Habari za kuaminika kutoka katika klabu ya Azam ni kwamba
imewasimamisha nyota wake watatu wa kikosi cha kwanza kutokana madai ya kuchukua rushwa katika mchezo miwili ambayo timu hiyo ilifungwa na kulwa na doto wa soka la Tanzania.
Wachezaji ambao wametuhumiwa katika kesi wapo sita, lakini Said Morad, kipa Deogratius Munishi
'Dida' na kiungo Erasto Nyoni ndio ambao wamesimamishwa kuichezea Azam.
Chanzo cha kuaminika kutoka Azam kinasema kwamba, kuna wachezaji wengine watatu akiwemo nahodha Aggrey Morris na viungo wa kutumainiwa wawili wa timu hiyo nao wapo katika kesi hiyo, lakini kutokana na umuhimu wao katika timu imekuwa shida kidogo kuweza kuwasimamisha.
"Dida amesimamishwa kwasababu pengo lake litazibwa na Mwadini, wakati Saidi Morad nafasi yake yupo Owino, na pia Nyoni yupo dogo Nuhu. Hao wengine wameepuka adhabu ya kusimamishwa kwa sababu wataidhoofisha timu." - Kilisema chanzo hicho cha habari.
Azam wanatafuta visingizio tu. Kwanza Nyoni hakuwepo kwenye mechi na Simba. Bocco alicheza ovyo na Yanga mbona hajahusishwa na hiyo rushwa? Wanatakiwa kuelewa kwamba walifungwa na timu bora kabisa za Tanzania! Kama wana uhakika kwamba wachezaji hao walichukua rushwa then everyone concerned must be suspended.
ReplyDeleteHawa nao wameshaingia ktk siasa za kulwa na doto coz hii timu ilivyoanza 2lijua kuwa wamekuja kulea mapinduzi ya soka lakini ss hv watapotea hawana muda mrefu wanaacha kucheza soka wanaendekeza siasa.
ReplyDeleteAzam nao wameshakuwa na Majungu..Wanatakiwa kufahamu Simba na Yanga nni team zipofit kiuwezo wa mpira kuliko wao,ata ukijaribu kucheki record za Azam kuzifunga hizo team ni za kuesabika......kabla ya kuanza kujitetea lazima wajaribu kuchungulia record zao dhidi ya hizi team,Mbona wao wamemfunga coast 4-0 lkn coast wamekaa kimya na ukiangalia coast kwa ss wapo poa sn kisoka.Azam bado mna muda wa kujipanga kisoka na siyo majingu kama sisi Simba na Yanga.
ReplyDelete