Search This Blog

Saturday, June 23, 2012

Yaliyojili kwenye usahili wa Epiq Bongo Star Search Visiwani Zanzibar

 
WASHIRIKI WAKIPANGA MSTARI KINGIA KWA MAJAJI

 
MADAM RITA AKISIMAMA KUMPONGEZA SALMA YUSUF KWA KUIMBA VIZURI

 
WASHIRIKI WAKISUBIRI ZAMU YAO MBELE YA MAJAJI

 




AWAICHI MAWALLA WA ZANTEL AKIIMBA KWA AJILI YA MAJAJI

BREAKING NEWS! SIMBA YAMSAJILI BEKI MASOMBO LINO TOKA DC MOTEMA PEMBE

Hatimae wekundu wa msimbazi Simba leo hii wamefanikiwa kumsajili beki MASOMBO LINO kutoka klabu ya Dc Motema Pembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Masombo Lino amabaye anacheza nafasi ya beki wa kati amekamilisha uhamisho mara tu baada ya kutua nchini leo asubuhi, awali Simba ilitaka kumsajili beki wa zamani wa Étoile Sportive du Sahel ya nchini Tunisia Gladys Bokese amabaye kwasasa anaichezea Dc Motema Pembe lakini imesitisha mpango huo na kuamua kumpa kibarua MASOMBO.

OKWI AGEUKA LULU SOKO LA USAJILI: SASA TIMU MOJA YA SERIE A NA MAMELODI SUNDOWNS ZAGOMBEA SAINI YAKE

Nyota ya mshambuliaji wa kimataifa wa Simba raia wa Uganda Emmanuel Okwi, inazidi kuwaka, siku chache baada ya klabu bingwa ya Orlando Pirates kutuma barua ya kumtaka mshambuliaji huyo wa Simba aende kufanya majaribio kwenye klabu hiyo, leo hii timu pinzani ya Orlando kwenye ligi ya Afrika kusini, Mamelodi Sundowns wameuambia uongozi wa Simba kwamba wapo tayari kumnunua mshambuliaji huyo.

Taarifa zilizothibitishwa kutoka ndani ya uongozi wa Simba zinasema kwamba Mamelodi wametuma maombi ya kutaka kumsaini Okwi ambaye amekuwa na msimu mzuri sana ndani na nje ya ligi kuu ya Vodacom msimu ulioisha.

Pia chanzo changu hicho cha habari kutoka ndani ya Simba kilisema kwamba kuna timu moja inayoshiriki ligi kuu ya Italia Serie A, wameonyesha nia ya kumtaka Okwi lakini wamesema kwamba wanasubiri mpaka michuano ya Euro itakapoisha ndipo watakapoamua juu ya suala la usajili wa mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uganda.

CHEMSHA BONGO: UNAWAJUA WACHEZA SOKA WEWE? WATAJE HAWA WOTE KWA MAJINA.


Hiki ni kikosi cha moja ya timu zilizoshiriki kwenye Euro 2012.
After a year of scandals, this Barking-born boy is aiming to be crowned champion of Europe for the second time in just two months
2
He shed the unfortunate fringe and has gone on to become England's midfield enforcer and Mr Reliable
1

 
All all-round athlete who excelled at cricket and athletics, this England regular recently won his first league title
5
He replaced Rio Ferdinand, and then Gary Cahill in the England back four, but has been one of the stand out stars of Euro2012 so far
4:


England's youngest ever player, this Londoner has shone so far this summer as manager Roy Hodgson's super sub
8
6: He was tall, even as a schoolboy, but didn't take up football until he was 15 - preferring cricket during his early years.
7


8: England's new captain fantastic, a deadball specialist who has shone with the armband this summer
9   
9: The baby of the team, this photo is barely a decade old. This star in the making is a second generation England player 
14: There's no mistaking that mischievous grin. Back after a break, England fans are praying we've not seen the best of him yet
12: The baby face is long gone on this star, arguably England's best player and the best in the world in his position. If England make the final, it'll win him his 100th cap13: A child footballing prodigy who's living up to his hype. Scorer of one of the best goals of the tournament so far11: England's first choice number 2 and a solid performer in Poland/Ukraine. One of 6 Liverpool players hoping to find success this summer
10: A regular in the England set-up, he shrugged off a personal tragedy to compete at Euro2012, where he hopes to win his 50th cap
Add caption
                                         10

7: Went to the same school as Gazza and followed in his footsteps to Newcastle and then England
10

UJERUMANI WAVUNJA REKODI: WAIFUNIKA SPAIN KWA KUSHINDA MECHI 15 MFULULIZO

Germany wameweka rekodi mpya ya kushinda mechi mfululizo kwenye soka la kimataifa kufuatia ushindi wao 4-2 dhidi ya Ugiriki kwenye robo fainali ya Euro 2012.

Ushindi wa jana dhidi ya mabingwa wa Euro 2004 ulikuwa wa 15 mfululizo kwa vijana wa Joachim Low, wakizivunja rekodi za kushinda mechi 14 mfululizo uliowekwa na Ufaransa, Uholanzi, na Spain.


HIVI NDIVYO WALIVYOWEZA KUVUNJA REKODI


Germany 3-2 Uruguay |
Hapa ndipo vijana wa Low walipoanzia katika kuelekea kuvunja rekodi kwa kushika nafasi ya tatu kwenye kombe la dunia 2010.
Belgium 0-1 Germany | Klose tena aliwatungua Ubelgiji


Germany 6-1 Azerbaijan | 'Podolski aliongoza mauaji haya.

Germany 3-0 Turkey | Ozil na mchezaji mwenzie wa Real Madrid wakiumana kwenye timu zao za Taifa na Ozil kuibuka mshindi.


Kazakhstan 0-3 Germany | Ushindi wao wa tano mfululizo ulikuwa dhidi ya Kazakhstan


Germany 4-0 Kazakhstan | Klose and Muller wote walifunga magoli mawili mawili.


Austria 1-2 Germany | Gomez alipofunga goli la ushindi kwenye dakika za majeruhi dhidi ya Austria.

Azerbaijan 1-3 Germany | Ozil akiwaumiza waarabu wa ulaya

Germany 6-2 Austria | Klose alpowaliza Austria kwenye ushindi wa goli 6-2

Turkey 1-3 Germany | Gotze alipowamaliza Uturuki


Germany 3-1 Belgium | Vinana wa Joachim Low walimaliza michuano ya kufuzu kwa ushindi wa goli 3-0 dhidi ya Ubelgiji.

Germany 1-0 Portugal | Gomez akiwatungua Portugal kwenye mechi ya ushindi ya kwanza ya kundi la kifo Euro 2012..
Netherlands 1-2 Germany | Mario Gomez akafunga foli mbili na kuwapa ushindi Ujerumani dhidi ya Wadachi


Denmark 1-2 Germany | Lars Bender aliwapa uongozi wa kundi la kifo

Germany 4-2 Greece | Lahm, Khedira, Klose & Reus walipovunja rekodi jana.

UJERUMANI YAZIDI KUTISHA - WAITANDIKA 4-2 UGIRIKI: WAWASUBIRI WAINGEREZA AU WAITALIANO NUSU FAINALI

SIRI IMEFICHUKA: MCHEZAJI WA GHANA AKIRI UDANGANYIFU WA UMRI KWENYE TIMU ZA TAIFA

Tabia ya wachezaji wa kiafrika kudanganya umri imezidi kukitihiri kwenye soka.

Mchezaji wa zamani wa kikosi cha under 17 cha Ghana Yaw Preko amekiri kwamba ni kweli amewahi kudanganya umri wake, na kwamba wachezaji wengi waliowahi kucheza michuano ya FIFA ya vijana wamekuwa wakidanganya umri wao halisi.

Preko pamoja na kukiri kudanganya umri, ameiambia Liquid Sports kwamba suala la kudanganya umri sio jambo geni kwenye timu za taifa hasa barani Afrika na Amerika ya kusini.

"Waafrika tunaongoza na hata kwenye bara la South America hakuna nchi ambayo haifanyi udanganyifu wa umri. Nakumbuka tulipocheza nchini Qatar mwaka 1991, tuliona kama tunacheza na timu ya ligi kuu ya England."

Na vipi kuhusu yeye mwenyewe? Alijibu: "Ndio, siwezi kudanganya, sikucheza soka kwa kusema umri wangu sahihi, japokuwa sikupunguza miaka 20 kwenye wangu wa ukweli."

"Kwenye zama zetu chama cha soka ndio kilikuwa kinatupangia umri, tulifanikiwa sana kudanganya juu ya umri wetu ndio maana nilifanikiwa kucheza 17 barani ulaya."

Preko alikuwa mmoja ya wachezaji waliounda kikosi cha Black Starlets kilichoshinda kombe la dunia chini ya miaka 17 mwaka 1991, na pia kile cha Black Meteors kilichocheza kwenye Olympic Games mwaka 1992.

Friday, June 22, 2012

KOLO TOURE AFUNGA NDOA NA MAMA WATOTO WAKE

Mlinzi wa Manchester City Kolo Toure amefunga ndoa na mchumba wake wa siku nyingi na mama wa watoto wake wawili Chimene Akassou siku ya Alhamisi katika mji mkuu wa Ivory Coast - Abdijan, kwenye sherehe iliyowakutanisha watu tofauti kutoka kwenye matabaka tofauti kuanzia kwenye michezo mpaka wanasiasa.

Harusi hiyo imefanyika kwenye msikiti na itaendelea jumamosi ambapo Kolo na mkewe watasaini vyeti vya ndoa kiserikali.

Pia kutafanyika reception ya hatari sana wikiendi hii, huku wageni wengi wakitegemewa kuwa ni wachezaji wa timuya taifa ya Ivory Coast.

Ndugu wa Kolo, na mchezaji mwenzie kwenye klabu na Taifa, Yaya Toure alikuwa ndio best man.

Wanandoa hao wapya wamekuwa wakiishi pamoja Uingereza tangu mwaka 2003, mwaka mmoja baada ya Kolo Toure kuhamia Arsenal akitokea Asec Mimosas.

SHINJI KAGAWA AJIUNGA RASMI NA MAN UTD




Kiungo raia wa Japan Shinji Kagawa hatimae amejiunga na Man utd kwa makataba wa miaka minne.

SD TV: KELVIN YONDANI AKIWA NA KIKOSI CHA YANGA MAZOEZINI!

MISRI YAOMBA KUIKABILI NGORONGORO HEROES

Chama cha Mpira wa Miguu Misri (EFA) kimeomba mechi mbili za kirafiki kwa timu yao ya vijana na timu ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 ya Tanzania (Ngorongoro Heroes).

EFA imeomba mechi hizo zichezwe Julai 3 na Julai 5 mwaka huu kwa masharti maalumu. Ikiwa zitachezwa Misri, mwenyeji (EFA) atagharamia Ngorongoro Heroes kwa malazi, chakula, usafiri wa ndani na sehemu ya kufanyia mazoezi.

Ikiwa mechi hizo zitachezwa Dar es Salaam, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) litaigharamia timu ya Misri kwa malazi, chakula, usafiri wa ndani na sehemu ya mazoezi. Hivyo kila timu itajigharamia kwa usafiri wa ndege na posho kwa timu yake.

Sekretarieti ya TFF inafanya uchambuzi wa gharama ili kujua ipi ni nafuu kabla ya kufanya uamuzi wa wapi mechi hizo zichezwe.

Ngorongoro Heroes imeingia raundi ya pili ya michuano ya Afrika ambayo fainali zake zitafanyika mwakani nchini Algeria baada ya kuitoa Sudan katika raundi ya kwanza.

Itacheza mechi ya kwanza ya raundi ya pili Julai 28 mwaka huu jijini Dar es Salaam wakati ya marudiano itakuwa Agosti 11 mwaka huu nchini Nigeria.

AWAMU YA KWANZA USAJILI MWISHO AGOSTI 10


Kipindi cha kwanza cha usajili wa wachezaji kwa ajili ya msimu wa 2012/2013 kitamalizika Agosti 10 mwaka huu kulingana na kalenda ya Matukio ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ya 2012/2013.
Uhamisho wa wachezaji unafanyika kuanzia Juni 15 hadi Julai 30 mwaka huu wakati kipindi cha kuacha wachezaji (sio wa Ligi Kuu. Wachezaji wa Ligi Kuu wanacheza kwa mikataba) ni kuanzia Juni 15- 30 mwaka huu.

Kwa klabu za Ligi Kuu kutangaza wachezaji watakaositishiwa mikataba yao ni kuanzia Juni 15-30 mwaka huu na usajili wa wachezaji unafanyika kuanzia Juni 15 hadi Agosti 10 mwaka huu.

Tunasisitiza kipindi cha usajili kiheshimiwe na mikoa yote kwa sababu usajili huo huo ndiyo utakaotumika katika michuano ya Kombe la FA. Kwa maana nyingine hakutakuwa na kipindi kingine cha usajili wa wachezaji kwa klabu zote nchini hadi hapo litakapofunguliwa dirisha dogo.

Mechi ya kufungua msimu ya Ngao ya Jamii (Community Shield) kati ya mabingwa wa Ligi Kuu, timu ya Simba na makamu bingwa Azam itachezwa Agosti 25 mwaka huu wakati Ligi Kuu itaanza Septemba Mosi mwaka huu, na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) yenyewe itaanza Septemba 15 mwaka huu.

Ratiba ya Ligi Kuu itatolewa Julai 23 mwaka huu.

TIMU 20 KUCHEZA LIGI DARAJA LA KWANZA

Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeridhia mapendekezo ya Kamati ya Mashindano ya kutaka Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kuwa na timu 20 badala ya 18 za sasa.

Lengo la mabadiliko hayo ni Ligi ya Taifa (NL) kuchezwa kwa kanda, hivyo msimu huu timu mbili zaidi (ukiondoa tatu ambazo zimeshapanda kutoka NL) zitaongezwa ili kufikisha idadi ya timu 20 katika FDL.

Timu ambazo zimepanda kutoka NL iliyochezwa katika vituo vitatu ni; Kanembwa JKT ya Kigoma iliyoongoza Kituo cha Kigoma, Ndanda SC ya Mtwara iliyoibuka kinara Kituo cha Mtwara na Polisi Mara iliyokamata usukani katika Kituo cha Musoma.

Kamati ya Utendaji pia imepitisha mapendekezo ya kuchezwa play off ili kupata timu mbili zaidi za kucheza FDL msimu huu. Timu zitakazocheza play off katika utaratibu utakaotangazwa baadaye na Kamati ya Mashindano ni tatu zilizoshuka kutoka FDL na tatu nyingine zilizoshika nafasi za pili katika NL kutoka vituo vya Kigoma, Mtwara na Musoma.

Timu tatu zilizoshuka FDL ni AFC ya Arusha, Samaria ya Singida na Temeke United ya Dar es Salaam wakati zilizoshika nafasi za pili katika NL na vituo vyao kwenye mabano ni Kurugenzi ya Iringa (Mtwara), Mwadui ya Shinyanga (Kigoma) na Tessema ya Dar es Salaam (Musoma).

Hata hivyo, timu zitakazoshuka kutoka Ligi Kuu bado zitaendelea kuwa tatu kama ilivyo kwa zitakazopandwa.

YONDANI AANZA MAZOEZI YANGA LEO ASUBUHI LEO



 







Kelvin Patrick Yondan, beki wa kimataifa wa Tanzania, ameanza mazoezi rasmi leo katika klabu yake mpya, Yanga SC. Yondan alitinga maeozini asubuhi na kushangiliwa ile mbaya na mashabiki wa klabu hiyo Uwanja wa Kaunda, Jangwani, Dar es Salaam. Picha tofauti zikimuonyesha Yondan mazoezini nYanga

Picha kwa hisani ya BIN ZUBEIRY.


CRISTIANO RONALDO AMJIBU RAISI WA BARCA KWA GOLI - AIPELEKA URENO NUSU FAINALI


Czech Republic 0-1 Portugal (Quarter Final) by fasthighlights-2012

KENNETH ASAMOAH ATEMWA YANGA - KULIPWA FIDIA

Hatimaye mshambuliaji wa Yanga kutoka Ghana Kenneth Asamoah ametemwa na klabu hiyo baada ya kuitumikia kwa takribani msimu mmoja tu.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya Yanga, Asamoah amefikia makubaliano na Yanga kwa kulipwa fidia ya kuvunjiwa mkataba wake aliousaini msimu uliopita.

Kenneth Asamoah anaondoka Yanga huku akiwaachia wapenzi wa klabu hiyo kumbukumbu ya goli zuri la kichwa alilowafunga Simba kwenye fainali ya kombe la Kagame mwaka jana kwenye uwanja wa Taifa.

KWANINI SIMBA NA YANGA ZIMEKUWA NA KASUMBA YA KUWA NA MALIMBIKIZO YA MADENI YA MISHAHARA?

Moja ya sababu kubwa zinazotufanya watanzania tusiendelee kwenye upande wa soka ni kukosa uongozi bora kuanzia kwenye vyama vya soka mpaka kwenye vilabu.


Siasa imewatala sana viongozi wa soka kiasi kwamba mpaka kwenye vitu ambavyo siasa hahitajiki tunajaribu kuiweka ili tuweze kufanikisha malengo yetu binafsi. Suala hili ni moja ya matatizo makubwa yanayoikumbuka soka letu la Tanzania, hasa kwenye vilabu vyetu vikubwa vya Simba na Yanga.


Navitaja vilabu hivi kwa sababu kiukweli lazima tuseme kwamba ndio nguzo kuu ya soka la Tanzania, vyenyewe vinapokuwa vinaboronga basi kwa kweli na soka letu linayumba. Vilabu hivi siku zote vimekuwa vikikosa viongozi wenye mawazo endelevu ya kuvifanya vilabu hivi kuendelea mbele. Moja ya matatizo makubwa yanayosababishwa na uongozi mbovu wa vilabu hivi ni mfumo wa usajili.


Usajili wa Simba na Yanga siku zote unafanywa kihuni, mtu yoyote ambaye anaweza kujiita mdau anaweza akamsajili fulani kwa kutumia fedha zake bila baraka za benchi la ufundi aidha kwa kutaka sifa au kujipigia kampeni kwa kutaka uongozi ndani ya klabu, na mwisho wa siku wachezaji wanaosajiliwa muda mwingine wanashindwa kuingia kwenye mipango ya kocha kwa kuwa labda hakuwa anawahitaji kwenye timu yake.


Pamoja na matatizo yote yanayovikabili vilabu hivi lakini leo katika makala yangu hii nitabase kwenye upande wa usajili. Nasukumwa kuandika makala hii kutokana na hali inayoendelea kwenye vilabu vyetu Simba SC na Dar Young Africans ambao kwa sasa hawana kocha baada ya kocha mkuu Mserbia Kostadin Papic kuondoka.


UPANDE WA YANGA


Yanga ambao kwa sasa wapo katika mchakato wa kufanya uchaguzi baada ya ule uongozi uliokuwepo chini mwanasheria Lloyd Nchunga kujiuzulu, hawana kocha mkuu, lakini cha ajabu timu hiyo inafanya usajili wa wachezaji ambao wanasajiliwa na watu wanaojiita wadau au wanachama wa klabu hiyo. Kesi ya suala la kiufundi tuiache pembeni kwa leo kwa usajili wa wachezaji tuangalie kwa upande wa kiuchumi.


Moja ya matatizo makubwa yaliyoukumba uongozi wa Lloyd Nchunga ni madeni pamoja na malimbikizo ya mishahara na fedha za usajili. Mmoja ya viongozi waliojizulu kwenye uongozi uliopita anasema: "Wakati tupo madarakani tulipatwa na matatizo mengi ya kifedha kwa mfano suala la mishahara. Wachezaji walisajiliwa na kikundi cha watu ambao ni wadau wa Yanga, wakaingia nao makubaliano kwa niaba ya Yanga kwa mfano utakuta wachezaji wamesaini mkataba wa miaka miwili kwa kulipwa mshahara wa dola 1000 mpaka  5000 kwa kiwango cha juu kwa mwezi na posho mbalimbali, wakati ukija kwenye bajeti halisi ya mwezi utakuta fedha yote tuliyonayo inazidi tunayotakiwa kulipa. Na hapo ndipo malimbikizo ya madeni ya mishahara yalipoanza kuzidi. Hili suala lilitokea kwa takribani wachezaji wote pamoja na hata kwa upande wa kocha.
'Pia kulikuwepo na madeni ya fedha za usajili, utakuta fulani anamsajili mchezaji kwa makubaliano ya millioni 30, labda anampa shilingi milioni 20 na 10 zilizobakia anahaidiwa kumaliziwa baadae, muda unapofika mchezaji anapohitaji kumalizia fedha zake, uongozi unashindwa kwa sababu fedha hizo zinakuwa hazipo kwenye bajeti."


Haya sasa hivi Yanga ikiwa haina kocha wala uongozi mkuu, timu imeshasajili wachezaji wasiopungua watano wapya kwa fedha ambazo zinatolewa na kikundi cha wadau wa Yanga, na kama ilivyo kawaida msaada wao wakishamaliza usajili wanauachia uongozi mahitaji mengine ambayo mwisho wa siku yanakuwa yanazidi bajeti nzima ya klabu kwa ajili ya kugharimia matumizi. Hivyo kupelekea timu kujawa madeni na wachezaji kuwa na migomo isiyoisha.
Mwisho wa siku hata huu uongozi mpya unaotarajiwa kuingia madarakani utakutana na hicho kimbembe kwa kuwa haukuhusika kwenye mchakato wa kuwasajili wachezaji.


Kwa hali hii timu itafanya vipi vizuri kwenye michuano inayoshiriki? Hivyo wito wangu kwa wanayanga kuangalia juu ya suala hili la usajili kwa umakini, kama halitowasumbua kiuchumi ikiwa wenye pesa wataingia madarakani basi litakuwa na madhara kiufundi kutokana na usajili kufanywa na watu wasiohusika na benchi la ufundi - nasema kwa kuwa timu sasa inatafuta kocha na bado inasajili mwisho wa siku ndio matatizo ya miaka yote yanaendelea kuikumba klabu hii.

KWA UPANDE WA SIMBA
Simba nao hawana tofauti na ndugu zao Yanga, ingawa wenyewe atleast kwa sasa bado wana kocha na uongozi ukiwa bado upo madarakani.
Lakini linapokuja suala la usajili ishu ipo vile vile kama kwa wenzao Yanga, viongozi ndio wanaosajili wachezaji na sio kocha, ikumbukwe takribani mwezi mmoja uliopita niliandika makala iliyokuwa na kichwa cha habari "UONGOZI MBOVU: KABURU AMSAJILI ABDALLAH JUMA BILA KUPATA BARAKA ZA KAMATI YA UFUNDI".
Hili ni tatizo kubwa sana, yaani mambo yanakwenda ovyo ovyo ndani ya hizi timu mbili, kiongozi mkuu yeye ndio anafanya kila kitu, kulipa mishahara yeye, posho yeye, hata kusajili yeye. Sasa kocha na kamati yake ya ufundi wao kazi yao nini? Hilo moja.


La pili kwenye kusajili wachezaji hao hao, kama ilivyo kwa Yanga, Simba nao wamekuwa na mfumo wa kikundi cha wadau wenye fedha kumsajili mchezaji wanayemtaka na kumleta kwenye timu huku wakiacha msala wa kumuhudumia mchezaji yule kwa uongozi ambao nao unakuwa hauna fungu la kummudu, hivyo kupelekea madeni ya malimbikizo ya mishahara. Tatizo ambalo limekuwepo miaka nenda rudi ndani ya vilabu hivi.


Halafu kwa Simba bado nashindwa kuelewa wapi walipopeleka fedha nyingi ambazo walizipata kutokana na mauzo ya wachezaji kama Mbwana Samatta, Musa Mgosi, na Patrick Ochan,moja ya sababu ambazo Kelvin Yondan kuwa na mgogoro nao ni kutokana kudai kwamba Simba walimkopa fedha za usajili wakati akisaini mkataba mpya. Haya ni matokeo ya timu hizi kujiendekeza na kutokuwa na mipango endelevu ya kuweza kujitegemea zenyewe bila kusubiri kutembeza bakuli kwa watu wanaojiita wadau ambao siku zote wamekuwa ndio wanatumia fedha zao kuvuruga amani kwenye vilabu hivi pale wanapoona interest zao zinaingiliwa.


UTEGEMEZI WA MAPATO YA MILANGONI
Ukiachana mkataba walionao Simba na Yanga kutoka TBL, Vilabu hivi siku zote vimekuwa tegemezi kwa mapato yanayotokana na get collections kuweza kugharamia mambo mbalimbali katika kuziendesha timu hizi mbili. Lakini siku hizi kumekuwepo na utaratibu wa kutoa bonasi kwa wachezaji kila mechi ambazo zinakuwa na matokeo ya sare au kushinda. Pale timu inaposhinda basi asilimia kubwa ya mapato ya milangoni yanaashia kwenda kwa wachezaji, hivyo kile kidogo kinachobakia hakitoshi kuweza kuendesha kwa kugharamia vitu vingine kama vile kulipa mishahara. Japokuwa wanapata fedha fulani kwa mdhamini wao TBL kila mwisho wa mwezi lakini fedha hizo hazitoshelezi kwa sababu Yanga na Simba vinalipa mishahara mikubwa kuliko kile wanachoingiza. Mwisho wa siku ndio unakuta wachezaji wanakopwa mishahara yao mpaka miezi mitano na kuendelea huku wakiambulia posho za mapato ya getini ikiwa timu inashinda au kutoa sare.


Kwa mfumo huu soka letu litaendelea kupata wakati kuendelea mbele. Simba na Yanga badilikeni, viongozi acheni kuvitumia vilabu kwa manufaa yenu binafsi.