ushindi huo unamaamsha kwamba kwamba Azam sasa imefikisha pointi 24, mbili nyuma ya vinara Yanga wenye pointi 26, na moja juu ya watetezi Simba wenye pointi 23.



Coastal Union nayo imeutumia vyema uwanja wa nyumbani wa Mkwakwani, Tanga baada ya kushinda 1-0 dhidi ya timu inayoshika mkia ya Polisi Morogoro na kufikisha pointi 22, moja tu nyuma ya Simba.


Nayo Mtibwa imeshinda 1-0 dhidi ya JKT Ruvu kwenye uwanja wa nyumbani wa Manungu, Turiani katika mechi nyingine ya ligi iliyowashuhudia wenyeji wakimaliza wakiwa tisa uwanjani baada ya nyota wao wawili Vincent Barbanas na Salum Machaku kutolewa kwa kadi nyekundu
na refa Ibrahim Kidiwa wa Tanga kutokana na kutoa lugha chafu.

Mtibwa imebaki katika nafasi ya sita ikiwa na pointi 19, moja nyuma ya Kagera Sugar yenye pointi 20 katika nafasi ya tano.


Matokeo hayo yanafanya mchuano kileleni mwa msimamo kuwa mkubwa na wa kiushindani zaidi huku timu zikiachana kwa pointi chache -- Yanga (pointi 26), Azam (24), Simba (23), Coastal (22), Kagera (20) na Mtibwa (19) baada ya timu zote kucheza mechi 12 kila moja.   


Daniel Lihanga aliifungia Coastal goli lao la ushindi katika dakika ya 3 na kuifanya timu hiyo ya Tanga ipande hadi nafasi ya nne ikiwa na pointi 22, moja tu nyuma ya Simba yenye pointi 23.


Issa Rashid alisherehekea kuitwa na kocha Kim Poulsen kwenye kikosi cha timu ya Taifa Stars kilichotajwa leo kwa kufunga goli lililoipa ushindi timu yake ya Mtibwa dhidi ya JKT Ruvu kwa juhudi binafsi akikimbia na mpira kutokea kwenye nusu yake ya uwanja hadi goli katika dakika ya 26.


Kwenye Uwanja wa Chamazi, Kipre Tchetche alifunga goli lake la saba msimu huu na kumfikia kinara wa mabao wa ligi Didier Kavumbagu wa Yanga katika dakika ya nne kwa njia ya penalti iliyotolewa na refa Livingstone Lwiza kutoka Kagera baada ya Yasin Juma kuunawa mpira ndani ya boksi, lakini wenyeji Azam walimaliza wakiwa 10 baada ya Himid Mao kutolewa kwa kadi nyekundu katika dakika ya 88 kutokana na kumcheza rafu mchezaji wa Oljoro.


Mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo unamalizika wikiendi hii kwa timu zote 14 kushuka uwanjani ambapo miongoni mwao, vinara Yanga watakuwa wageni wa Coastal Union kwenye Uwanja wa Mkwakwani Tanga, Azam watawavaa Mgambo Shootings, Simba itawaalika Toto Africans.



  PICHA NA HABARI KWA HISANI YA http://straikamkali.blogspot.com/)

PAMOJA NA KUAMBIWA KIWANGO KIMESHUKA - KASEJA AITWA STARS - MAKINDA EDO CHRISTOPHER NA MSUVA NAO NDANI

Kikosi kamili cha wachezaji hao 22 waliotangazwa na Poulsen akiwa jijini Mwanza leo ni:
Makipa: Kaseja (Simba) na Deogratias Munishi (Azam)

Mabeki: Kelvin Yondani (Yanga), Aggrey Morris na Erasto Nyoni (Azam), Issa Rashid (Mtibwa), Nassoro Masoud ‘Cholo’, Shomari Kapombe na Amir Maftah (Simba).

Viungo: Salum Abubakar “Sure Boy” (Azam), Amri Kiemba, Mwinyi Kazimoto, Ramadhan Singano na Mrisho Ngassa (Simba), Athuman Iddi ‘Chuji” na Frank Domayo (Yanga) na Shaaban Nditi (Mtibwa Sugar).

Washambuliaji: John Bocco (Azam), Simon Msuva (Yanga), Christopher Edward (Simba) na Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe)

SIKU KAMA YA LEO MIAKA 26 ILIYOPITA - SIR ALEX FERGUSON ALIANZA KAZI MANCHESTER UNITED

ADRIANO ATEMWA TENA NA FLAMENGO BAADA YA KUKATAA KURUDI UWANJANI MWAKA HUU

Mkurugenzi wa Flamengo Zinho amesema kwamba klabu hiyo ya Brazil haina mpango kumsaini upya Adriano wakati mshambuliaji huyo wa kibrazil atakaporudi uwanjani mwaka 2013.

Zinho alisema jana Jumanne itakuwa ngumu sana kwa klabu hiyo kumrudisha Adriano mara baada ya mapema leo baada ya mchezaji kutangaza kwamba hatorudi uwanjani mpaka mwakani.
 Mkurugenzi huyo alisema hataacha kujaribu kumsaidia  Adriano mwenye miaka 30 kurudi kwenye hali yake ya kawaida katika maisha yake binafsi, lakini kikazi amenawa mikono yake na kufikia kikomo.

Akiwa anasumbuliwa na matatizo ya nje ya uwanja kwa muda mrefu, Adriano aliacha kufanya mazoezi mara nyingi tangu alipojiunga na Flamengo mwezi wa August baada ya kufukuzwa na Corinthians kwa kutokuwa makini na kujitunza juu ya majeruhi yaliyokuwa yakimsumbua.

Adriano amesema uamuzi wa kutocheza mwaka huu ni mzuri kwa kw na klabu pia. 

MJADALA:NI KWELI YANGA WALINYIMWA PENATI ?

SDTV: YANGA 2:0 AZAM FC

BAADA YA KIPIGO NA VURUGU ZA WANACHAMA: UONGOZI WA SIMBA WAMTETEA KASEJA - WAMTAKA MILOVAN NA BENCHI LA UFUNDI KUPELEKA RIPOTI YA CHANZO CHA MATOKEO MABOVU

UONGOZI wa Simba SC unapenda kuzungumza yafuatayo kuhusiana na matukio ya karibuni kuhusiana na klabu ya Simba.

  1. Uongozi umesononeshwa na matokeo ya siku za karibuni ya timu ya Simba hususani yale ya kufungwa mabao 2-0 na Mtibwa Sugar ya Morogoro. Kutokana na hali hiyo, Kamati ya Utendaji ya Simba imeliagiza benchi la ufundi la Simba kutoa ripoti kuhusiana na mwenendo wa timu katika mechi za karibuni.
Ikumbukwe kwamba Simba ilianza ligi kwa vishindo na hadi kufikia mechi ya 12, ilikuwa ikiongoza ligi na ilikuwa timu pekee ambayo haikuwa imepoteza mechi.

Mara baada ya ripoti ya benchi la ufundi kukamilika, Kamati ya Utendaji ya Simba itakutana na kutoa maamuzi kuhusiana na yaliyomo kwenye ripoti. Kutokana na hali hiyo, uongozi unaomba wapenzi na wanachama wake kuwa watulivu katika kipindi hiki ambapo uongozi na benchi la ufundi linatafuta suluhisho la kudumu kuwezesha timu kuendelea kushinda.

Hata hivyo, uongozi wa Simba unasisitiza kwamba hakuna kiongozi yeyote wa Simba –kuanzia wa juu zaidi hadi wa chini zaidi, ambaye amejiuzulu au kuachia ngazi ndani ya klabu.

Ifahamike kwamba uongozi huu ulipewa dhamana na wanachama miaka minne iliyopita ya kuiongoza klabu kisasa na kuipa maendeleo endelevu kwa kipindi hicho.

Chini ya uongozi huu, Simba ilikuwa mshindi wa pili misimu miwili iliyopita (ikiwa pointi sawa na mabingwa ila ikizidiwa kwa pointi, ilikuwa mabingwa msimu uliopita, iliingia hatua ya 16 bora michuano ya CAF, imesajili wachezaji msimu huu kwa fedha zake yenyewe (miradi mbalimbali) na inaendesha timu tatu za vijana.

Bado kuna kazi za kufanya na uongozi unatambua hilo. Ndiyo maana uongozi hauamini kwamba maneno mabaya yanayosambazwa dhidi ya viongozi yanatoka kwa wanachama wake. Kazi nzuri ya uongozi huu inaonekana na iko dhahiri.
Uongozi wa Simba unaomba wapenzi na wanachama wake kuwa wamoja katika kipindi hiki ili kuwezesha ushindi kupatikana dhidi ya Toto African ya Mwanza Jumamosi ijayo.


2. Kuhusu mchezaji Juma Kaseja

Uongozi umesikitishwa na vitendo ambavyo baadhi ya washabiki walivifanya dhidi ya nahodha wa Simba, Juma Kaseja. Washabiki hao walimtukana, kumkashifu, kumdhihaki na kumtishia maisha mchezaji huyo mara baada ya mechi dhidi ya Mtibwa.

Kaseja ni miongoni mwa wachezaji wanaoheshimika sana ndani na nje ya nchi. Vitendo vya kumkashifu si vya kiungwana na uanamichezo. Nahodha huyu ameitumikia Simba kwa moyo mmoja na ni mmoja wa wachezaji wenye kuheshimika sana miongoni mwa wachezaji.

Hatua ya kumtukana inaharibu heshima ya klabu. Ni mchezaji mgani mzuri atataka kujiunga na Simba iwapo ataona Kaseja anafanyiwa hivyo? Benchi la ufundi la Simba ni makini na iwapo kutakuwa na tatizo lolote la kiuchezaji, litafanya mabadiliko.

Kama Kaseja angekuwa anapendelewa Simba, asingechaguliwa kuwa kipa namba moja wa Taifa Stars na nahodha pia.

Tunachukua fursa hii kutangaza kwamba uongozi wa Simba, kuanzia sasa, hautavumilia matusi kwa wachezaji au viongozi wake. Wote watakaobainika kufanya matendo haya, sheria itachukua mkondo wake.

Imetolewa na

Ezekiel Kamwaga
Ofisa Habari
Simba SC

ARSENAL YASHINDWA KURUDISHA KISASI KWA SCHALKE - ZATOKA SULUHU



szólj hozzá: Schalke vs Arsenal 2:2 GOALS HIGHLIGHTS

MANCINI HALI YAZIDI KUWA TETE - CITY IKITOKA SARE YA 2-2 NA AJAX NA KUBAKI MKIANI



M2-2A www.fasthighlights.com by fasthighlights-2013

OZIL AIOKOA REAL MADRID NA KIPIGO CHA PILI KUTOKA KWA DORTMUND

PEPE
R2-2D www.fasthighlights.com by fasthighlights-2013

DADA WA MSHAMBULIAJI WA KIBRAZIL HULK ATEKWA NYARA

Dada wa mchezaji wa  Zenit St Petersburg  Hulk ametekwa nya nchini Brazil, maofisa wa kituo cha polisi cha eneo la Campina Grande wamethibitisha.

Angelica Aparecida Vieira alikuwa nje ya mgahawa ambapo anafanya kazi siku ya Jumatatu katika eneo la Brazilian City.

Msichana huyo mwenye miaka 22 alichukuliwa kutoka kwenye gari lake mwenyewe na kuwekwa kwenye gari la watekaji kwa mujibu wa meneja wa mgahawa Helio da Silva ambaye alishuhudia tukio hilo, na alipata mshtuko wa moyo na ikabidi apelekwe hosptali lakini sasa ameachiwa.

Polisi bado hawajathibisha ni watu wangapi walihusika na utekaji nyara huo, ambao ulitokea muda wa 8 mchana kwa muda wa Brazili.

Hulk hakuwa amepangwa kucheza mechi yao ya leo usiku ya Champions League dhidi ya Anderletch kutokana na majeruhi ambayo yatamuweka nje ya dimba kwa wiki mbili.

CRISTIANO RONALDO: LIONEL MESSI SIO RAFIKI YANGU - NA HATUNA MATATIZO YOYOTE

Cristiano Ronaldo amesema ana mahusiano ya kazi tu na mpinzani wake Lionel Messi  na sio marafiki na nyota huyo wa Argentina na Barcelona

Wawili hao wamekuwa wakishindanishwa kwa kila kitu  katika miaka ya hivi karibuni, huku wachezaji wote wawili wakicheza kwa jitihada kubwa kushinda makombe na tuzo binafsi. Hta hivyo japo anakiri kwamba hakuna urafiki wa karibu, Ronaldo anasisitiza hawana ugomvi na Lione Messi na pia akazungumzia heshima yake kwa mshambuliaji huyo wa Barcelona. 

"Yeye [Lionel Messi]ni mchezaji mzuri na mkubwa sana ," Ronaldo aliiambia beIN sport. "Nina mahusiano ya kikazi tu na yeye kama niliyonayo na wachezaji wengine. Messi sio rafiki yangu. kwa sababu hatushei chumba cha kubadilishia nguo. Namheshimu kama mchezaji. Sisi sio marafiki, japokuwa tuna mahusiano ya kikazi tu.

"Hakuna ugomvi wowote kati yetu japokuwa kuna baadhi ya watu wanajaribu kutengeneza hali ya namna hiyo, na sio kitu kipya kimekuwa kikitokea kwa takribani miaka mitano iliyopita. Siwezi kukizuia."

Ronaldo aliendelea mbele na kusema kwamba anaweza kucheza na Messi timu moja, kitu ambacho hata hivyo amekiri ni kigumu.
"INaweza nikacheza vizuri sana na yeye ikiwa tu atasaini kujiunga na Real Madrid, lakini hilo ni gumu sana," anasema Ronaldo.

Tuesday, November 6, 2012

CESC FABREGAS NA TUHUMA ZA KUVUNJA NDOA YA WATU

'He stole her from me': Her ex-husband only found out about the relationship after he spotted her picture in the newspaper while on holiday with FabregasCesc Fabregas na girlfriend Daniella Semaan wamekuwa kwenye mapenzi mazito katika kipindi cha miezi kadhaa iliyopita. Walionekana wakila raha hivi karibuni wakati wa kipindi cha kiangazi huko Italy - lakini sasa kidudu mtu kimeanza kuingia kwenye mapenzi yao.

Aliyekuwa mume wa mchumba wake Fabregas, Millionea Elie Taktouk amejitokeza na kusema kwamba ulikuwa ndio wakati huo wa mapumziko ya kiangazi alipogundua mkewe anamsaliti - wakati wakiwa wanajaribu kupata mtoto wa tatu.

Millionea huyo amekuwa akizungumzia maumivu aliyoyapata juu ya usaliti wa mkewe aliyekuwa akiufanya na mchezaji wa Barcelona mwenye miaka 25.
In love: Cesc Fabregas and Daniella Semaan were spotted in an intimate embrace on holiday in Italy earlier this summer

Akiongea na The Sun, Mfanyabiashara huyo alisema kwamba aligundua juu ya usaliti wa mkewe na nahodha huyo wa zamani wa Arsenal alipoona picha za wawili hao kipindi cha kiangazi mwaka jana.
Danielle Semaan, 38, na Elie wameshatalikiana, kama ambavyo anasema kwamba baada ya kuona picha za mkewe na Cesc, akaona ni bora aachane na mkewe huyo.

Wanandoa hao wawili wana watoto wawili, mtoto wa kiume mwenye miaka 11 na wa kike mwenye miaka 8.


'Disgusted': Eli Taktouk, here pictured on the left with an unidentified friend, said he wants nothing to do with his ex Daniella
Eli Taktouk(kushoto), akiwa na rafiki yake.