Search This Blog

Saturday, January 4, 2014

LUIS SUAREZ NDIYE MWANASOKA ANAYEONGOZA KWA UBORA MPAKA SASA DUNIANI.


TAKWIMU MBALI MBALI KWA MWAKA 2013 ZA LIGI 5 BORA ULAYA.



THE 11 –PROGRAMU YA KUZUIA AU KUEPUSHA MAJERAHA MICHEZONI/SOKA



 Pengine Umewahi kusikia mtu ambaye amewahi kuumia . Mchezo wa soka ni mchezo ambao una hatari ya kumletea majeraha mtu anayecheza. Lakini habari njema ni kwamba utafiti wa kisayansi umeonyesha kuwa matukio ya kuumia katika soka kunaweza kupunguzwa kwa progammu maalum za kuzuia majeraha kwa wachezaji.
11 ni proggramu rahisi na yenye kutumia muda mfupi ya kumuepusha au kumkinga mchezaji na majeraha ambayo inajumuisha mazoezi kumi ambayo yana ushahidi unaoonyesha jinsi inavyofanya kazi. 

11 ni progranu inayolenga kuongeza uungwana yaani FAIR PLAY latika mchezo na haihitaji kitu kingine cha ziada zaidi ya mpira na inafanywa kwa muda usiopungua dakika 10 mpaka 15 . Programu hii ni ya uhakika kuliko mazoezi mengi ambayo wachezaji huyatumia na inaweza kutumika katika nafasi ya mazoezi mengine.

Mazoezi yaliyopo katika programu hii yamejikita kwenye mbinu maalum za ambazo makocha wanapaswa kujifunza na kuzizoea ili waweze kuwapa wachezaji ili waweze kujenga misuli hasa ya mapaja pamoja na kumudu mnyumbuliko wa misuli kuendana na kasi ya mchezo. 

Moja ya mazoezi haya ni jinsi ya kujenga misuli kunyooka na kuwa thabiti.
Kanuni na programu hii ya 11 inatakiwa kufanywa kila siku katika wakati wa mazoezi ya wachezaji hasa baada ya kupasha mwili moto na kunyoosha misuli . Ili kuhakilisha uhakika wa mazoezi haya yanatakiwa kufanywa kama inavyotakiwa bila kukosea na kabla ya mechi unapaswa kuyafanya mazoezi haya kwa ufupi ili misuli isikakamae.

Programu hii ilianzishwa na kuendelezwa na FIFA katika idara yake ya afya na utafiti kwa ushirikiano na kundi la wataalamu wa kimataifa wa masuala ya afya michezoni . Baada ya kufuata programmu hii mchezaji ataongeza kiwango chake cha kuperform na kupunguza uwezekano wa kupata majeraha .

Friday, January 3, 2014

WAAMUZI 11 WAPATA BEJI ZA FIFA

 ISRAEL NKONGO,Mmmoja wa waamuzi waliopata beji ya FIFA.


Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limewapatia beji waamuzi kumi wa Tanzania kwa mwaka 2014.

Waamuzi wa kati waliopata beji hiyo ni Ramadhan Ibada, Oden Mbaga, Israel Mujuni na Waziri Sheha.

Waamuzi wasaidizi ni Josephat Bulali, Ferdinand Chacha, Hamis Changwalu, John Kanyenye, Ali Kinduli, Erasmo Jesse na Samuel Mpenzu.

WATATU WAOMBEWA ITC SHELISHELI


Shirikisho la Mpira wa Miguu la Shelisheli (SFF) limetuma Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) maombi ya Hati ya Uhamisho ya Kimataifa (ITC) kwa wachezaji watatu wa Tanzania.

Wachezaji walioombewa hati hiyo ili wakajiunge na timu ya La Passe FC inayocheza Ligi Kuu nchini humo ni Salum Kinje aliyekuwa akiichezea timu ya Simba, Semmy Kessy aliyekuwa Lipuli ya Iringa na Rashid Gumbo aliyekuwa timu ya Mtibwa Sugar.

TFF inafanyia kazi maombi hayo na mara taratibu zitakapokamilika hati hizo zitatolewa.
SALIM KINJE....
RASHID GUMBO

KATA MTI PANDA MTI, TOM OLABA ASAINI MKATABA WA MIEZI 6 KUMRITHI MKWASA RUVU SHOOTING!!



Na Baraka Mpenja, Dar es salaam

MAAFANDE wa jeshi la kujenga Taifa wa mkoani Pwani, Ruvu Shooting, wamemsainisha mkataba wa miezi sita kocha, Tom  Alex Olaba ili kurithi mikoba ya kocha aliyetimkia Yanga, Charles Boniface Mkwasa `Masta`.

Afisa habari wa klabu hiyo, Masau Bwire amesema Olaba ameshafika Mabatini jioni ya leo na kila kitu kimemalizika baina ya pande mbili.

“Tunafurahi kutangaza kuwa tumempata mrithi wa Mkwasa. Olaba ni mwalimu mzuri na tuna uhakika atatuongoza vizuri mzunguko wa pili”. Alisema Masau.

Olaba ambaye amewahi kuifundisha Mtibwa Sugar ataanza kazi rasmi kesho kukinoa kikosi cha Ruvu Shooting kuelekea mzunguko wa pili wa ligi kuu soka Tanzania bara unaotarajia kuanza kutimu vumbi januari 25 mwaka huu.

Kwa upande wake Olaba alisema amefurahi kurudi ligi kuu Tanzania bara kwa mara nyingine, lakini hawezi kuzungumza lolote mpaka atakapoongea na wachezaji wake hapo kesho mazoezini.

“Nimechoka sana ndugu yangu, ujue nimetoka safarini. Hata hivyo kwasasa siwezi kuzungumza lolote mpakaa nikikutana na kuongea na wachezaji wangu. Kikubwa nimefurahi kurudi  katika changamoto ya ligi ya Tanzania”, Alisema Olaba.

YANGA YAANZA KUJIFUA

 

Mkwasa (mwenye rangi za Bluu) akiongoza mazoezi leo asubuhi katika uwanja wa Bora Mabatini Kijitonyama.




Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara timu ya Young Africans leo imeeanza kujifua katika viwanja vya bora Mabatini Kijitonyama kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu na mashindano ya kimataifa chini ya kocha msaidizi Charles Boniface Mkwasa.
Young Africans ilisimama kufanya mazoezi kwa siku takribani tatu kufuatia kufanya mabadiliko ya benchi la Ufundi na leo rasmi imeanza mazoezi asubuhi chini ya makocha wasaidzi Mkwasa na kocha wa makipa Juma Pondamali.

Mkwasa alitumia muda wa dakika 5 kuongea na wachezaji wote waliofika mazoezini siku ya leo, kuwaelekeza nini wanapaswa kufanya na kuzingatia mafunzo yake ambapo wachezaji waliweze kutekeleza kwa kiwango cha hali ya juu.

Kocha wa makipa Juma Pondamali aliwafua vilivyo magolikipa Juma Kaseja, Ally Mustafa "Barthez" na Deogratias Munish "Dida" na kusema huu ni mwanzo tu kwani anaamini wachezaji hao watakua katika kiwango kizuri kutokana na uwezo wanaouonyesha katika mazoezi anayaowapatia.

Kikosi cha Young Africans kesho kitaendelea na mazoezi asubuhi katika uwanja wa Mabatini Kijitonyama ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mzunguko wa pili na mashindano ya kimataifa.
Aidha washambuliaji Hamis Kiiza na Emmanuel Okwi waliokwenda kwao nchini Uganda kwa ajili ya matatizo ya kifamilia wanatarajiwa kurejea nchini mwishoni mwa wiki tayari kuungana na wenzao kujiandaa na mzunguko wa pili.

Source: youngafricans.co.tz

EZEKIEL KAMWAGA AELEZA SIRI YA KUIPENDA SIMBA SC.


HIGHLITES : AZAM FC ILIPOIFUNGA SPICE STARS MABAO 2 -0 KWENYE MICHUANO YA KOMBE LA MAPINDUZI.


Na Baraka Mpenja, Dar es salaam

MABINGWA watetezi mara mbili mfululizo wa kombe la Mapinduzi, Azam fc wameanza vyema michuano hiyo baada ya kuifunga Spice Stars mabao 2-0 katika mchezo wa Kundi C jioni ya leo Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Mabao ya Azam fc yamefungwa katika dakika ya 71 kupitia kwa Mshambuliaji Mganda, Brian Umony kufuatia kuwatoka mabeki wa Spice  na kupiga mpira uliomshinda mlinda mlango, Mohamed Silima.

Pasi ya bao hilo litoka kwa kiungo mahiri wa Azam fc Salum Abubakar ‘Sure Bo”.
Bao la pili lilifungwana na Himid dakika ya 86 kwa shuti kali, baada ya kuuwahi mpira uliokuwa unaelekea mikononi mwa kipa Silima kufuatia shuti la Salum Abubakar.

Afisa habari wa Azam fc ameuambia mtandao huu kuwa  mchezo ulikuwa mgumu sana kwani wapinzani wao wameonekana kuwa imara.

“Tumeanza vizuri kwa ushindi, lakini inaonekana michuano ya mwaka huu ni migumu sana. Spice wameonesha upinzani  mkubwa sana kwetu, lakini hatuwezi kusema lolote kwani ni mapema sana”. Alisema Jafar.

Jafar aliongeza kuwa kocha wao Mcameroon, Joseph Marius Omog anakisuka kikosi chao, hivyo makosa yanayotokea yatafanyiwa  marekebisho na kuhakikisha wanatwaa ubingwa wao.

Aidha, Jafar kwa niaba ya viongozi wa Azam fc amewapongeza vijana wao kwa kujituma na kupata ushindi ambao haukuwa rahisi kabisa.

Kwa ushindi huo, Azam inaongoza Kundi C kwa pointi zake tatu, na kubaki au kushuka itategemea na matokeo ya mchezo wa pili usiku wa leo  leo Uwanja wa Amaan kati ya Ashanti United ya Dar es Salaam na Tusker FC ya Kenya.

Kueleka katika mchezo huo, wauza mitumba wa Ilala wamesema wapo tayari kuwamaliza wakenya.

Marijani rajab, afisa habari wa Ashanti ameuambia mtandao huu kuwa kocha mkuu wa kikosi chao, Abdalaah Kibaden Mputa amewapanga vijana wake kutokana na uzoefu wake katika michuano mikubwa barani Afrika.

Katika mchezo mwingine wa Kundi A, Uwanja wa Gombani, Pemba, URA  ya Uganda imetoka sare ya 2-2 na Chuoni ya Zanzibar.

Mabao ya URA yamefungwa na Owen Kasuule dakika ya 44 na 57, wakati ya Chuoni yalifungwa na Shaaban Moke dakika ya 21 na Mwinyi Mngwali dakika ya 45 


Thursday, January 2, 2014

HATIMAE TOM HUDDLESTONE ATIMIZA AHADI YA KUZINYOA NYWELE ZAKE.

Kiungo wa Hull City Tom Huddlestone ametimiza ahadi yake ya kunyoa nywele zake iwapo angefunga bao baada kukaa miaka miwili na nusu bila kufunga,kiungo huyo aliifungia timu yake bao moja kwenye mchezo ambao timu yake iliifunga Fulham mabao 6-0.







MKWASA, PONDAMALI, KUINOA YANGA



 


Uongozi wa Young Africans SC umepata warithi wa nafasi tatu za benchi la ufundi (Charles Boniface Mkwasa, Juma Pondamali na Dr. Suphian Juma), huku wakiendelea na mchakato kumpata kocha mkuu ambaye atachukua nafasi ya mholanzi Ernie Brandts aliyesitishiwa mkataba wake mwishoni mwa mwaka 2013.

Charles Boniface Mkwasa "Master" aliyekua kocha mkuu wa timu ya Ruvu Shooting katika mzunguko wa kwanza anachukua nafasi ya aliyekua kocha msaidizi Fred Felix "Minziro" ambaye muda wake umemalizika mwishoni mwa mwaka 2013.
Mkwasa ambaye aliichezea Young Africans miaka ya 80's kwa kiwango cha hali juu pia alishawahi kuwa Kocha Mkuu/Msaidizi kwa kikosi cha Jangwani kwa vipindi tofauti jambo ambalo linamfanya aiwe mgeni katika mitaa ya Twiga na Jangwani.

Kocha wa makipa wa timu ya Taifa Tanzania "Taifa Stars" Juma Pondamali "Mensah" anachukua nafasi ya aliyekua kocha wa makipa mkenya Razaki Siwa ambaye pia alistishiwa mkataba wake mwishoni mwa mwaka 2013.

Pondamali golikipa aliyeichezea Yanga miaka ya 80's kwa kwa kiwango cha hali ya juu hata kufikia kuwa katika kikosi cha Tanzania kilichoshiriki mashindano ya Mataifa Afrika nchini Nigeria mwaka 1980, sio mgeni katika timu ya Young Africans kwani awali alishwahi kuwa kocha msaidizi kwa vipindi tofauti.
Dr Suphian Juma anachukua nafasi ya Dr Nassoro Matuzya ambaye pia alisitishiwa ajira yake mwishoni mwa mwaka 2013 pamoja benchi la Ufundi.

Mara baada ya kuwapata viongozi hao watatu wa Benchi la Ufundi kikosi cha Young Africans kesho kitaanza mazoezi jioni katika Uwanja wa Bora Kijitonyama kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom pamoja na mashindano ya Kimataifa huku kocha Mkwasa akiongoza benchi hilo la Ufundi mpaka atakapopatikana kocha mkuu ambaye watafanya watafanya kazi kwa pamoja.

Source: youngafricans.co.tz

JE KIPIGO CHA JANA CHA MAN UTD NI ISHARA TOSHA YA KUTOKUWA NA UBAVU WA KUTETEA UBINGWA WAO ?

Hapo jana Manchester Utd ilifungwa nyumbani mabao 2-1 na Totenham Hotspurs,kipigo ambacho kilikuwa ni cha pili mfululizo kwenye uwanja wake wa nyumbani toka kwa Spurs.
Kipigo cha jana kwa Man Utd kilikuwa cha kwanza kwa bingwa mtetezi tangia mwaka 1989 kupoteza mchezo siku ya mwaka mpya na pia ilikuwa mara ya kwanza tangu mwaka 1986 Manchester Utd kufungwa michezo minne kwenye uwanja wa Old Trafford kufikia siku ya mwaka mpya .
Siyo tu jana takwimu zilikuwa mbaya kwa  Man Utd tu pia ilikuwa ni mara ya kwanza kushuhudia timu zote zinazoshika nafasi nne za juu kuibuka na ushindi siku ya tarehe 1 january.
Baada ya kipigo cha jana,Man United sasa ipo nyuma kwa tofauti ya pointi 11 na vinara Arsenal na pointi 5 nyuma ya nafasi ya kufuzu Uefa Champions League.

Msimu mzima uliopita ambao Man Utd waliibuka mabingwa kwa kukusanya jumla ya pointi 89 walipoteza jumla ya pointi 25 tu,lakini mpaka kufika nusu ya msimu huu tayari wameshapoteza jumla ya pointi 26 hii inamaana wakishinda michezo yao yote iliyosalia watafikisha jumla ya pointi 88 tu.

Kibaya zaidi Manchester UTD haijawa na matokeo mazuri dhidi ya timu zilizo juu yake kwenye msimamo wa ligi kuu ya England, ukiangalia Msimamo uliotengenezwa kutokana na matokeo baina ya timu zinazoshika nafasi nane za juu utaona Manchester Utd inashika mkia ikimaanisha kutopata matokeo dhidi ya timu zinazoonekana kuwa bora msimu huu.

JE HII NI ISHARA TOSHA YA KWAMBA MAN UTD HAWANA UBAVU WA KUTETEA UBINGWA WAO ?

SOLSKJAER RASMI KOCHA MPYA WA CARDIFF CITY.

 Klabu ya Cardiff City imemtangaza rasmi mshambuliaji wa zamani wa Manchester Utd Ole Gunnar Solskjaer kuwa meneja wao mpya.
Solskjaer ambaye ni raia wa Norway hapo awali alikuwa kocha wa timu ya Molde aliyoiongoza kutwaa mataji mawili ya ligi kuu ya Norway.

MAKALA: AZAM FC WAONDOE KASORO HIZI WATWAE UBINGWA


Na Baraka Mbolembole

AZAM FC, kwa sasa ni moja ya timu mashuhuri katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati. Umaarufu wa timu hiyo hautokani na mafanikio ya soka katika michuano ya ukanda huu. Ni timu changa katika soka la Tanzania, haijawahi kutwaa ubingwa wa ligi kuu, ila katika misimu miwili ya mwisho wameweza kumaliza katika nafasi ya pili ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Na hadi wakati huu wa mapumziko kupisha michuano ya Challenge, Azam inashikilia nafasi ya pili katika ligi, nyuma ya Yanga SC kwa tofauti ya pointi moja.

WAPO KATIKA MWENDO MZURI KUELEKEA UBINGWA...
Ukitazama mafanikio yao ya kumaliza katika nafasi ya pili katika misimu ya 2011/ 12, na 2012/ 13, Azam ilikuwa katika mbio za ubingwa kwa misimu minne mfululizo ya mwisho. Katika msimu wa 2009/ 10 ambao timu ya Simba walitwaa ubingwa pasipo kupoteza mchezo wowote, Azam ilikuwa ni timu tishio katika ligi, walikuja kuangushwa kutoka nafasi ya kwanza hadi ya tatu mwishoni mwa msimu. Ni wakati huo kocha Itamor Amourin alikuwa amewekeza nguvu zake kwa wachezaji vijana, huku wakiongozwa na kundi la wachezaji bora wa ndani, na baadhi wa kigeni.

Ni wakati huo timu ilipokuwa imeanza uwekezaji wa uhakika wa kusajili wachezaji nyota kutoka ndani na nje ya nchi. Aggrey Morris, Ramadhani Chombo, Jabir Aziz, Mrisho Ngassa, Mwadini Ally, Kipre Tcheche, Ibrahim Shikanda, Kally Ongalla, marehemu Patrick Mafisango, Joseph Owino walitua hapo mara baada ya msimu kumalizika. Kocha, Itamor alikuja kuondolewa na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa mkurugenzi wa ufundi wa timu ya taifa ya Zanzibar, Stewart Hall. Kocha huyo alianza duu la pili la msimu wa 2010/ 11 kwa kutoa vichapo kwa timu mbalimbali ikiwemo mechi ya kukumbwa wakati walipoizamisha Simba kwa mabao 3-1, na kuonesha dalili za kutwaa taji.

Yanga waliokuwa taabani katika ligi walianza kunyanyuka taratibu kimchezo, Simba ikawa inashuka kutoka juu kwenda chini, huku Azam wakipanda hadi juu ya msimamo kwa tofauti ya pointi zaidi ya tatu kuelekea michezo minne ya mwisho. WAkaenda kucheza na Yanga katika mchezo ambao ulikuwa ni muhimu kwa kila timu, kwa Azam ilimaanisha kuwaondoa Yanga katika mbio za ubingwa, huku Yanga wakipigania kuingia katika nafasi ya pili. Azam ilipoteza mchezo huo kwa mabao mawili ya Jerry Tegete, akifuta lile la uongozi lililokuwa limefungwa na John Bocco. Siku chache baadae, kocha Hall alimtimua kipa Vladimir Niyonkuru kwa madai kuwa ' alitumika'. Azam ikashuka hadi nafasi ya tau mwishoni mwa msimu, Yanga waliokuwa watatu wakatwaa taji kwa stahili ya aina yake, baada ya kuwazidi bao moja timu ya Simba. ILikuwa ni nafasi ya Azam. Kwa nini walikosa, ni kupoteza mchezo dhidi ya Yanga, na mbuzi wa kafara akawa, Niyonkuru.

Katika kilichotajwa kama msimu mbaya wa ligi kuu katika miaka ya karibuni, ni upendeleo wa waamuzi kwa baadhi ya timu katika msimu wa 2011/ 12. Moja ya timu zilizokuwa zikilalamikiwa sana ni Azam, timu nyingi zilidai kuwa timu hiyo ilikuwa inabebwa na waamuzi, kitu ambacho hakikuwa na maana yoyote. Kwani ni msimu ambao Azam walikuwasanya pointi 12 kutoka kwa Simba na Yanga. Kwa nini hawakutwaa taji. Kama wangeshinda mchezo wao dhidi ya Mtibwa Sugar, Mei, 2012 katika uwanja wa Chamanzi walikuwa na nafasi ya kutwaa taji siku ya mwisho ya msimu. Said Bahanunzi wakati akiwa Mtibwa alifunga bao la kuongoza, likakataliwa na mwamuzi, baadae wakati akigombea mpira na mlinzi wa Azam akaoneshwa kadi nyekundu. Hadi dakika za mwisho matokeo yalikuwa 1-1, ambayo yalikuwa yanaipandisha Simba hadi kileleni na kwenda kuisubiri Yanga siku ya mwisho ya msimu.

Mwamuzi akatoa mkwaju wa penati wakati mlinzi Juma Abdul ( wakati yupo Mtibwa) alipozuia kiki kwa kifua na kusema kuwa aliushika mpira huo. Wachezaji wa Mtibwa waligomea penati hiyo na kupekea mwamuzi kuvunja pambano. Haki na kanuni zikapindishwa, mechi hiyo ikapigwa tena katika uwanja wa taifa siku mbili kabla ya kumalizika kwa ligi na Azam wakalala kwa bao 1-0 ambalo lilifungwa na Juma Abdul. Kwa nini walikosa ubingwa? Walifanya kazi kubwa sana kwa msimu mzima kuzima marudio ya kumaliza nafasi ya tatu kwa msimu wa tatu mfululizo. Hapa mchawi hakupatikana.

Kuanzia msimu huu timu hiyo imejihimarisha zaidi kiuchezaji na kiufundi. Ikiwa ni timu iliyocheza michezo mingi ya ugenini katika duru la kwanza, Azam wanakabiliwa na changamoto ya kuzishinda kwa wakati mmoja Simba na Yanga. Ni kazi sana, ila kuna mahali tayari wameonesha ubabe dhidi ya vigogo hao wa soka nchini. Katika uwekezaji Azam huwezi kuilinganisha na Simba na Yanga, wapo juu katika hilo. Je hiyo ndiyo inaweza kuwa sababu ya kumaliza juu ya Simba na Yanga kwa wakati mmoja? Wanaweza ila ni lazima mambo haya ya ndani kabisa wayatambue.

Binadamu tunasema kuwa wivu ni sehemu ya maendeleo, au pengine tunakuwa tunasema kuwa Majungu ni sumu ya maendeleo. AZam kwa sasa wana wivu na matamanio ya kutaka ubingwa wa ndani ili wapate kucheza michuano ya klabu bingwa Afrika. NI jambo zuri kwa kuwa mtazamo wao hauishii tu katika kucheza michuano ya ndani kila mwaka. Ila wakati Jockins Atudo alipokuwa anaondoka katika timu hiyo mwezi ulipita aliwahi zungumza mahali kuwa kuna matatizo fulani ndani ya timu hiyo ambayo yanatakiwa kutazamwa na kuondolewa kama kweli wanahitaji kuwa timu imara ndani ya uwanja.

Yeye alisema kuwa kuna majungu sana ndani ya timu hiyo, huku vinara wakiwa ni makocha wasaidizi wawili wa timu hiyo. Alisema makocha hao wamekuwa wakiwapiga majungu wachezaji kwa viongozi wao wa juu, huku akisikitika pia mtu anayetoka naye nchi moja kuwafanyia wenzake hivyo. Moja ya sababu za wachezaji wa Kenya kushindwa kudumu hapo ni mmoja kati ya makocha hao wasaidizi.

Pia, inakuwaje kila mchezaji akawa na mawasiliano ya moja kwa moja na bosi wa timu. Jambo hili pia limekuwa likirahisha mawasiliano mabaya kati ya wachezaji na mmiliki wa timu. Wakati fulani Salum Abubakary aliposimamishwa na uongozi ni kutokana na ' unoko' wa uliofanywa na mmoja wa wachezaji kwenda moja kwa moja kwa bosi wa timu, na kumopigia simu akimueleza mambo ya uongo.

Jambo lingine ambalo linatakiwa kuachwa kwa sasa ni kuwatumia wachezaji kama sehemu ya kisasi kwa mtu fulani jambo ambalo limemwondoa Hall, ukiacha propaganda zote zilizokuwa zinasemwa ni kocha huyo kujisifia mara kwa mara kuwa ndiye msimu wa soka la Azam. Baadhi ya viongozi wakawa ni watu wa kukasirika, kwa kuwa wao ndiyo walitaka kuwa msingi wa historia ya timu kimafaniko. Hall alijiamini kuja kutwaa ubingwa siku moja kwa kuwa tayari alikuwa anajua namna ya kuziadhibu Simba na Yanga.

Kuwa sehemu ya historia nzuri ni jambo la kupendeza sana, lakini ni wakati wa Azam kutambua kuwa Jose Mourihno ndiye aliywekata ukame wa miaka 50 wa Chelsea kutwaa ubingwa wa ligi kuu, ila huwezi kuzungumzia uwekezaji wa Roma Abramovich kuwa ndiyo sababu ya mafanikio yote hao. Jose atabaki ni ' mtu maalumu' na Roman atabaki mtu wa aina yake katika historia ya Chelsea. Mafaniko ni ya wote. Azam wanaweza kutwaa ubingwa, ila wakumbuke kuwa wachezaji wao ni walevi sana. Au, ndiyo, fanya kazi, upate pesa, ufanye matanuzi?

PICHA ZA WATANGAZAJI NA WANAFAMILIA WENGINE WA CLOUDS FM WAKITOA MISAADA DSM.


100Ni tukio ambalo limefanyika Jan 1 2014 ikiwa ni siku ya kilele cha shamrashamza za miaka 14 ya kuzaliwa kwa Clouds FM ambapo ikiwa ni radio ya watu na kutambua kwamba kuna wengine wanaopitia matatizo kwenye maisha yao kwa wakati huu, team nzima iliingia mtaani na kutoa misaada mbalimbali.
Misaada ilianza kutolewa kwenye hospitali ya Temeke ambapo ilitolewa kwa Wagonjwa na kwa hospitali yenyewe na baada ya hapo team nzima yenye zaidi ya watu 30 ikaelekea moja kwa moja kwenye kituo cha Keko Machungwa ambacho kinamilikiwa na kijana Yohana aliekua anatumia dawa za kulevya ambae ameacha na kuanza kusaidia wengine.
Kwenye kituo hiki ambacho kilitambua umuhimu wa maneno ‘radio ya watu’ kilipeleka maombi ya kusaidiwa mashine ya Compressor ili kurahisisha kazi ya useremala kwenye ofisi ya kituo hiki chenye waathirika 40 ambao baada ya kutibiwa wamekua wakipewa mafunzo ya useremala ili kupata kipato kwa hiyo kazi.
101Team CLOUDS FM na wagonjwa hospitalini
103Mrisho Mpoto ni mmoja wa Wasanii waliojitokeza kuunga mkono.
104Regina Mwalekwa hospitali
105
106Mtu wako wa nguvu kwenye wodi ya watoto
107
122Kuanzia hii picha ya juu na hizi zinazofata ni tukiwa kwenye kituo cha Keko Youth Centre
121Shamba wanalolimia mboga watu wanaosaidiwa na kituo hiki
120Yohana mwenye kituo, Sebastian Maganga ambae ni mkuu wa vipindi Clouds FM pamoja na Said Fela kiongozi wa Wanaume Family.
119
118
117Team Clouds ikimsikiliza Yohana
116Msaada uliotolewa na Clouds FM
115Sehemu ya miradi inayomilikiwa na kituo hiki cha kusaidia watu walioathirika na dawa za kulevya.
114
113Mtu wako wa nguvu na watu wake wa nguvu mtaani, ni furaha yangu.
112Hizi picha hapa chini zinazofata ndio Team Clouds ilikua inakabidhi misaada kwa hospitali ya Temeke.
111
110
109
108

GEBI PRESHA ILIPOIFUNGA CLOUDS MEDIA MABAO 2-1


 Mchezaji wa timu ya Clouds Media Group Said Tully akiwania mpira kuku akizongwa na mchezaji wa ya timu ya Gebi Presha ya Magomeni (kushoto) katika mchezo maalumu wa kusherehekea miaka 14 ya Clouds Media Group uliofanyika katika Uwanja wa Tanganyika Packers jijini Dar es Salaam. Gebi Presha ilishinda 2-1.


Kocha wa timu ya Clouds Media, Alex Lwambano akitoa maelekezo kwa wachezaji wa timu yake wakati wa mchezo huo.
Kocha wa Gebi Presha akiwapa mbinu mpya wachezaji wake.
Mashabiki wa timu ya Gebi Presha wakichagiza ushindi wa timu yao.

Mshambuliaji wa timu ya Clouds Media, Shaffih Dauda akiipangua ngome ya Gebi Presha.