Search This Blog

Saturday, February 11, 2012

MAN UNITED WAIUA LIVERPOOL, HENRY AIAGA VIZURI EPL. CHELSEA WAENDELEA KUFUNGWA .


Inaonekana leo ni siku ya rangi nyekundu kutamba, baada ya mnyama kuwaua Azam, nchini Uingereza klabu ya Manchester United imeibamiza goli 2-1 mahasimu wao Liverpool – huku Wayne Rooney akifunga magoli yote ya United na Luis Suarez akifunga la kufutia machozi.
Arsenal nao wakaifunga Sunderland 2-1, babu chogo Thierry Henry akitupia kambani magoli yote.
Chelsea wakafungwa na na Everton kwa 2-0, shukrani zimuendee Steven Piennaar.

SIMBA WAITAFUNA AZAM TAIFA LEO.


Klabu ya Simba ya Dar es Salaam leo imekata ngebe za wapinzani wao Azam FC baada ya kuwafunga katika mechi ya Vodacom Premier League, huku wana msimbazi wakitandaza soka safi katika pitch ya uwanja wa taifa jijini.

Magoli ya Simba yalifungwa na Emmanuel Okwi  katika dakika ya 31 kwa shuti hafifu lilowapita mabeki wa Azam na kumzidi ujanja kipa Mwadini Ally.

Baadae katika kipindi cha pili tena Okwi aliziona tena nyavu za Azam katika dakika ya 65, baada ya kupkea mpira mrefu uliowapita mabeki wa Azam na kumkuta Okwi aliyemchambua Mwadini na kutikisa nyavu.

Kwa matokeo hayo Simba wamerudi kileleni wakiwa na pointi 37 lakini wakiwa wamewazidi mchezo mmoja Yanga wenye pointi 34.

WEMA SEPETU: LIVERPOOL LEO WANAKUFA 3-0: CHEZEA.... MAN UNITED

Mwanadada ambaye alikuwa Miss Tanzania 2006, Wema Abraham Sepetu amezungumzia mchezo utakaopigwa masaa machache kutoka sasa kati ya timu yake anayoipenda kwa moyo wake wote Manchester United dhidi ya Liverpool.


Wema ametabiri kuwa Liverpool watapokea kipigo cha goli 3-0  kutoka United. "Manchester United leo tunashinda kabisa, tena tunapiga wale wanaojiita majogoo wa jiji 3-0. Magoli yatafungwa na Wayne Rooney, Paul Scholes na Luis Nani."


 


"Mimi ni mshabiki wa Manchester United na nimeanza kuipenda tangu nianze kujua kama ipo ulimwenguni, nilijikuta tu naipenda timu hi. Kwa hapa nyumbani mini naipenda Yanga lakini simjui hata mchezaji mmojawapo wwa timu hiyo, lakini nikisika Yanga kafungwa labda na Simba roho inaniuma sana." aliongea Wema Sepetu.

MAN UNITED VS LIVERPOOL: VITA TANO ZITAKAZOTOKEA KATIKA MECHI YA MAHASIMU HAWA


Moja ya mahasimu wakubwa wa soka nchini Uingereza Manchester United na Liverpool  zinakutana katika uwanja wa Old Trafford masaa machache yajayo.
Mechi hii itaonyeshwa live kwenye nchi karibia 200 na inatazamia kuangalia na watu wapatao millioni 900.
Kama vile haitoshi uhusiano mbaya uliopo baina ya timu hizi 2, na ukizingatia matukio yaliyotokea mechi kadhaa zilizopita, muda mchache ujao tutaona namna Luis Suarez atakavyokutana kwa mara ya kwanza na mashabiki wa United tangua alivyofungiwa mechi 8 baada ya FA kumkuta na hatia ya kumtolea maneno ya kibaguzi mlinzi wa kushoto wa United Patrice Evra.
Hivi hapa ni vita vitano vitakavyotokea masaa machache yajayo at Theatre Of Dreams.

DAVID DE GEA VS ANDY CARROLL
Golikipka kinda wa United kutoka Spain bado hajaweza kuzoea mikikiki ya English premier league.
Maamuzi na utawala wake ndani ya eneo la penati umekuwa maswali kila siku. Kosa lake la hivi karibuni ni lile wakati wa mechi ya FA @Anfield, ambapo mshambuliaji mwenye mwili mkubwa wa Liverpool Andy Carroll aliposimama mbele yake katika kona na kutengeneza pasi ya goli.
Japokuwa, uwezo wa De Gea wa kuzuia mashuti ya mbali pia umekuwa ukizua mashaka, lakini wikiendi iliyopita katika droo ya 3-3 dhidi ya Chelsea aliokoa magoli mawili ya wazi yaliyopigwa na Juan Mata na Gary Cahill na kuhakikisha United wanapata japo pointi @Stamford Bridge.
Mechi ya muda mchache ujao na kama Carroll akiwa uwanjani itatoa picha kama amejifunza kutokana na makosa aliyoyafanya katika mechi ya Anfield walipokutana na Liverpool kwa mara ya mwisho.

PEPE REINA VS WAYNE ROONEY
Hakuna golikipa aliyekuwa na clean sheet nyingi kuliko Pepe Reina mwenye 10 katika Premier league msimu huu.
Spanish goalkeeper ameendelea kuendelea kuwa nguzo ya ukuta wa Liverpool, na ana bahati mbaya kuwa kwa sasa anapambana na Iker Casillas na Victor Valdes kuwania nafasi ya kwanza katika kikosi cha Spain.
Rooney, hivi karibuni amekuwa katika form nzuri, na alikuwa ndio chachu ya mapambano ya United katika kurudisha mabao matatu katika 26 za kipindi cha pili @Stamford Bridge wiki iliyopita.
Kama ataendelea kuwa katika form aliyokuwa nayo wiki iliyopita ama kwa hakika atampa shida kubwa Pepe Reina.
ANTONIO VALENCIA VS LUIS ENRIQUE
Wakati mara nyingi Rooney amekuwa akitengeneza vichwa vya habari, iwe kwa mazuri au mabaya, Valencia siku za hivi karibuni amekuwa akitengeneza vichwa vya habari kama mchezaji bora kabisa wa United msimu huu so far.
Mecuardor  huyu amekuwa chachu ya ushindi wa United msimu huu, kwani ndiye mchezaji mwenye assists nyingi kuliko wote ndani ya United.
Kwa upande mwingine Jose Enrique anategemewa kurudi kutoka kwenye majeruhi baada ya Mhispania huyo kukuosa mchezo wa Jumatatu dhidi ya Spurs.
Enrique kwa sasa ni moja ya mabeki wa kushoto wazuri zaidi duniani, na ndio maana anatajwa kama ndio the best summer signing katika kikosi cha Dalglish, na ndio mtu sahihi wa kupambana na Tony V aliye katika kiwango cha juu.

PAUL SCHOLES VS STEVEN GERRARD
Paul Scholes amereje uwanjani baada ya kustaafu mwishoni mwa msimu uliopita, na amerudi katika wakati ambao United wamekuwa wadhaifu katika safu ya kiungo.
Anakutana na mmoja ya wachezaji wenzie wa England, Steven Gerrard. Nahodha wa Liverpool (na inawezekana ndiye nahodha ajaye wa England) ambaye nae ameipa uhai mkubwa timu yake tangu arejee kutoka kwenye majeruhi on Boxing day.
Hii itakuwa vita ya ujuzi katika kuhakikisha kila mmoja anaisadia timu yake  kushinda.
ALEX FERGUSON VS KENNY DALGLISH

Mechi ya kwanza ya Dalglish katika siti ya moto ya Liverpool iilikuwa dhidi ya mahasimu wao wakubwa Man United katika kombe la FA-raundi ya 3.
The retired manager aliitikia wito wa kumrithi Roy Hodgson akiwa anaponda raha katika boti ya kifahari, na zawadi yake kwa kukatisha starehe zake ilikuwa ni kipigo cha 1-0 walichopta @Old Trafford.

Tangu hapo, mechi zao 3 baina yao na United zote zilifanyika Anfield, huku Liverpool wakishinda 2(moja ya FA na nyingine ya Carling) na United wakipata droo ya 1-1 katika EPL mwezi October mwaka jana, mechi ambayo ndipo lilipotokea dhahama ya Suarez na Evra.
United wameshinda mechi zao 3 za mwisho dhidi ya Liverpool katika uwanja wao, na saba kati ya nane ya mwisho.
Je Dalglish atakubali kuendelea kuwa mteja wa United pale Old Trafford au Fergie ataendeleza uababe wake akiwa Theatre of Dreams?





LUIS SUAREZ VS OLD TRAFFORD
Acha tuseme tu, Suarez anakwenda kukutana na matusi yote yaliyomo katika kila kinywa cha mashabiki zaidi ya 70,000 at Old Trafford.
Haijalishi maneno yoyote watakayoambiwa mashabiki na kocha yoyote wa timu hizo mbili, au hata kama Suarez au Evra watayamaliza kwa kupeana mikono, Muruguay huyo atapata mapokezi mabaya mno tangu aanze kwenda Old Trafford.
Itakuwa ni hali ya ambayo ni vigumu kwa mwanadamu mwenye hisia kuivumilia, lakini yote itategemeana na jinsi Suarez atakavyo react katika dk 90 za mchezo.

Friday, February 10, 2012

Kaseja: Tutawafuta machozi kwa Azam

NAHODHA wa Simba, Juma Kaseja, amesema wachezaji watawafuta machozi washabiki kwenye mechi dhidi ya Azam Jumapili ijayo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Kaseja alisema wachezaji wa Simba wanajua maumivu waliyonayo washabiki mara baada ya kupoteza mechi dhidi ya Villa Squad na ndiyo maana wanataka kurekebisha mambo.
Jumamosi iliyopita, Simba ilifungwa na Villa bao 1-0 katika pambano lililofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini, matokeo ambayo yaliwauma washabiki wengi ikizingatiwa kuwa timu hiyo ndiyo inayoshika mkia kwenye ligi.
“Soka ni mchezo wa ajabu sana. Kuna kipindi kunakuwa na matokeo ambayo hakuna anayeyategemea. Ila mimi ni muumini wa dini na ninaamini kuwa kuna wakati Mungu naye anakuwa na mipango yake. Alipangalo Mungu haliepukiki,” alisema.
Hata hivyo, Kaseja alisema ana imani washabiki watasahau kuhusu mchezo wa Villa iwapo Simba itaibuka mshindi katika pambano gumu dhidi ya Azam Jumapili ijayo.
Alisema ndiyo maana sasa wachezaji wote wa Simba wameleekeza nguvu zao zote katika pambano hilo wakifahamu fika kuwa matokeo ya mchezo huo yakiwa mazuri, Simba itatulia.

Owino amaliza ngwe ya kwanza ya mazoezi, sasa kuanza mazoezi ya kucheza mpira na Academy

Hali ya mchezaji Joseph Owino wa Azam FC inaendelea vizuri kwa kufikisha asilimia 70 ya  mazoezi ya viungo kujiweka sawa kabla ya kuanza mazoezi na timu ya wakubwa kamili kucheza mechi za ligi miezi miwili ijayo.
Owino alijiunga na Azam msimu huu akisumbuliwa na jereha la mguu wa kushoto, baada ya matibabu yupo katika mazoezi maalum ya viungo ili kurejesha mguu huo katika hali ya kawaida.
Akizungumza na www.azamfc.co.tz mwalimu wa viungo toka Ujerumani Paul Gomez amesema Owino hali yake inaendelea vizuri kadilii muda unavyokwenda amebakisha asilimia 30 kufikisha 100 ili kuwa kamili kwa kucheza mpira.
"Kutokana na tatizo lake anapata mazoezi ya viungo kwanza yatakayoufanya mguu wake urudi kama zamani na kuweza kuhimili kucheza na kukimbia bila kufanya hivyo mguu utamletea matatizo zaidi" Alisema Gomez.
Aliongeza kuwa baada ya kumaliza mazoezi ya viungo atajiunga na timu ndogo ya Azam Academy muda wowotekuanzia sasa kufanya mazoezi mepesi ya mpira wa miguu, endapo ataonekana kufanya vizuri atajiunga na timu kubwa na kuanza kucheza. kwa kuwa hatutaki kumharakisha tunatarajia itachukua miezi miwili lakini kama tungetaka kumharakisha tungeweza mtumia alisema Gomes.
Gomez alisema atafanya mazoezi na timu ndogo kwa muda ili kujenga uwezo wa kucheza na baadaye kurudi katika timu kwa ajili ya mechi za ligi kuu.
Owino alisajiliwa na Azam FC mwezi September mwaka jana, kabla ya kujiunga alikuwa mchezaji wa Simba SC.

Source: www.azamfc.co.tz

PATRICK VIEIRA: WAAMUZI HAWATAKI CITY TUCHUKUE UBINGWA WA ENGLAND




Patrick Vieira amewabwatukia marefa wa premier league na kusema kwamba wana agenda ya siri ya kuhakikisha Manchester City hawachukui ubingwa wa English premier league.
Vieira, ambaye ni mkurugenzi wa kitengo cha ukuzaji vipaji cha Manchester City, anaamini vijana wa Roberto Mancini wamekuwa wakitendewa visivyo na marefa katika siku za hivi karibuni.

City walimpoteza nahodha wao Vincent Kompany na mshambuliaji Mario Balotelli waliofungiwa kwa mechi 4 kila mmoja huku wakiwa wapo mbele kwa pointi 2 mahasimu wao Manchester United.


Kompany alitolewa nje kwa kufanya tackle ya miguu miwili dhidi ya Nani wakati wa mechi ya kombe la FA dhidi ya Manchester United lakini Vieira aliitolewa mfano tackling ya ya Frank Lampard dhidi ya Adam Hammill wa Wolves na mwisho wa siku star huyo wa Chelsea alipata kadi ya njano tu.

Balotelli aliadhibiwa baada ya kumkanyaga kwa makusudi kiungo wa Spurs Scott Parker  na pia hapo tena Vieira amesema Peter Crouch alifanya hivyo kwa mchezaji Jonas Olssson lakini hakuadhibiwa.


‘Sipendi kufikiria kuhusu jambo hili kwa sababu sitaki kusema kila mtu haipendi City au jambo lolote la namna hiyo.

‘Lakini unapoangaliwa katika maamuzi ya hivi karibuni, unajiuliza mwenyewe kama kuna tatizo lolote dhidi yetu, au hawataki City tuchukue ubingwa. Vieira aliongeza” “Tackle ya Lampard ilikuwa inaonekana hatari mno ukilinganisha nay a Vincent, au namna Peter Crouch alipomuingiza vidole machoni mpinzani wake, ilikuwa hatari zaidi.

“Tunajitahidi kufanya vizuri tushinde kombe, tunakuabli adhabu zetu, lakini unapoangalia matukio yanayolingana yanapotolewa maamuzi tofauti, unahisi kuonewa na inaudhi sana hali hiyo.”

JOHN TERRY AONDOKA UINGEREZA - AENDA ZAKE URENO KUPUNGUZA STRESS.


Baada ya kuandamwa na mikosi nahodha aliyevuliwa kitambaa John Terry ameamua kuondoka England na kwenda nje ya nchi kwa mapumziko mafupi.

Mlinzi huyo wa Chelsea amepewa ruhusa ya wiki moja na Andre Villas-Boas na imefahamika ameelekea nchini Ureno na familia yake kwa ajili kupumzisha akili yake baada ya kuandamwa na msongo wa mawazo tangu avuliwe unahodha wiki iliyopita.

Terry ambaye pia ni majeruhi wa goti ataukosa mchezo wa jumamosi dhidi ya Everton.

DAGLISH: FA KAMA WANATAKA KOCHA MUINGEREZA WAMCHUKUE ALEX FERGUSON



Manager wa Liverpool Kenny Dalglish ametoa ishara kwamba anadhani mpinzani wake mkubwa kocha wa mahasimu wake Manchester United, Sir Alex Ferguson, inabidi awe kocha wa England.
Baada ya kuondoka kwa Fabio Capello wiki hii, kocha wa Tottenham Harry Redknapp amekuwa akitajwa kama mtu sahihi kumrithi mtaliano Capello.

Lakini Dalglish, ambaye timu yake inaenda Old Trafford kesho, anafikiri kama chama cha soka na waingereza wanataka mzaliwa wa nchi hiyo amrithi Capello basi inabidi wamchague mwenye rekodi bora zaidi.

“Mimi hainisumbui sana hili suala la kocha ajaye wa England, ni wazi kabisa waskotishi ndio makocha wenye asili ya Uingereza wanaofanya vizuri zaidi kama makocha.”
“England wapo katika kutafuta kocha mwingine, na kama wanataka kocha mzaliwa wa Uingereza inabidi wamchukue kocha mwenye rekodi nzuri kuliko wote katika Premier League.

Dalglish aliweka wazi hakuwa anamzungumzia Harry Redknapp lakini akasema kama Redknapp atapewa jukumu hilo itakuwa vizuri.
Alipoulizwa kama alipokuwa akizungumzia kocha mwenye rekodi nzuri katika premier league alikuwa anamaanisha Sir Alex Ferguson, Dalglish alicheka na kusema “Jamani sijataja jina la mtu.”

GIGGS ASAINI MKATABA MPYA UNITED



Ryan Giggs amesaini mkataba wa mwaka mmoja zaidi kuendelea kuichezea Manchester United.
Giggs, 38, ambaye alianza kuichezea United in 1990, na aliichezea mechi yake ya kwanza in March 1991.
Kutoka kipindi hicho mpaka leo ameshaichezea timu hiyo mechi 898 na akifunga magoli 162.
Ameshinda makombe 12 ya EPL, manne ya FA Cup, matatu ya Carling Cup, moja la Super cup, pia ameshinda kombe la mabara na kombe la dunia la vilabu.

HABARI KATIKA PICHA!



                          HAYA KINA DADA MPOOO....STYLE HIYO MNAIONA ? JE MMEIPENDA ?
                        DE SANCTIS GOLIKIPA WA NAPOLI
EMANUEL EBOUE AKIWA AMEMMEBA GOSSO GOSSO MARA TU BAADA YA IVORY COAST KUINGIA KWENYE FAINALI.
            HARPER AKIWA NA MAMA YAKE VICTORIA ADAMS
                                    NEYMER STYLE

TAARIFA KUTOKA TFF

LIGI KUU YA VODACOM 2011/2012

Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inaingia raundi ya 17 kesho (Februari 11 mwaka huu) kwa mechi tano huku ile ya Kagera Sugar na Mtibwa Sugar iliyokuwa ichezwe Februari 12 mwaka huu ikilazimika kusogezwa mbele kwa siku moja. Mechi za kesho (Februari 11 mwaka huu) ambazo zitaanza saa 10 kamili jioni ni kati ya Simba na Azam (Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam), Toto Africans na Moro United (Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza), Polisi Dodoma na Villa Squad (Uwanja wa Jamhuri, Dodoma), Coastal Union na African Lyon (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga) na JKT Oljoro na JKT Ruvu (Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha). Kagera Sugar na Mtibwa Sugar sasa zitacheza Februari 13 mwaka huu kwa vile Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba siku ya Februari 12 mwaka huu umetolewa kwa shughuli za kijamii. Mabadiliko hayo pia yamesababisha mechi kati ya Toto Africans na Mtibwa Sugar iliyokuwa ichezwe Februari 15 mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba sasa kuchezwa Februari 16 mwaka huu. Nayo mechi namba 119 kati ya Yanga na Ruvu Shooting iliyokuwa ichezwe Februari 12 mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam- Chamazi, sasa itafanyika siku hiyo hiyo kwenye Uwanja wa Taifa. Mechi hiyo imehamishiwa Uwanja wa Taifa kutokana na maombi ya Yanga kwa vile itakuwa ni sehemu ya sherehe za maadhimisho ya miaka 77 tangu kuasisiwa kwa klabu hiyo.

MGAMBO, MORANI KUCHEZA FEB 12

Mechi ya Kundi A ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kati ya Mgambo Shooting ya Tanga na Morani ya Manyara iliyokuwa ichezwe Februari 11 mwaka huu kama ilivyokuwa ile ya Kundi C kati ya AFC ya Arusha na Polisi ya Morogoro zimesogezwa mbele kwa siku moja.Mabadiliko hayo yametokana na mechi hizo kuingiliana na za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) zinazochezwa kwenye viwanja vya Mkwakwani, Tanga na Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha. Mechi nyingine za FDL zitaendelea kesho (Februari 11 mwaka huu) kama ratiba inavyoonesha. Kundi A, Burkina Faso itakuwa mwenyeji wa Polisi Dar Salaam kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro wakati Temeke United na Transit Camp zitaoneshana kazi Uwanja wa Mabatini mjini Mlandizi. Kundi B litashuhudia mechi kati ya Mbeya City na Majimaji kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya huku JKT Mlale wakiwa wenyeji wa Small Kids kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea. Nayo Tanzania Prisons itakuwa mgeni wa Polisi Iringa kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Samora. Mechi ya Kundi C itakuwa moja ambapo Rhino FC itakaikaribisha 94 KJ ya Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.

 KOZI YA MAKOCHA NGAZI PEVU YAAHIRISHWA

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeahirisha kozi ya ukocha ngazi pevu (Advanced Level) iliyokuwa ifanyike jijini Dar es Salaam kuanzia Februari 12- 25 mwaka huu. Kozi hiyo imeahirishwa kwa vile wengi wa makocha walioomba hawakufikia vigezo vilivyowekwa. Vigezo vya msingi vilikuwa mwombaji awe na cheti cha ukocha ngazi ya kati (Intermediate Level), wawe wanafanya kazi hiyo ya ukocha (active) na kuwasilisha cheti cha elimu ya sekondari (kidato cha nne). Mwisho wa kuwasilisha maombi kwa ajili ya kozi hiyo ilikuwa Februari 5 mwaka huu. Makocha 34 waliwasilisha maombi kwa ajili ya kushiriki kozi hiyo, lakini waliokidhi vigezo ni 12 tu. Makocha waliokidhi vigezo kwa ajili ya kozi hiyo ni Sospeter Vedasto kutoka mkoani Pwani, Beatus Manga (Temeke), Renatus Shija (Pwani), Ntungwe Selemani (Pwani), William Mamiro (Kinondoni), Ngawina Ramadhan (Temeke), Khatib Mtoo (Temeke), Hamisi Chimgege (Temeke), Selemani Mkumya (Temeke), Idd Cheche (Azam), Mohamed Mayosa (Temeke) na Imam Mbarouk (Shinyanga). Wawezeshaji wa kozi hiyo ambayo sasa tarehe yake ya kufanyika itatangazwa baadaye ni Mkufunzi wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Jan Poulsen, Mkufunzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Sunday Kayuni na Mkufunzi wa Chama cha Mpira wa Miguu cha Denmark (DBU), Kim Poulsen. 

KIPRE BOLOU WILFRIED RUKSA AZAM

Mshambuliaji Kipre Bolou Wilfried aliyejiunga na Azam kutoka Ivory Coast sasa ni ruksa kuichezea timu hiyo michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inayoendelea kwenye viwanja mbalimbali nchini. Shirikisho la Mpira wa Miguu la Ivory Coast (FIF) jana (Februari 9 mwaka huu) limetoa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa mchezaji huyo aliyeombewa uhamisho katika dirisha dogo la usajili kutoka timu ya Sewe Sport ya nchini humo.

YANGA, MTIBWA SUGAR ZAINGIZA MIL 49/-

Pambano la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Yanga na Mtibwa Sugar lililochezwa Februari 8 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh. 49,510,000. Jumla ya watazamaji 14,604 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo namba 112 kwa kiingilio cha sh. 3,000, sh. 5,000, sh. 10,000 na sh. 15,000 kwa VIP A. Baada ya kuondoa gharama za awali za mchezo na asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ni sh. 7,552,372.88 kila timu ilipata sh. 8,933,048.14, uwanja sh. 2,977,682.71.  Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,191,073.08, TFF sh. 2,977,682.71, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 1,488,841.36, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 297,768.27 na asilimia 10 ya gharama za mechi ni 2,977,682.71. Gharama za awali za mechi zilikuwa nauli ya ndani kwa waamuzi sh. 10,000, nauli ya ndani kwa kamishna wa mchezo sh. 10,000. Posho ya kujikimu kwa kamishna na waamuzi sh. 160,000, mwamuzi wa akiba sh. 30,000, tiketi sh. 4,000,000, maandalizi ya uwanja (pitch) sh. 400,000, umeme sh. 300,000, usafi na ulinzi kwa uwanja sh. 2,350,000 na Wachina (Beijing Construction) sh. 2,000,000.  Gharama nyingine ni Jichangie ambayo ni sh. 200 kwa kila tiketi; kila klabu ilipata sh. 1,022,280 wakati Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) kilipata sh. 876,280. 

MECHI ZA YANGA, SIMBA CAF

Klabu za Zamalek ya Misri na Kiyovu Sport zimekataa maombi ya mechi zao za marudiano za Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho dhidi ya Yanga na Simba kusogezwa mbele kwa wiki moja kutoka wikiendi ya Machi 2, 3 na 4 mwaka huu. Baada ya mazungumzo na klabu za Simba na Yanga, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) lilituma maombi Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kuomba mechi hizo zisogezwe ili wachezaji wapate fursa ya kutosha kuzitumikia klabu zao na timu ya Taifa (Taifa Stars). Februari 29 mwaka huu Taifa Stars itacheza mechi ya mchujo ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa ajili ya fainali za mwakani nchini Afrika Kusini dhidi ya Msumbiji kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Wikiendi ya Machi 2, 3 na 4 mwaka huu Yanga itakuwa inarudiana na Zamalek ugenini wakati Simba itarudiana na Kiyovu Sport jijini Dar es Salaam. CAF ilikuwa tayari kuridhia maombi hayo iwapo Chama cha Mpira wa Miguu cha Misri (EFA) na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Rwanda (FERWAFA) wangekubali. Lakini EFA na FERWAFA wamekataa ombi hilo kwa vile litavuruga ratiba ya mechi za ligi katika nchi hizo

Boniface Wambura

Ofisa HabariShirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

VILLA SQUAD YAALIKWA BUNGENI BAADA YA KUIFUNGA SIMBA BAO 1:0

Klabu ya Villa Squad imealikwa bungeni kutokana na ushindi walioupata hivi karibuni dhidi ya Simba kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom.

UJANJA UJANJA KWENYE SOKA MPAKA LINI?

Na Magesa Japhari
HABARI zenu ndugu wasomaji wangu popote pale mlipo nje na ndani ya Tanzania.
Mara nyingi nimekuwa nikifuatilia na kujiuliza; hivi ni kwa nini Soka letu hapa Tanzania linakuwa na hatua za mlevi, yaani mbele nne na kurudi nyuma nane na kisha viongozi wetu kuanza kujitapa eti wamefanya kazi kubwa.

Lakini kwangu mimi sioni hatua tuliyopiga zaidi ya kuona ujanja ujanja unaofanyika katika Soka letu. Ukiangalia kwa makini utaona ninachozungumzia kwani tukianza na vilabu vyetu vinavyoshiriki mashindano mbali mbali utaona jinsi gani vinavyoandaliwa.

Vilabu vinaandaliwa bila hata mechi za majaribio na katika mazingira magumu, lakini viongozi wa vilabu hivyo wakihojiwa utasikia timu iko vizuri na inaendelea na kambi vizuri lakini mwisho wa siku katika mashindano yenyewe wanaangukia pua na majibu yao hubadilika gafla; oh! timu haikuwa na maandalzi mazuri isitoshe hatukucheza mechi hata moja ya majaribio.

Sasa wakati unatwambia kambi ya timu ni nzuri na timu iko katika hali nzuri ulikuwa na maana gani. Nadhani wakati umefika tuambiane ukweli kama kocha wa riadha anavyoweka mambo hadharani na wala si kupakana mafuta kwa mgongo wa chupa.

Tukirudi katika timu zetu za taifa ndio kichekesho kabisa; ulishaona timu inajiandaa kucheza mashindano ya kimataifa eti inajaribiwa na timu ya Vijana ya Azam. Mara inacheza na Vijana wa TSA, sasa tujiulize kama hawa vijana wa Azam wana uwezo wa kuipima Timu ya Taifa, kwa nini wasichukuliwe wao na wakaenda kuwakilisha taifa badala yao.

Kwa viongozi wetu wa vilabu, sasa naona imekuwa vurugu kwani wanafikiri kuonekana katika luninga wakisema jambo ndio wataonekana wanafanya kazi, matokeo yake wamesahau kuwa kila mmoja katika klabu ana mamlaka yake na kazi yake inabidi aifanye. Sasa wewe mwenyekiti, wewe msemaji wa klabu, wewe katibu wa klabu, sasa wenzio watafanya kazi gani au unataka wote waishie kujiuzulu au kuomba kuacha kazi?

Kiongozi badala ya kufanya mikakati ya kuendeleza klabu unaanza kuzunguka kutafuta vyombo vya habari ili tu uonekane. Mimi nina wasiwasi na viongozi kama hawa. Inawezekana kabisa hawapo kwa ajili ya kuongoza Soka letu bali kwa maslahi yao binafsi, maana haiwezekani ukataka kuonekana kila mara katika vyombo vya habari kama ndilo lengo. Viongozi kama hawa nadhani hawatufai katika Soka letu maana wanatufanya tuzidi kurudi nyuma katika soka.

Tukiangalia katika uongozi wa TFF ni madudu mengi yanayofanyika na wamekuwa wakiongoza pia kwa ujanja ujanja mwingi na kupelekea timu zetu za Taifa kuwa vichekesho katika mashindano ya kimataifa. Mfano mzuri ni pale timu ya Taifa iliposhinda Kombe la Tusker na baadaye kualikwa katika mashindano huko Misri. Matokeo yake naamini kila mtu anayajua na sina haja ya kusema. Je ni lini tumewahi kuzipeleka timu za vijana katika mashindano yoyote ambayo tumealikwa?

Na ni lini tumewahi kuandaa kikosi cha vijana kikadumu na hatimaye kuwa timu ya taifa ya wakubwa? Mimi naamini kama tungekuwa na utamaduni wa kuwatunza vijana wenye vipaji tulionao tungefika mbali. Mfano mzuri ni wale vijana walioshinda Kombe la Kopa CocaCola kule Brazil, je kuna mtu yeyote anajua walipo na wana hali gani?
Ukipata jibu basi ndio utajua nini nazungumzia kwani kwa jinsi ninavyoona ujanja ujanja unatawala sana Soka letu.

 Kama bado hujaamini, basi naomba uangalie jinsi timu zinazopanda daraja zinacheza mechi ngapi. Mpaka kupata zile timu zinazopanda daraja ndipo utagundua kuwa tunacheza makida kwa sababu wachezaji hawapati kucheza mechi za kutosha ambazo zitawaweka fiti kwa ajili ya mashindano ya kimataifa; na ndiyo maana utaona tukienda katika mashindano mbalimbali ya kimataifa tunanusa tu na kuondolewa mapema kabisa. Mfano mzuri ni wakati Simba ilipopata ubingwa bila ya kupoteza hata mechi moja, lakini katika mashindano ya kilabu bingwa Afrika wakatolewa mapema kabisa.


Je, wale wanaosema kwamba vilabu vya Simba na Yanga vinanunua mechi si wakweli? Maana kama wangekuwa mabinwa wa kweli basi tungekuwa tunaona ubora wao na si siasa za viongozi wao ambao wanazuga katika Soka; na lengo lao likiwa kupata umaarufu na kisha kukimbilia kugombea ubunge.

Nadhani, sasa wakati umefika wa kuweka siasa pembeni na kuamua kufanya kazi ya Soka na kuachana na ujanja ujanja unaofanyika kwa kuweka timu kambini kwa muda wa siku mbili bila hata ya majaribio na kisha kutaka ushindi; na eti tunasimama na kuwataka Watanzania wajitokeze kuwapa sapoti. Karne hii si ya ujanja ujanja kama tunavyofanya, kama kweli tuko tayari basi na tuwekeze katika vijana wadogo na si mbwembwe kama zile za TFF na kisha kufunga kituo cha TSA eti kisa magodoro na baadhi ya vifaa vimekwisha, sasa huo kama sio ubabaishaji ni nini?

Hebu tujipange na tuache huu ujanja ujanja wetu wa kuandaa timu zetu kama mapulizo ya kupamba kwenye harusi na badala yake tufuatilie program tunazopewa na walimu wa timu zetu na kuzifanyia kazi.

E- mail: magesajaph@yahoo.co.uk
Simu: 0784269812/0755826102/0714368843

ERIC ODHIAMBO: MTANZANIA PEKEE KUCHEZA LIGI KUU SCOTLAND





MSHAMBULIAJI  chipikuzi mwenye asili ya Tanzania, Eric Geno Sije Odhiambo, anaweza kuwa na mchango mkubwa kwa timu yake ya Inversness Caledonian Thistle ya Scotland. Eric ambaye alijiunga na timu hiyo iliyomaliza katika nafasi ya saba katika ligi kuu ya Scotland mwaka 2009, amekwishacheza michezo 55 na ameifungia mabao 7. Hiyo imempelekea kuwa mchezaji kipenzi cha kocha wake Muingereza Terry Butcher.


Kijana huyu aliyezaliwa katika jiji la Oxford huko England, ni mwenyeji wa Mkoa wa Mara kiasili; na miaka michache iliyopita alikuja nchini kumzika baba yake Mzee Sije Odhiamo pamoja na nduguze ambao pia ni wanasoka wa kulipwa nchini England.






Eric ametokea kuwa mshambuliaji wa kutegemewa wa Inversness Thistle baada ya kupata 'msoto' katika vilabu vya Leicester City ambako ndiko alipoanzia katika academy yao. Alikuwa katika kikosi cha Leicester City kuanzia mwaka 2006-2009 lakini alikuwa akipelekwa kwa mkopo katika timu za Southend United ambako alicheza mechi 5 na hakufunga bao lolote. Hiyo ilikuwa mwaka 2007. Mwaka 2008 alipelekwa kwa mkopo katika timu ya Dundee United inayocheza ligi kuu ya Scotland na alicheza mechi nne tu, kabla ya mwaka huo huo kupekwa kwa mkopo Brentford.


Timu ya Inversness Thistle, imeanzishwa mwaka 1994 miaka minne baada ya Eric kuzaliwa. Eric huvaa jezi namba saba katika kikosi cha timu hiyo na ametokea kuwavutia wengi kutokana na kipaji chake cha kufunga mabao.

Kwasasa Eric amejiunga na klabu ya Denizlispor inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini Uturuki.

CHEMSHA BONGO! TAJA WALAU MAJINA YA WACHEZAJI 3 KUTOKA KWENYE PICHA HII.

MSAADA TUTANI: HAWA WACHEZAJI NI AKINA NANI?

HINT: WANACHEZA TIMU MOJA YA TAIFA.

ZAMALEK WAMEKATAA KUCHEZA MECHI MOJA YA YANGA.


Klabu ya Zamalek kupitia meneja msaidizi wa Klabu ya hiyo, Ismail Youssef amesema Zamalek imetupilia mbali maombi ya Yanga ya kutaka mechi kati yao ya Ligi ya Mabingwa kuchezwa moja.Yanga imekuwa ikihofia usalama wake kwenye mchezo wa marudiano uliopangwa kufanyika Cairo kutokana na tukio la vurugu za mashabiki nchini Misri zilizosababisha watu 74 kupoteza maisha jijini Port-Said.

“Yanga imeomba kucheza na sisi mchezo moja kwa sababu ya kuhofia usalama wao Cairo, lakini kanuni za CAF zinatutaka Zamalek kuthibitisha kwanza hilo,” alisema Youssef.

Alisema, "tumekataa pendekezo lao hilo na hatutakubali kunyimwa haki yetu ya kucheza nyumbani kama timu nyingine kwenye mashindano haya."CAF ndio watakaoamua kwamba mechi yetu ya nyumbani tutacheza hapa Cairo au uwanja mwingine kama wakiona hapa Cairo hapafai,"alisema Youssef.

Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Yanga,  Selestine Mwesigwa alisema yeye hana tatizo na mtazamo huo wa Zamalek kwa kuwa wao wanasubiri kauli ya CAF.

"Sisi tunasubiri kauli ya CAF, hatuwezi kuzungumza lolote kutokana na madai ya Zamalek," alisema Mwesigwa.

Tayari Shirikisho la Soka la Sudan limeonyesha nia ya kutaka kuwa mwenyeji wa mechi hiyo kwa kutuma maombi yao kwa CAF.Timu hizo zitakutana Februari 19 jijini Dar Es Salaam na zitarudiana wiki mbili baadaye huko Cairo. 

Wakati huohuo; Kocha wa Zamalek, Hassan Shehata amesisitiza kuwa ataendelea kubaki na timu hiyo na kukanusha madai kuwa alikuwa na mpango wa kwenda kujiunga na Ittihad Jeddah.

EXCLUSIVE: XHERDAN SHAQIRI AZITOSA UNITED NA LIVERPOOL AHAMIA BAYERN MUNICH


Shqiri anakumbukwa kwa alichowafanya Man United wakati wa mechi ya mwisho ya makundi ya UCL msimu huu.


Bayern Munich wamekamilisha usajili wa kiungo wa FC Basle Xherdan Shaqiri, ambaye alikuwa akiwindwa na Liverpool na Manchester United.

Kiungo huyo mwenye miaka 20 kutoka Uswiss alifaulu vipimo vya afya mjini Munich wiki hii.

The Bavarian wametangaza kwamba makubaliano rasmi yameshafikiwa na Basle na mchezaji mwenyewe, ambaye amesaini mkataba wa miaka 4, na atajiunga Bayern mwanzoni mwa msimu ujao.

“Tuna furaha sana kutangaza kwamba tumefanikiwa kumsaini Xherdan Shaqiri, moja ya wachezaji bora chipukizi barani ulaya.” Alisema mkurugenzi wa ufundi wa timu hiyo Christian Nerlinger.

Kocha wa Bayern Jupp Heynckes anaagalia mbele kuja kufanya kazi na kinda hilo msimu ujao “Shaqiri atakiimarisha kikosi chetu msimu ujao kwa uwezo wake mkubwa alionao. Nimekuwa nikimtazama kwa muda mrefu sasa na nimekubali anaweza kuwa mchezaji muhimu katika timu yetu.”

Shaqiri atapambana na Bayern Munich wiki mbili zijazo akiwa na timu yake ya sasa FC Basle katika hatua ya 16 ya Champions league.
Ada ya uhamisho ya Shaqiri haijatajwa lakini inaaminika ipo karibu na euro million 10.