Jonathan Kakolaki amekuwa mchezaji wa mwisho kufunga dirisha la usajili kwa Azam FC msimu wa 2012/13. Kakolaki, beki kisiki ambaye amekuwa na Azam FC toka madaraja ya chini hadi ligi kuu mwishoni mwa wiki iliyopita alishinda tuzo ya mchezaji mwenye nidhamu wa Azam FC alimwaga wino wa kuichezea Azam FC mwanzoni mwa wiki na kumaliza uvumi ulioanza kutanda kuwa kuna timu moja kubwa ilikuwa ikimnyatia
Pia kukamilishwa kwa usajili kunavunja tetesi zilizozagaa mitaani kuwa kuna wachezaji wa Azam FC watakaotimkia timu flani au wachezaji wa timu flani kutakiwa kujiunga na Azam FC.
Tofauti na msimu uliopita ambapo Azam FC ilisajili nyota wapya 11 na baadaye kuongeza wengine wanne hapo Disemba na kufikisha jumla ya wachezaji 15 wapya, Msimu ujao Azam FC imeongeza wachezaji wawili tuu ambao ni George Blackberry Odhiambo toka Randers FC ya Denmark na Deo Munishi Dida toka Mtibwa Sukari ya Manungu.
Kwa maana hiyo Azam FC imesajili wachezaji 27 na haijaacha mchezaji hata mmoja ingawa mwalimu Stewart Hall ameacha maagizo ya kupelekwa kwa mkopo wachezaji wanne, ambapo wa kiungo katikati ni wawili, kiungo pembeni mmoja na golikipa mmoja ili kuwapa nafasi ya kucheza kutokana na mlundikano wa wachezaji kwenye nafasi hizo.
Azam FC ambayo itawakilisha nchi kwenye mashindano ya kimataifa hapo mwakani inajivunia kikosi ilichonacho na usajili huu ulikuwa na lengo la kuziba mapengo yaliyoachwa wazi ambapo Blackberry anachukua nafasi ya Mghana Wahab Yahaya na Dida anachukua nafasi ya golikipa Mserbia Obren Cuckovic. Azam FC inajivunia kurudi na kupona 100% Mlinzi George Owino Gere ambaye atanza kuonekana uwanjani kuanzia msimu ujao.
Pia Azam FC inajivunia nyota wake wa Under 20 ambao imewapandisha juu ambao ni Aishi Salum, Juckson Wandwi, Dizana, Ibrahim Rajab Jeba na Joseph Kimwaga
Kikosi Kamili cha Azam FC msimu ujao ni kama ifuatavyo
Magolikipa ni Mwadini Ally, Deo Munishi "Dida" Aishi Salum na Jackson Wandwi
Mabeki wa Pembeni kulia ni Ibrahim Shikanda na Erasto Nyoni na kushoto ni Waziri Salum na Samih Haji Nuhu
Babeki wa kati ni Luckson Kakolaki, Said Moradi, George Owino na Aggrey Morris
Viongo ni Kipre Bolou, Abdulhalim Humud, Himid Mao, Salum Abubakar, Abdi Kassim Sadala, Ramadhani Selemani Chombo, Abdulghani Ghulam, Ibrahim Rajab Jeba, Jabir Aziz Stima, na Ibrahim Joel Mwaipopo
Washambuliaji wa pembeni ni Kipre Tchetche, Mrisho Ngasa, Zahoro Pazi, Khamis Mcha, na George Odhiambo "Blackberry"
Washambuliaji wa kati ni Gaudence Mwaikimba na mchezaji bora wa Azam FC John Raphael Bocco "Adebayor"
Search This Blog
Saturday, May 12, 2012
UDAMBWIDAMBWI KWA HISANI YA KAKA Adam Fungamwango
BABA yake mzazi Aunt Ezekiel!! MCHEZAJI huyu anaitwa Ezekiel Grayson Jujuman! Aliichezea Yanga mwaka mmoja baadaye Simba miaka kibao kuanzia miaka 70 hadi mwanzoni mwa miaka ya 80 hadi anastaafu soka! Sasa ni marehemu na atakumbukwa na wapenzi wa Simba kwa uwezo wake mkubwa wa kusakata kambumbu na chenga za maudhi akiufanya mpira anavyotaka kiasi cha mashabiki kumpachika jina la Jujuman yaani mchawi! Huyu ndiye baba yake mzazi Aunt Ezekiel mwigizaji wa filamu maarufu nchini!!!!
DENNIS BERGKAMP: ANGALIA MAGOLI YAKE 120 NA ASSISTS ZAKE 116 AKIWA NA WASHIKA BUNDUKI WA LONDON
MAGOLI YOTE ALIYOWAHI KUIFUNGIA ARSENAL
PASI ZA MWISHO ZOTE ALIZOTOA AKIWA ARSENAL
PASI ZA MWISHO ZOTE ALIZOTOA AKIWA ARSENAL
PHOTOS: YANAYOENDELEA SUDAN ILIPO SIMBA - WAJIPIKIA CHAKULA WENYEWE
Mjumbe wa kamati ya utendaji ya Simba Swed Nkwabi akiwa na wenzie wakikagua uwanja kabla ya mchezo hapo kesho. |
VITUKO VYAENDELEA SUDAN: SIMBA WANYWESHWA CHAI YA MAZIWA YA NGAMIA
WACHEZAJI wa Simba walijikuta wakinywa chai iliyotengenezwa na maziwa ya ngamia juzi Alhamisi lakini Emmanuel Okwi na Shomari Kapombe walishituka na kunywa chai ya rangi. Simba ikiwa Khartoum ikijiandaa na safari ya kwenda mji wa Shandy, ilifikia katika hoteli ya Sharga ambako ndio walikunywa chai hiyo ya maziwa ya ngamia. Tangu Simba ilipotua Sudan, Jumatano iliyopita, wachezaji wake wamekuwa wakipata shida na chakula cha Sudan. Huku baadhi ya wachezaji wengi kama Felix Sunzu wakila mikate na mayai ya kukaanga na chai maziwa ya ngamia, Okwi na Kapombe wao waliagiza chai ya rangi. Chai ya maziwa ya ngamia ndio inanyweka zaidi nchini Sudan kutokana na kutopatikana maziwa ya ng'ombe, ambao ni nadra sana Sudan kwa kuwa eneo kubwa la huko lina ukame na kufanya upatikanaji wa majani ya kulishia mifugo kuwa mgumu. "Sijawahi kunywa maziwa ya ngamia," alisema Okwi, ambaye sambamba na Kapombe walimtaka mhudumu wa hoteli awapelekee chai isiyokuwa na maziwa. Maziwa ya ngamia yanapatikana kwa wingi Sudan na hutumika kwenye chai katika hoteli na migahawa mingi ya Sudan. Ngamia wako wengi Sudan kutokana na nchi hiyo iliyopata uhuru mwaka 1956 kuwa na eneo kubwa lenye ukame. |
FORTUNE WA MANCHESTER UNITED AOMBA KAZI YA KUIFUNDISHA SERENGETI BOYS
Mchezaji wa zamani wa Manchester United, Quinton Fortune amesema
yuko tayari kuifundisha timu ya Taifa ya Vijana ya Tanzania chini ya
miaka 17 kama atapewa nafasi hiyo kwa sababu kiu yake ni kuona soka ya
Kusini mwa jangwa la Sahara inakuwa na kufikia kiwango cha Afrika
Magharibi na Kaskazini.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Fortune alisema ingawa haifahamu rekodi ya timu ya Taifa ya Tanzania, lakini anaamini kama atapata nafasi ya kuifundisha timu ya vijana itakuwa ni faraja zaidi kwani atakuwa ametimiza kiu yake ya kufundisha soka na kuinua kiwango cha soka la Afrika ya Mashariki.
Fortune ambaye yuko nchini kwa lengo la kuzindua mashindano ya vijana ya Airtel Raising Stars, alisema anaamini wachezaji wa Ukanda huu wa Sahara wana matatizo yanayofanana na ndiyo sababu ya kushindwa kucheza soka katika ligi kubwa duniani kama England.
"Matatizo ya vijana wengi ni elimu ya soka, wana vipaji, lakini lazima upate elimu kwanza ili uweze kufanya vizuri katika soka,"alisema Fortune.
Fortune alisema tatizo lingine ni kushindwa kutafsiri mikataba mbalimbali ya soka, kushindwa kutambua umuhimu na malengo yao katika soka la kimataifa.
Alisema yeye alifanikiwa kucheza Ulaya kwa sababu aliondoka kwao akiwa na miaka 14 na kujiunga na klabu za huko ambazo zilimtunza kufikia hapo.
"Baada ya kumaliza kozi yangu ya ukocha pamoja na kumaliza kazi nilizopewa na klabu yangu ya Manchester United nitarudi Tanzania rasmi kwa ajili ya kufuatilia soka la Tanzania kwa undani zaidi pamoja na kutafuta vipaji na kufuatilia zoezi la Airtel Rasing Stars linavyoendelea pamoja na kuangalia maendeleo yao baada ya hapa,"alisema Fortune.
Mbali na Uzinduzi huo pia Fortune alitembelea Shule ya Msingi ya Maarifa iliyopo Gongolamboto na kucheza soka na wanafunzi wa shule hiyo huku akikabidhi madawati 30 mipira 40 na jezi jozi tatu.

source:http://www.mwananchi.co.tz
UMRI WANGU HAUNIRUHUSU TENA KUCHEZA SOKA LA ULAYA - NESTA ATOA SABABU ZA KUONDOKA AC MILAN.
Katika kizazi cha dhahabu cha soka la kushambulia, ambapo wachezaji wawili wanaweza kufunga magoli nusu karne ndani ya msimu mmoja, muda mwingine ni rahisi sana kusahau kwamba kuna wachezaji wengine wenye ujuzi wanaocheza katika eneo lingine la uwanja ambao kazi yao ni kuwazuia
Mmmoja wao ni Alessandro Nesta, beki mwenye halisi kabisa aliyebarikiwa uwezo mkubwa wa kukaba ambaye akiwa na miaka 36 sasa ameamua kuacha kucheza soka la Seria A.
Alipewa ofa ya mkataba mpya na Milan, Nesta akakataa, akisema kwamba hana tena uwezo uwezo wa kuendelea kucheza soka la level ya kwanza.
"Mchezo wa kasi ya juu ya soka la Italia, champions league na Italian Cup unamaanisha kwamba kwa umri wangu sitoweza kucheza muda wote, Na mimi sio mtu wa kukubali kukaa na kusubiri kwenye benchi."
Hivyo ni wapi panamfaa mchezaji huyu ambaye anakiri sasa umri unamtupa mkono? MLS - ligi ya Marekani.
Alipoulizwa kuhusu kuhusishwa na kujiunga na New York Red Bulls, Nesta akakiri: "Nitaenda kwa moyo mmoja, ningependa kwenda kucheza huko lakini mpaka sasa hakuna kilichosainiwa, na pia kuna nafasi nyingine zimejitokeza kwa ajili yangu.

RAUL AIOKOA TIMU YAKE YA UTOTONI KUFILISIKA
Raisi wa klabu ya San Cristobal del los Angeles, Pedro Albares Iniesta, amesema leo kwamba klabu hiyo imenusurika kufilisika na kuvunjika kabisa kutokana na mchango wa £4,000 kutoka mchezaji wa zamani maarufu kabisa katika historia ya klabu hiyo, Raul Gonzales Blanco.
Mshambuliaji huyo alikaa na klabu hiyo miaka mitatu kabla ya kujiunga academy ya Atletico Madrid mwaka 1990 na baadae kuhamia Real Madrid.
Klabu ya San Cristobal ilitangaza wiki kadhaa zilizopita kwamba wanahitaji kupata kiasi cha £4,000 kabla ya mwisho wa June ili kuweza kuiwezesha klabu hiyo kuendelea kuwepo - na hapo ndipo mchezaji wao wa zamani alipokuja kutoa msaada.
"Nimetaarifiwa kwamba fedha kutoka kwa Raul zimeshatumwa na na kila kitu kimekaa sawa sasa,: Iniesta alisema jana Alhamisi.
"Raul anamaanisha kila kitu hapa. Lakini tumemuomba kitu kimoja kingine : tunataka aje hapa siku moja tumkumbatie na tuongee na kumkumbusha siku zile za zamani...."

Friday, May 11, 2012
BREAKING NEWS! SIMBA WAZIMIWA TAA,WAZUIWA KUFANYA MAZOEZI
Wachezaji wa Simba wakiwa wameduwaa uwanjani baada ya kukataliwa kufanya mazoezi na timu ya wenyeji ikiendelea na mazoezi.
Taarifa nilizozipata hivi punde Simba imezuiliwa kufanya mazoezi na wenyeji wake timu ya AL AHLY Shendi.
'' Visa vimekuwa vikubwa mno hata sijui hawa jamaa wanataka nini,jamaa wamegoma kutuachia uwanja tufanye mazoezi ''- Mjumbe wa kamati ya Utendaji,Swed Nkwabi

KALI YA LEO: MMILIKI WA KAMPUNI YA KUBETI KUPOTEZA £500,000 CITY WAKICHUKUA UBINGWA.
Mwaka 1998, muasisi na mmiliki wa kampuni ya kubeti(wazee wa kuweka mizigo) Fred Done alipoteza £500,000 kwa kuweka mzigo au kubeti mapema kwamba Manchester United watachukua taji la Premier League wakati timu hiyo ilipokuwa ikiongoza kwa pointi 12 mbele ya Arsenal - lakini baadae Arsenal wakaiifikia United na kuwazidi kwa pointi moja na kutwaa ubingwa.
Done ambaye alikuwa ndio mtu wakwanza kutoa kucheza kamari mapema katika mbio za ubingwa za msimu huo na ungeweza kufikiri labda angejifunza, lakini haikuwa hivyo.
Mwezi uliopita, Bwana Done ambaye ni shabiki mkubwa wa Man United - alilipa kiasi cha £500,000 kwenye kubeti kwamba klabu yake anayoipenda itachukua kombe tena. Done alikaririwa akisema hivi kwenye mtandao wa twitter.
"Hata bado kukiwa kuna Manchester Derby na huu uongozi wa pointi tano ni vigumu sana kwa City kutupiku, hivyo kwa mara nyingine tena naweka mzigo wangu mapema kwa United kiasi cha nusu millioni paundi.
"Mwaka 1998 baada ya Arsenal kuchukua ubingwa Fergie aliniambia nisirudie tena kuweka fedha zangu mapema lakini Sir Alex hahitaji kuwa na wasiwasi, siwezi kukosea tena mara hii, United kwa hakika watabeba ndoo msimu huu."
Lakini kama ambavyo baadhi ya wafanyakazi wa United wanavyosema kwamba kamwe usiudharau ushauri wa Sir Alex Ferguson. Mambo yamegeuka City wamepangua uongozi wa pointi 5 za United na sasa jumapili wanaweza kubeba ndoo na kumfanya bwana Fred Done kupoteza zaidi ya billioni moja za kitanzania kwa mara nyingine tena ndani ya miaka 12.
Ili bwana Done aepuke hasara hiyo inabidi QPR wapate matokeo ya chanya dhidi ya City na United washinde mechi ya dhidi ya Sunderland na kubeba ubingwa wa 20 wa EPL.

MARK HUGHES KUPEWA PAUNDI MILLION MOJA AKIWEZA KUWAZUIA CITY KUCHUKUA NDOO JUMAPILI
Mark Hughes yupo njiani kupokea kiasi cha £1millioni kama bonasi ikiwa ataiwezesha QPR kubaki katika Barclays Premier league Jumapili na matokeo ambayo ambayo yanawza kutibua sharehe za Manchester City kunyakua kombe lao kwanza la ligi baada ya miaka 43.
Wasaidizi wa Hughes, Mark Bowen na Eddie Niedwiecki, pia watapata mkwanja mrefu ikiwa Rangers watabaki EPL.
Timu hiyo ya London Magharibi inahitaji japo pointi moja tu pale Etihad Stadium kuepuka kushuka darJ. Ingawa Roberto Mancini na vijana wake wanahitaji ushindi ili kujihakikishia ubingwa wa ligi wa kwanza tangu 1968, huku mahasimu wao Manchester United wakiwa wanahitaji ushindi na kuiombea mabaya City ili kuweza kubeba ubingwa wa 20.
City walimtimua Hughes mwaka 2009 na kumpa ulaji Roberto Mancini - jambo ambalo mwalimu wa United Sir Alex Ferguson akikielezea kitendo hicho ni kwamba hakikuwa sahihi.

MMILIKI WA QPR TONY FERNENDES AKIMKUMBATIA HUGHES. |
City walimtimua Hughes mwaka 2009 na kumpa ulaji Roberto Mancini - jambo ambalo mwalimu wa United Sir Alex Ferguson akikielezea kitendo hicho ni kwamba hakikuwa sahihi.
AC MILAN YAZIDI KUKIMBIWA NA MASTAA WAKE: BAADA YA NESTA JANA - LEO GATTUSO KUONDOKA MWISHO WA MSIMU
Siku moja baada ya Alessandro Nesta kutangaza kwamba ataondoka AC Milan mwishoni mwa msimu leo hii kiungo wa kutumainiwa wa ukabaji wa klabu hiyo Gennaro Gattuso nae ametangaza ataondoka San Siro mwishoni mwa msimu.
Gattuso ambaye alijiunga na AC Milan mwaka 1999, amefanikiwa kuichezea timu hiyo mechi 463 na kufunga mabao 11 - huku akitwaa makombe mawili ya Seria A, Coppa Italia 1, Supercopa Italia 2, UEFA Champions league 2, UEFA Super Cup 2, FIFA Club World Cup 1.

KIMENUKA YANGA: WANACHAMA WAFANYA VURUGU MAKAO MAKUU - POLISI WAPAMBANA NAO
Baadhi ya wanachama wa Yanga wakifanya
fujo klabuni hapo kupinga mkutano wa waandishi wa habari uliokuwa
ufanywe na mwenyekiti wa klabu hiyo Bw. Loyd Nchunga leo mchana ambapo
polisi walifika klabuni hapo na kuimarisha ulinzi.
Mmoja wa askari akimuondoa mmoja wa wanachama wa klabu hiyo katika eneo lililokuwa na vurugu klabuni hapo.
Polisi wakiwa katika magari yao tayari kabisa kuzuia vurugu endapo zingezuka klabuni hapo.
Moja wa magari ya polisi likiwa limeegeshwa nje ya klabu hiyo kwa ajili ya kulinda usalama klabuni hapo leo mchana. |
unafahamu kwanini Yanga walibadili kutoka nyeusi to kijani?
unafahamu kwanini Yanga walibadili kutoka nyeusi to kijani? wapenzi wa yanga watajibu sahihi lakini
mashabiki watajibu kishabiki kama kawaida yao.sijui wewe mwenzangu uko kundi gani? dah yaani haya
majembe haya acha kabisa. kwa wa sasa wakina nani wanawezafananishwa kiduchu na hawa? bado wa simba.
* * *
From Left; Hamisi Gaga Gagarino (marehem), saidi mwamba kizota (marehem), David Mwakalebela,
Method Mogella (marehem) abeid mziba Ken Mkapa(captain) na Salum kabunda ninja.
Aaah, Enzi hizo bana.., watoto mlioanza kushabikia mpira 2005 mnawakumbuka hao ??
TP MAZEMBE NAO YAWAKUTA YA SIMBA -WAFANYIWA VITIMBI NA AL MERREIKH - GARI LAO LASHAMBULIWA NA RISASI
Utaratibu wa timu za kisudani kuzipokea vibaya timu pinzani zinapoenda kucheza nchini kwao umeendelea, baada ya Simba sasa ni TP Mazembe ambao jana mashabiki wa klabu ya Al Merreikh ya Sudan wameufanyia fujo msafara wa klabu ya Tout Puissant Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) mjini Khartoum, wakidai na wao walipokewa vibaya na klabu hiyo mjini Lubumbashi wiki mbili zilikzopita. Mazembe yenye washambuliaji wawili Watanzania, Mbwana Ally Samatta na Thomas Emmanuel Ulimwengu ipo Khartoum kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Merreikh, hatua ya 16 Bora. Katika vurugu hizo, basi walilokuwa wamepanda wachezaji wa Mazembe limevunjwa vioo na athari zaidi ikiwemo hali hali za wachezaji bado hazijajulikana. Sasa mechi hiyo iliyopangwa kufanyika kwenye Uwanja wa Omdurman, hatima yake ipo mikononi mwa Shirikisho la Soka Afrika (CAF)- ambayo inatarajiwa kuchukua hatua muda mfupi ujao, kubwa zaidi ikitarajiwa kuifuta mashindanoni Merreikh na kuifungia hivyo Mazembe kusonga mbele. |
OMBI LA JULIO LASIKILIZWA: JAN POULSEN ATEMWA TAIFA STARS - MDOGO KIM ACHUKUA NAFASI
Siku mbili baada ya kocha Jamahuri Kihwelo kutoa maoni kwamba Kim Poulsen ndio mwalimu sahihi wa kuifundisha timu ya taifa ya Tanzania, leo hii shirikisho la soka nchini TFF limeamua kutomuongezea mkataba Jan Poulsen na kumpa jukumu la ukocha wa timu ya taifa mdogo wake Kim Poulsen ambaye alikuwa akipigiwa chapuo na Julio.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, Rais wa TFF, Leodegar Tenga amesema Kim amepewa mkataba wa mwaka mmoja baada ya Shirikisho kuamua kutomuongezea mkataba Jan. Mkataba wa Jan uliokuwa wa miaka miwili unamalizika Julai 30 mwaka huu.
Amesema kwa vile Taifa Stars inakabiliwa na mechi za mchujo za Kombe la Dunia raundi ya pili Kanda ya Afrika na mechi za mchujo za Kombe la Mataifa ya Afrika (CAN), TFF imeona ni lazima iwe na kocha mpya mapema kabla ya mkataba wa Jan kumalizika.
Kim ambaye ni raia wa Denmark amekuwa nchini kwa mwaka mmoja sasa akifundisha timu za Taifa za vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) na miaka 20 (Ngorongoro Heroes), hivyo anawafahamu vizuri wa wachezaji wa Tanzania.
TFF imeanza mchakato wa kutafuta kocha mwingine wa timu za vijana atakayeziba nafasi ya Kim. Ili kuwa na makocha wenye falsafa moja, kocha huyo anatafutwa kutoka Denmark.
Bakari Malima ‘Jembe Ulaya’-2
Nonda Shabani 'Papii ' watatu waliosimama kutoka kushoto,Bakari Malima wapili waliochuchumaa kutoka kushoto
*Nonda Shaaban alishangaa kuniona nipo pale Kinshasa
*Siku chache akaniachia mamilioni, nikamalizia nyumba yangu
*Wakati naanza kuzoea, nikaambiwa nindoke Congo si salama
Na Saleh Ally
LEO ASUBUHI, Malima alikuwa ameungana na kundi la waandishi wa habari waliokuwa wanamsubiri Nonda atoke kwenye chumba cha hoteli. Hakujua la kufanya kwa kuwa alibakiwa na dola 50 ambayo isingetosha kumpeleka kokote?
WAKATI nikiwa pale na waandishi ninasubiri, mara mdogo wake aliingia kwenye maegesho ya hoteli yaliyokuwa upande wa nyuma, taratibu akashuka kwenye lile gari aina ya Range Rover Vogue.
Baada ya kuniona akanikumbuka, nilimsogelea na kuanza kuzungumza naye na kumueleza niliamua kuwahi kuja pale hotelini. Haraka nilipata wazo, nikatoa zile picha nilizopiga na Nonda wakati tukiwa Dar es Salaam na Afrika Kusini.
Zilimshangaza sana, akaonekana kuamini kuwa kweli mimi na kaka yake ni marafiki. Aliniambia nimuachie aingie nazo akampe Nonda ili amuulize kama angeweza kuniona. Mara moja nikakubali wazo lake na akaondoka nazo kwenda ndani.
Baada ya muda niliona waandishi wakiongezeka upande niliokuwepo, baadhi walianza kuweka vifaa vyao sawa, kwangu ilikuwa ni dalili kwamba Nonda alikuwa anakuja upande wetu.
Nilijaribu kujumuika na waandishi, kila mmoja alitaka kuzungumza naye. Nilijaribu kuinuka juu ili akitokea anione. Kundi la waandishi lilikuwa kubwa sana na baada ya muda mchache nilimuona akija upande wetu akiwa anaongozana na yule mdogo wake.
Nilijitahidi kukaza macho upande wake, lakini niliona asingeweza kuniona. Nilichoamua ni kufanya lolote na liwe, nilipanda juu, sehemu ambayo niliamini ataniona na mara moja nikamuita kwa sauti ya juu. Aligeuka upande wangu na aliponiona akashituka na kusema: “Bakari, vipi! Siku hizi unaishi hapa?”
Sikujali kama waandishi walikuwa wanatusikiliza, nilimueleza nilitoka Lubumbashi kwa ajili ya kumfuata yeye. Aliniambia ingekuwa vizuri tukaongozana pamoja hadi nyumbani kwake. Nikamuacha aendelee na mkutano na waandishi na baada ya hapo, tukaungana na kupanda gari lake.
Baada ya muda mchache tulikuwa nyumbani kwake, hatukukaa muda mrefu sana ingawa aliniuliza maswali kadhaa na alishangazwa na namna nilivyopata shida hadi kufikia kulala nje.
Tulipofika kwake hatukukaa muda mrefu, mara moja alinionyesha sehemu ambayo nilioga na kuvaa nguo nzuri ambazo zilikuwa zake. Baada ya hapo, tukaondoka pamoja kuelekea sehemu maalum kwa ajili ya chakula na baadaye akanipeleka nyumbani kwao.
Baba yake ni raia wa Burundi na mama yake ni Mkongo, nilifika hadi nyumbani kwao ambako alinitambulisha kwa wazazi na ndugu zake na kuwaeleza namna tulivyoishi vizuri kwa kuelewana wakati tukiishi Tanzania na Afrika Kusini.
Akawaambia wazazi wake wanichukulie kama mtoto wao hata kama ikitokea nimeenda pale yeye akiwa hayupo Kongo basi wanipokee vizuri. Wazazi walifurahi sana na baada ya kuzungumza nao kwa kipindi fulani, mimi, Nonda na mdogo wake tukatoka na kuingia mtaani.
Kwa kuwa nilikuwa nikikatiza naye mitaa, baada ya muda mfupi tu nikawa maarufu pale Kinshasa, ilikuwa lahisi sana kujulikana kutokana na umaarufu wake katika eneo hilo.
Siku zake za kurejea Ufaransa ziliwadia, hivyo Nonda akaniambia lazima ataondoka, akanitaka niendelee kubaki pale nyumbani kwake hata kama itakuwa ni mwezi au zaidi ili niendelee na maisha yangu kama nitaona inafaa. Kwangu niliona bora nifanye hivyo.
Kilichotokea kizuri ni kwamba, Nonda alinipa fedha, kwa kweli siwezi kutaja lakini ilinisaidia sana. Ilikuwa ni fedha nyingi ambayo kiasi fulani ilisaidia kuimalizia nyumba yangu ya Kinondoni. Kwa wakati huo sikuwa na sababu ya kuondoka haraka.
Baada ya kupokea fedha, niliamua kubaki, nikamueleza. Siku iliyofuata nilimsindikiza uwanja wa ndege nikiwa na yule mdogo wake na baada ya hapo wote tukarejea nyumbani. Maisha yakaendelea Kinshasa na safari hii nilikuwa mwenyeji kila kona.
Nikiwa nimeanza kuzoea hasa mji wa Kinshasa, kikajitokeza kitu kimoja cha ajabu sana. Watu walikuwa wakiniomba fedha kila waliponiona, maana nilikuwa maarufu kama rafiki wa Nonda. Unajua kabla hajaondoka alikuwa akikutana na watu, aliwagawia fedha.
Kwa kuwa alishaondoka, ikawa ni zamu yangu kuombwa fedha. Kiana nikawa najitutumua lakini nilipozidiwa nikaanza kujikausha. Yule mdogo wake akanishauri kitu kimoja cha msingi.
Akaniomba bora niondoke na kurejea Dar es Salaam maana Kinshasa haukuwa mji salama na kitu kibaya zaidi watu wengi waliamini huenda Nonda aliniachia mamilioni ya dola. Akasema wangeweza kunivamia siku yoyote wakidhani nina mamilioni nimehifadhi.
TAYARI MALIMA AMEPEWA USHAURI WA KUONDOKA JIJINI KINSHASA. JE, ATAKUBALIANA NAO AU ATAAMUA KUENDELEA KULA RAHA NA WASHIKAJI ZAKE. endelea kufuatilia http://www.shaffihdauda.com/
Simba sasa yateswa Sudan
Na Ezekiel Kamwaga, Khartoum
*Walishwa lunch saa 10 jioni
*Chakula cha usiku saa sita usiku
*Rage, Kisaka, wanyimwa pa kulala, walala mapokezi
* Wachezaji wajifua kivyao
UONGOZI wa Simba SC unakusudia kuwasilisha malalamiko rasmi kwa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kutokana na unyama inaofanyiwa nchini Sudan inakosubiri pambano lake dhidi ya Al Ahly Shendi kesho.
Tangu iwasili nchini Sudan juzi, Simba imekuwa ikifanyiwa vitendo visivyo vya kiungwana na wenyeji wake, Shirikisho la Soka Sudan (SAF) na Al Ahly Shendi.
Jana, Simba ilifanyiwa vitendo hivyo kabla ya kwenda katika mji wa Shendi itakakochezwa mechi hiyo na baada ya kufika katika mji huo uliopo takribani kilomita 170 kutoka mji mkuu Khartoum .
Simba iliwasili Shendi majira ya saa mbili usiku kwa saa za Sudan (sawa na saa za huko) baada ya safari ya takribani masaa manne kutoka Khartoum .
Safari ya kutoka Khartoum hadi Shendi ilianza majira ya saa kumi jioni na timu ikafika saa mbili usiku, kwa maana ya masaa manne ya safari ya barabara jambo ambalo ni kinyume cha kanuni za CAF zinazozungumzia umbali usiozidi masaa mawili.
Ingawa kanuni ya CAF kifungu cha 5 (3) kinazungumzia umbali wa kusafiri kwa basi usizidi kilomita 200, Simba inaweza kutuma malalamiko kwamba kutoka Khartoum hadi Shendi ni zaidi ya kilomita 150 kwa vile si haiwezekani kutumia masaa manne kwa umbali huo.
Zaidi ya usumbufu huo wa kusafiri muda mrefu, Simba pia inajiandaa kutuma malalamiko CAF kwa vile hoteli waliyopangiwa haina kiwango kinachokubalika na shirikisho hilo .
Kwa mujibu wa kanuni ya CAF kifungu cha 7 (c), timu mwenyeji inatakiwa kuhakikisha kuwa timu mgeni inaishi katika hoteli ya daraja la kwanza na pia msafara mzima unakaa katika hoteli moja.
Hata hivyo, Simba imewekwa katika hosteli inayofanana na mabweni ya wanafunzi na imepewa vitanda 24 tu huku msafara ukiwa na watu takribani 30.
Wakati ilipokuja Tanzania , Simba ililipia gharama za watu 30 wa timu hiyo na kulikuwa na makubaliano kwamba na wao watafanya hivyo wakati Wekundu watakapokwenda Sudan .
Kutokana na ukosefu huo wa vyumba, Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage, alilala kwenye makochi ya chumba cha mapokezi pamoja na kocha msaidizi wa makipa wa Simba, James Stephan Kisaka.
Viongozi wengine wa Simba, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Swedy Mkwabi na kiongozi wa msafara, Hussein Mwamba ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, pia walikosa pa kulala na hivyo wakalazimika kwenda kulala nje ya hosteli hiyo ya Shendi.
Wakizungumzia hali hiyo, wawakilishi wa timu ya Shendi walidai kwamba inatokana na ukweli kuwa mji wao ni mdogo na hakuna hoteli nyingine kubwa kuliko hiyo mji mzima.
“Kusema kweli mlitupokea vizuri sana tulipokuja Dar es Salaam na hatuna malalamiko yoyote yale. Hata hivyo, huu ndiyo uwezo wetu na hatuna la kufanya. Hata Ferroviaro ya Msumbiji walikaa hapahapa walipokuja hapa, alisema Hamdy Ibn Hossein,” mwakilishi wa Shendi.
Rage alisema Simba itacheza mechi yake dhidi ya Shendi wakati tayari ikiwa imewasilisha malalamiko yake CAF kupitia kwa kamisaa wa pambano hilo ambaye alitarajiwa kuwasili hapa jana jioni (Ijumaa).
“Hawawezi kusema kwamba kwa sababu Ferroviarro walikaa hapa basi na sasa tukae. Hii si hoteli inayosemwa na CAF, hii ni hosteli ya kuweka wanafunzi. Huu ni uvunjaji wa wazi wa kanuni na tunaukataa,” alisema.
Ingawa Simba iliwasili Shendi saa mbili usiku, chakula kilicheleweshwa hadi saa sita usiku ambako wachezaji waliamshwa kula jambo linaloonyesha kuwa hujuma zimepangwa.
Jana, magazeti ya Tanzania yaliripoti kuhusu Simba ilivyotelekezwa katika hoteli ya Safiga jijini Khartoum kuanzia saa nne asubuhi hadi saa kumi jioni bila ya taarifa yoyote huku wenyeji wakidai wamekwama kwenye foleni.
Kutokana na Simba kuingia Shendi usiku, Kocha Mkuu, Milovan Cirkovic, aliamua kuwapa wachezaji mapumziko hadi jana lakini wachezaji waliamua kujifanyia mazoezi wenyewe.
Mmoja wa wachezaji waliokuwa wakijifanyia mazoezi binafsi ambayo yanajulikana kwa jina la individual, alikuwa ni Haruna Moshi Boban ambaye alikutwa akifanya mazoezi ya peke yake kuzunguka eneo la hosteli ilikofikia timu.
“Tangu juzi hatujafanya mazoezi kwa sababu ya safari na vituko vya hawa wenyeji wetu. Nimeamua kujifua mwenyewe kwa sababu ukikaa muda mrefu bila mazoezi hata mwili nao unazoea ulegevu. Ndiyo maana najifua,” alisema.
Zaidi ya Boban, wachezaji wengine waliokutwa wakifanya mazoezi majira hayo ya saa tano usiku ni Mwinyi Kazimoto, Juma Kaseja, Patrick Mafisango, Shomari Kapombe, Uhuru Selemani na Emmanuel Okwi.
Katika mechi ya kwanza iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Simba iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 na inahitaji sare ya aina yoyote au kufungwa chini ya mabao 3-0 ili kusonga mbele.
Airtel Yatoa Msaada wa Madawati na Mipira kwa shule za Msingi za Maarifa, Mwangaza na JICA zilizopo Gongolamboto Jijini DSM
Msanii wa kizazi kipya Ambwene Yesaya maarufu kama AY, akiwatumbuiza wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Maarifa iliyopo Gongo La Mboto nje kidogo Jijini Dar es Salaam wakati Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel ilipotoa msaada wa madawati 30, mipira ya miguu 40 na jezi seti tatu, Alhamisi Mei 10, 2012 ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mtaa (Elimu) Mh. Kassim Majaliwa. Shule zingine zilizofaindika na msaada ni Maarifa, JICA na Mwangaza zote za Gongo La Mboto, Dar es Salaam
Mchezaji wa zamani wa Klabu ya Manchester United ya Uingereza Quinton Fortune, akikabidhi moja ya madawati yaliyotolewa na Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Maarifa Mareitha Mulyalya huku Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Elimu), Mh Kassim Majaliwa akitazama. Kampuni ya Airtel Tanzania ilitoa mipira 30, jesi seti tatu na madawati 40 kwa shule za msingi za Maarifa, JICA na Mwangaza zote za Gongo La Mboto, Dar es Salaam.
Mchezaji wa zamani wa Klabu ya Manchester United ya Uingereza Quinton Fortune, akikabidhi moja ya mipira iliyotolewa na Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Maarifa Mareitha Mulyalya huku Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Elimu), Mh Kassim Majaliwa akitazama. Kampuni ya Airtel Tanzania ilitoa mipira 30, jezi seti tatu na madawati 40 kwa shule za msingi za Maarifa, JICA na Mwangaza zote za Gongo La Mboto, Dar es Salaam
Mchezaji wa zamani wa Klabu ya Manchester United ya Uingereza Quinton Fortune, akifurahia na wanafunzi wa shule ya Msingi ya Maarifa baada ya kukabidhi madawati 30, mipira 40 na jesi seti tatu zilizotolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania. Shule zingine zilizofaidika na msaada huo ni pamoja na Mwangaza na JICA zote za Gongo La Mboto, jijini Dar es Salaam. Msaada huo ulikabidhiwa na Naibu Waziri wa Tawala za Mkoa na Serikali za Mitaa Kassim Majaliwa, Alhamisi Mei 10, 2012.

CHEMSHA BONGO! TOFAUTISHA HIZI PICHA !
Zitofautishe hizi picha za mchezaji Javier Zanetti zikiwa ktk taswila mbali mbali tangia akiwa na umri wa miaka 17 mpaka leo hii akiwa na miaka 38.
TWIGA STARS, ZIMBABWE KUUMANA LEO
Timu ya Taifa ya mpira wa miguu kwa wanawake ya Tanzania (Twiga Stars) na Zimbabwe zinapambana kesho (Mei 12 mwaka huu) katika mechi ya kirafiki ya kimataifa itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Twiga Stars ambayo ilikuwa katika ziara ya mechi za kirafiki katika mikoa ya Dodoma na Mwanza imerejea leo (Mei 11 mwaka huu) jijini Dar es Salaam tayari kuikabili Zimbabwe. Ikiwa Mwanza jana ilicheza mechi ya kirafiki dhidi Rock City Queens, lakini mechi hiyo ilivunjika dakika ya 58 kutokana na mvua kubwa. Hadi mechi inavunjika, Twiga Stars ilikuwa ikiongoza kwa mabao 5-0.
Kwa mujibu wa kocha wa Twiga Stars, Charles Boniface Mkwasa, mechi hiyo itakuwa kipimo kizuri kwao kabla ya kucheza mechi ya mashindano ya Afrika (AWC) dhidi ya Ethiopia. Mechi hiyo itachezwa Mei 26 mwaka huu jijini Addis Ababa kabla ya kurudiana Dar es Salaam wiki mbili baadaye.
Naye Kocha wa Zimbabwe, Rosemary Mugadza amesema amefurahi kupata mechi hiyo kwa vile anaamini Twiga Stars ni kipimo kizuri kwao kabla ya kucheza mechi yao ya AWC dhidi ya Nigeria.
Twiga Stars na Zimbabwe zilishakutana mara mbili mwaka jana. Mara ya kwanza ilikuwa nusu fainali ya Kombe la COSAFA ambapo katika mechi hiyo iliyochezwa Julai 5 jijini Harare, Zimbabwe ilishinda kwa penalti 4-2.
Mechi ya pili ilikuwa michezo ya All Africa Games (AAG) iliyofanyika Maputo, Msumbiji ambapo timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2.
Viingilio katika mechi hiyo itakayochezeshwa na mwamuzi wa kimataifa Judith Gamba kuanzia saa 10.30 jioni ni sh. 1,000 tu kwa sehemu zote isipokuwa VIP A ambayo ni sh. 10,000 na VIP B ambayo kiingilio chake ni sh. 5,000.
RAMBIRAMBI MSIBA WA MWANDISHI RACHEL MWILIGWA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha Mhariri wa Michezo wa gazeti la Mtanzania, Rachel Mwiligwa kilichotokea leo (Mei 11 mwaka huu) katika Hospitali ya Mwananyamala, Dar es Salaam. Msiba huo ni mkubwa katika sekta ya habari na mpira wa miguu kwani Rachel kwa kipindi chote akiwa mwandishi na baadaye Mhariri alikuwa akifanya kazi nasi, hivyo mchango wake katika mpira wa miguu tutaukumbuka daima. TFF inatoa pole kwa familia ya marehemu Rachel, kampuni ya New Habari ambayo ndiyo inayomiliki gazeti za Mtanzania na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito. Mungu aiweke roho ya marehemu Rachel mahali pema peponi. Amina
Bakari Malima ‘Jembe Ulaya’-Nilifunga safari hadi Kinshasa, nikalala nje ya geti la Nonda,
Na Saleh Ally
*Baridi ilinipiga usiku kucha bado sikumpata
*Kabla, nilikamatwa na polisi kwa dawa za kulevya
MWAKA 2006 ndiyo Bakari Malima maarufu kama Jembe Ulaya aliamua kutundika daruga na kustaafu soka la ushindani, baada ya hapo yakaanza mambo mengine ya maisha.
Kabla ya hapo, Malima anajulikana kutokana na uwezo wake mkubwa wakati anaichezea timu ya Yanga na Vaal Professionals ya Afrika Kusini pamoja na timu ya taifa, Taifa Stars.
Sifa kubwa ya Malima, ilikuwa ni uwezo mkubwa katika ulinzi na kufunga mabao ya vichwa. Kila mshambuliaji aliyekabana na Malima alijua kazi aliyonayo, mwisho akabandikwa jina la Jembe Ulaya.
Baada ya kustaafu soka, pamoja na biashara ndogo ndogo, Malima aliamua kufanya kazi, aliajiriwa kuendesha mitambo na magari makubwa katika machimbo ya Barrick huko mkoani Shinyanga.
Maisha ya Malima, yamejaa misukosuko mingi nje ya uwanja na huenda akawa mmoja mchezaji mwenye simulizi za kusitikisha. Kupitia ukurasa huu wa Maisha Baada ya Soka, Malima anasimulia mambo yaliyowahi kumkuta.
Nonda Shaaban:
Nonda alikuwa alikuwa rafiki yangu mkubwa, wakati tukicheza wote Yanga alikuwa akiishi nyumbani kwangu kwa kipindi kirefu. Tuliishi vizuri sana na maisha yetu yalikuwa ni mazuri tu.
Wakati tulipokwenda Vaal Professionals kule Afrika Kusini, mwenzangu alifanikiwa kupata kibari cha kucheza soka na mimi nikakosa. Nitaelezea baadaye, labda nianze na mwishoni halafu nitarudi mambo yalivyokuwa mwanzo.
Maana nimewahi kukutana na misukosuko mingi sana, nakumbuka nikiwa nimebakiza mwaka mmoja kustaafu soka wakati huo nachezea timu ya Twiga, nilipata taarifa kuwa Nonda angerudi kwao Congo kwa ajili ya mechi ya kimataifa.
Wakati huo Nonda ambaye nilikula naye msoto Dar es Salaam na Afrika Kusini alikuwa amefanikiwa kimaisha. Alikuwa anaichezea Monaco ya Ufaransa na alishakuwa mshambuliaji tegemeo.
Nikaona itakuwa ni vizuri niende kumuona, maana baada ya kujaribu sana maisha tena kwa juhudi lakini mambo yalikuwa ni magumu na wakati huo soka lilikuwa linaenda ukingoni.
Unajua kuna wakati niliwahi kukamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam (DIA), kwa tuhuma za madawa ya kulevya. Nayo ikanirudisha nyuma sana, nitahadithia baadaye namna mambo yalivyokuwa.
Hivyo nilianza safari ya kumfuata Nonda, nilipofika Lubumbashi, hakukuwa na namna, ilikuwa ni lazima nipande ndege hadi Kinshasa ambako mechi ilikuwa inachezwa. Nakumbuka Congo walitoka sare katika mechi hiyo.
Baada ya hapo, nilianza kazi ya kuhakikisha nakutana na Nonda kwa kuwa kulikuwa kuna mambo mawili yalinitia hofu. Kwanza, sikuwa na fedha za kutosha, mfukoni nilikuwa na dola 50 tu.
Pili sikuwa na miadi na Nonda, halafu baada ya kufika Kinshasa nikagundua alikuwa ni staa mkubwa. Kila mtu aligombania kumuona na ulinzi wake ulikuwa mkali sana, hivyo kumuona ilikuwa ni mbinde.
Nilianza kutafuta alipokuwa anaishi, lakini ilikuwa ni kazi kubwa watu kukubali kunionyesha. Mtu mmoja alinielekeza hoteli aliyokuwa anaishi na nilipofika pale wakanieleza huwa analala nyumbani kwake.
Hivyo nilianza kutafuta watu wa kunielekeza wapi anakoishi, pia ilikuwa ni kazi kubwa wao kukubali. Niliwaeleza kuwa nilicheza naye soka Tanzania na baadaye Afrika Kusini, walikubali kunielekeza baada ya kuwaonyesha picha zangu na Nonda ambazo tulipiga pamoja.
Baada ya hapo, mmoja wao akanielekeza na kuniambia nisiseme kama yeye alinielekeza kwa kuwa hawakuruhusiwa kufanya hivyo. Basi nikaenda hadi sehemu niliyoelekezwa na nilipofika pale nikamkuta mlinzi.
Kukawa na tatizo kubwa limeibuka, yule mlinzi alikuwa hazungumzi Kiswahili wala Kingereza, alizungumza Kifaransa na Kilingala. Tukawa hatuelewani, ukazuka mzozo mkubwa kati yetu.
Mzozo huo ulisababisha majirani watoke, mmoja wao alisogea karibu na kutaka kujua kilichokuwa kinaendelea. Nikamueleza kuwa mimi ni Mtanzania na nilicheza soka na Nonda, shida yangu ilikuwa ni kukutana naye.
Basi akazungumza na yule mlinzi ambaye alizidi kuonyesha ni mkorofi, akasisitiza nikae pembeni. Yule jirani akaingia ndani na kutoka na kiti, geti lake lilikuwa karibu kabisa na pale kwa Nonda. Akaniambia nimsubiri pale.
Akaniambia kuna gari aina ya Range Rover Vogue ndiyo anatumia akiwa pale Kinshasa, hivyo niliona basi nijitambulishe. Lakini akasisitiza kama nitakuwa simjui Nonda, nitaingia matatizoni.
Nikakaa kwenye kiti pale nje, ilikuwa ni baridi kali sana, nilitetemeka usiku kucha hadi ilipofika muda kama saa tisa usiku, nikaona taa za gari. Nilipoangalia kweli ilikuwa ni Vogue inakuja. Nikaona nikizubaa tu, nitamkosa jamaa. Nikasimama katikati ya geti.
Yule mlinzi alikasirishwa na kitendo change, akataka kunitoa lakini taratibu vioo vya gari vikateremshwa na nikashituka baada ya kuona aliyekuwa kwenye gari ni mdogo wake na Nonda na si yeye mwenyewe.
Alihoji sababu ya mimi kusimama katikati ya geti, nilianza kumuelezea na nilishukuru alipoanza kuzungumza Kishwahili. Alionekana kunielewa, lakini akasisitiza kwa kuwa haniamini maana hanijui vizuri, nirudi na kulala tena pale nje hadi asubuhi.
Alisema akiamka, tutaongozana kwenda kwa Nonda ambaye alikuwa amelala hotelini na aliniambia ingekuwa vigumu kuruhusiwa kumuona bila ya kwenda naye.
Sikuwa na ujanja, nilirudi pale kwenye kiti nilichopewa na jirani. Dakika chache jirani akatoka na kuniuliza imekuwaje, nikamueleza mambo yalivyokwenda. Akaniambia niendelee kusubiri.
Nikalala pale hadi alfajiri, yule jirani wa Nonda aliyenipa kiti akatoka na kunishauri. Alinieleza kwamba huenda yule mdogo wake Nonda akalala hadi saa nne asubuhi, hivyo ingekuwa vizuri kama mwenyewe ningeondoka na kwenda hotelini kujaribu kumpata.
Niliona ni wazo zuri, nikarejesha kiti chake na kumshukuru, wakati huo nilikuwa sijala siku ya pili. Nikaanza safari ya kwenda kumtafuta Nonda. Nilipofika hotelini, bado hawakukubali nimuone, wala hawakutaka kumpigia simu.
Mhudumu mmoja akanishauri nizunguke nyuma ya hoteli kwa kuwa lazima angepitia huko. Niliamua kufunya hivyo na huko niliwakuta waandishi kibao wa habari ambao walikuwa wanasubiri kuzungumza na Nonda.
Hofu ya Malima ni kama kweli ataweza kumuona mshikaji wake, Nonda Shaaban Papii. Akimkosa, ataishi vipi au atarudi vipi Tanzania wakati amebaki na dola 50 pekee ambayo ugenini ni matumizi ya siku moja tu? MKASA ZAIDI, TUENDELEE KUWA PAMOJA!
Thursday, May 10, 2012
BAADA YA MASAA MANNE BARABARANI SIMBA YAFIKA MJI WA SHANDY KWA TAABU: WENYEJI WAWAKIMBIA - HAWAJALA KITU CHOCHOTE KWA MASAA TAKRIBANI SITA SASA
Hatimaye baada ya masaa manne ya kusafiri kutoka Khartoom mpaka Shandy wawikilishi wa Tanzania katika michuano ya kimataifa ya soka Simba SC imefika mjini Shandy salama kabisa.
Lakini katika hali ya kushangaza wenyeji wao timu Al Ahly Shady wamepotea na kuwaacha wageni wao Simba katika hali tata - kwa mujibu wa mchezaji Emmanuel Okwi wamefikia sehemu mbaya na tangu wamefika takribani masaa sita yaliyopita hawajitia kitu chochote mdomoni. "Bwana huku tumefika lakini kwa shida sana, tunashukuru mungu tumefika salama ila tangu tumefika hapa hatujatia kitu chochote mdomoni na wenyeji wetu hawaonekani. Ila tunawaomba wanasimba na watanzania kwa ujumla waendele kutakia kheri na tunawahidi hizi hila za wasudani hazitowaepusha na kipigo siku ya mechi." - Emmanuel Okwi.
ON THIS DAY: NAPOLI WACHUKUA UBINGWA WAO KWANZA WA SERIE A WAKIWA NA JEMBE DIEGO ARMANDO MARADONA
Siku kama ya leo miaka 25 iliyopita, Napoli walisherehekea ubingwa wao wa kwanza kabisa nchini Italia.
Matokeo ya sare dhidi Fiorentina yaliwawezesha Napoli kuwa timu ya kwanza kutoka kusini mwa Italia kushinda kombe la Scudetto chini ya mwanaume Diego Maradona.
Matokeo ya sare dhidi Fiorentina yaliwawezesha Napoli kuwa timu ya kwanza kutoka kusini mwa Italia kushinda kombe la Scudetto chini ya mwanaume Diego Maradona.
BRAZIL YATANGAZA SHERIA MPYA KWA AJILI YA KOMBE LA DUNIA 2014 - POMBE RUKSA VIWANJANI
Seneta ya Brazil hatimaye imeptisha sheria ya kombe la dunia na kutoa guarantii kwa FIFA waliyokuwa wakihitaji juu ya kuandaa kombe la dunia mwaka 2014.
Sheria hiyo imekuja siku moja baada ya serikali ya Brazil kukutana na maofisa wa FIFA nchini Switzerland kujadili maandalizi ya nchi hiyo na kusuluhisha tofauti zao.
Sio watu wote wamefurahishwa na sheria hiyo. Vilevi vimekatazwa katika viwanja vya soka nchini Brazil tangu mwaka 2003, na baadhi ya wabunge wameonekana kuwa na wasiwasi na usalama viwanjani baada ya mabadiliko mapya yaliyofanyika katiba sheria mpya.
Sheria mpya imeruhusu uuzwaji wa pombe ndani ya viwanja wakati wa kombe la dunia na michuano ya mabara.
Uuzwaji wa vilevi viwanjani ulikatazwa baada ya matukio vurugu kuzidi viwanjani nchini humo - hivyo kuna baadhi ya wabunge wa nchi hiyo wanahisi suala hilo linaweza likahatarisha usalama.

BREAKING NEWS: ADIDAS KUIDHAMINI TAIFA STARS
Habari za uhakika nilizozipata kutoka ndani ya shirikisho la soka Tanzania TFF ni kwamba kampuni ya utengenezaji wa mavazi ya Adidas imeingia mkataba wa kuidhamini Taifa Stars katika suala zima la jezi. Kwa taarifa zaidi endelea kutembea http://www.shaffihdauda.com/
Subscribe to:
Posts (Atom)