Search This Blog

Saturday, August 18, 2012

EDWARD CHRISTOPHER WA SIMBA B APIGA HAT TRICK FAINALI YA SUPER8 NA KUIBUKA MFUNGAJI BORA

Mshambuliaji wa klabu ya Simba B ambaye msimu ataonekana kwenye ligi kuu ya Tanzania bara, Edward Christopher ameibuka mfungaji bora wa michuano ya BancABC Super8 iliyomalizka leo kwa klabu ya Simba B kutwaa ubingwa wa michuano hiyo mipya.

Edward ambaye kabla ya mchezo wa leo alikuwa na mabao matano, katika mchezo wa fainali ya leo aliweza kufunga hat-trick na kusiadia timu yake kubeba ubingwa huku yeye mwenye akimaliza akiwa na magoli nane na hivyo kutawazwa kuwa mfungaji bora wa michuano hiyo ambayo ndio imefanyika kwa mara ya kwanza msimu huu.


SIMBA B WAITANDIKA MTIBWA 4-3 - WABEBA KOMBE LA BANCABC SUPER8

Timu ya soka Simba B ya Dar es salaam leo imefanikiwa kuwa mabingwa wa kwanza wa kombe la BancABC Super8 baada ya kuifunga Mtibwa Sugar ya Morogoro kwa mabao 4-3 katika mchezo mkali wa fainali uliochezwa kwenye dimba la taifa jijini Dar es Salaam.

Simba ndio waliokuwa wa kwanza kuzisalimu nyavu za Mtibwa katika dakika ya 18 kipindi cha kwanza baada ya mshambuliaji wake hatari Edward Christopher, kabla ya Shabaan Kisiga hajasawazisha dakika ya 31.

Mpaka mchezo unaisha kwenye dakika 90 timu hizo zilikuwa zimefungana mabao 3-3, na hivyo kupelekea timu hizo kuelekea kwenye dakika 120 na ndipo kwenye dakika hizo Simba wakapata bao la ushindi, na mpaka dakika 120 zinakamilika Simba 4-3 Mtibwa. 

Kwa usindi huo Simba B imelamba kiasi cha millioni 40 kama zawadi ya mshindi, huku Mtibwa kama washindi wa pili wakitia benki millioni 20.

OFFICIAL: BARCELONA NA ARSENAL ZAKUBALINA ADA YA UHAMISHO WA ALEX SONG


Klabu ya FC Barcelona imetangaza jioni hii kwamba imefikia makubaliano juu ya ada ya uhamisho wa kiungo Mcameroon Alexander Song kutoka Arsenal.

Song sasa atasafiri kwenda Barcelona ndani masaa 48 yajayo kwa ajili ya kufanya vipimo na kujadiliana huu ya maslahi binafsi kabla ya kusaini mkataba na Barcelona.

Uhamisho huu wa Song unakuja siku moja baada ya Robin Van Persie kukamilisha uhamisho wa kujiunga Manchester United akitokea Arsenal. Kuondoka kwa Song kunamaanisha Arsenal sasa itakuwa imeuza wachezaji wake muhimu waliocheza kwa kiwango kikubwa msimu uliopita na kuiwezesha kushika nafasi ya 3 kwenye ligi kuu ya England.

Alex Song anakuwa mchezaji wa nne wa Arsenal kujiunga ba Barcelona katika kipindi cha miaka 5 iliyopita, wa kwanza akiwa Thierry Henry, akafuatiwa na Alexander Hleb, Cesc Fabregas na sasa mcameroon huyo.

HAYA NDIO MABAO 132 YA ROBIN VAN PERSIE ALIYOYAFUNGA TANGU AJIUNGE NA ARSENAL MPAKA ANAONDOKA

KALI YA LEO: GOLI KAMA HILI ANGEJIFUNGA BARTHEZ AU KASEJA KWENYE MECHI YA SIMBA NA YANGA INGEKUWAJE???

MABADILIKO YA UONGOZI YANGA YALIVYOCHELEWESHA MCHAKATO WA KAMPUNI YA LIGI KUU (TPL)

Wakati ligi kuu ya Tanzaia bara ikiwa imepangwa kuanza ndani ya wiki mbili zijazo, kumekuwepo  hakuna taarifa yoyote rasmi juu ya muendeshaji wa ligi hiyo kampuni (Tanzania Premium League -TPL) ambayo itakuwa ikiundwa na vilabu vishiriki vya ligi kwa pamoja na TFF kama wenye hisa.

Kama itakumbukwa wakati wa ligi ya msimu uliopita ikiwa imefikia katikati, vilabu vya ligi kuu kwa kushirikiana na wadau tofauti walianzisha harakati za kutaka ligi kuu ya msimu uliopita ngwe ya pili iendeshwe na kampuni ya vilabu vyenyewe na sio TFF kama ilivyo kwenye ligi kuu za Kenya, EPL na nyingine duniani.

Vikaendeshwa vikao na ikaundwa kamati ya kushughulikia mchakato wa uanzishwaji wa kampuni iliyokuwa chini ya Uenyekiti wa Godfrey Nyange Kaburu akisaidiwa na katibu mkuu wa Yanga Celestine Mwesiga na viongozi wengine wa vilabu. Kamati ile ilifanya kazi usiku na mchana kuhakikisha awamu ya pili ya ligi msimu uliopita inachezwa chini ya TPL, lakini ikaenda na ikaonekana kwamba muda haukuwa sahihi kwa TPL kuichukua ligi katikati mwa msimu, hivyo ikashauriwa na TFF chini ya Leogdar Tenga iundwe kamati ya ligi kuu ambayo ingesimamia ligi kuu kwa nusu ya msimu iliyobakia na kampuni itachukua ligi msimu mpya huu wa 2012-13. Ikaundwa kamati ambayo iliundwa na timu ya viongozi hawa vilabu, Kaburu, Celestine Mwesiga, Meja Charles Mbuge, Said Mohamedi, Seif Ahmed 'Magari', na Henry Kabera.

Ligi ikaisha na mchakato wa kuanzisha Tanzania Premium League - TPL unaendelea vizuri na ilikuwa imebaki tu umoja wa vilabu wakiwakilishwa na kampuni yao  kukutana na shareholder mwingine TFF ili kuweza kuweka sawa mipango na taratibu za miwsho kabla ya mchakato kukamilika.

Ikumbukwe mwanzoni kabisa wakati wa kuanzishwa kwa mchakato wa kuunda kampuni vilabu vilishakubaliana vyote kwa pamoja kwamba wote watakuwa na haki sawa kwenye kampuni hiyo. Lakini hivi karibuni mambo yote yakiwa yapo mwishoni kwa bahati mbaya au nzuri mabingwa wa Kagame Cup wakafanya mapinduzi kwenye safu ya uongozi wa klabu yao, na hatimaye wakapata uongozi mpya chini mwenyekiti Yusuph Manji.

Wakati kikifanyika moja ya vikao vya mwisho, Manji kama mwenyekiti wa Yanga  alipata nafasi ya kuhudhuria kikao kimojawapo na ndipo akaleta hoja mpya ambayo ilishajadiliwa kuhusu mgawanyo wa mapato ya kampuni - akisema haifahamu na kwamba Simba na Yanga ndio vilabu vikubwa na vyenye kuingiza faida nyingi hivyo haviwezi kupata mgawo sawa na vilabu vidogo, akijenga hoja hiyo itakuwa ni kuvionea vilabu vya Simba na Yanga. Matokeo yake viongozi wa vilabu wengine wakapingana nae na wakasema hilo lilishajadiliwa na maamuzi yalishapitishwa chini ya viongozi wawikilishi wa vilabu vya Simba na Yanga - Godfrey Kaburu na Celestine Mwesiga,  hivyo kushindwa kufikia maafikiano na mambo kushindikana kuendelea mbele.

Wakati haya yakiendelea mdhamini anayemaliza muda wake wa udhamini kampuni ya simu ya Vodacom alionyesha nia ya kutaka kusaini mkataba mpya, kupitia mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo ikawasiliana na TFF juu ya kuanza mazungumzo ya mkataba mpya wa udhamini wa ligi, na kwa kuwa TFF yenyewe itaiachia kampuni ya TPL kuendesha ligi kuu hivyo Tenga imebidi aitishe mkutano na viongozi wa vilabu ambao tayari wameshaanza kutokuelewana juu ya maslahi - wakae pamoja ili kuweza kuujadili mkataba mpya na Vodacom kwa ajili ya udhamini wa ligi ya msimu ujao.

Friday, August 17, 2012

GWIJI LA ARSENAL IAN WRIGHT ASEMA: "VAN PERSIE AMEFANYA CHAGUO SAHIHI KUJIUNGA NA MAN UNITED.

Ian Wright na Van Persie
Robin Van Persie amejiunga na Manchester United kutokea Arsenal, na kwanza kabisa naomba nikiri sidhani kama ameondoka kwa sababu ya fedha.

Mholanzi huyo ambaye alikuwa nahodha wetu ameenda Old Trafford kwa sababu anaamini kuichezea United kutampa nafasi nzuri zaidi ya kushinda makombe.

Na hili linatuumiza mashabiki wa Arsenal.

Van Persie alijiunga na Gunners mwezi May 2004, muda mchache baada ya klabu yangu ya zamani kumaliza msimu bila kufungwa katika ligi kuu ya England.

Hii ilikuwa timu bora kabisa ya Arsenal. Ilikuwa na uwezo wa kuendelea kutawala kwa misimu mingi zaidi.

Lakini, mwaka baada ya mwaka, wachezaji wakubwa waliondoka.

Jens Lehman, Ashley Cole, Sol Campbell, Robert Pires, Thierry Henry na Patrick Vieira wote wakaondoka.

Na tangu awasili kutoka Feyenoord, Van Persie aliweza kushinda kombe moja tu - FA Cup, miaka saba iliyopita.

Ni aibu kubwa kuona mholanzi huyu akiwa anaungana listi ndefu ya wachezaji wazuri kuondoka Arsenal, ingawa haijanishangaza. Kama mashabiki wa Arsenal wanakuwa wakweli wa hisia zao, naamini hawatokuwa wameshutushwa  pia. Ni dalili za wakati mbaya.

Timu tatu ambazo siku zinaonekana kuweza kushinda makombe ni United, Man City, na Chelsea.

United hawakushinda chochote msimu uliopita na baadhi ya watu wanasema Alex Ferguson alikuwa na kikosi kibovu kuliko vyote katika historia ya kuifundisha United.

Lakini bado walipoteza kombe lao kwa tofauti ya magoli katika dakika za mwisho za ligi.

Kwa hakika mambo yatakuwa tofauti msimu wa 2-12/13, kama ambavyo imekuwa ni vigumu kwa United kumaliza msimu bila kushinda chochote.

Sipendi na ninachukia sana kuona wachezaji muhimu wakiondoka Emirates na itaendelea kuzidi kuwa vigumu kwa klabu kuwashikilia wachezaji wao wengine muhimu.

Kumbuka, Theo Walcott anakaribia mwisho wa mkataba wake akiwa amebakisha mwaka mmoja kwenye mkataba wake na naomba asaini mkataba mwingine mpya wiki chache zijazo.

United, City na Juventus wote walikuwa wakimtaka Van Persie lakini nafikiri amefanya maamuzi sahihi kujiunga na United.

City wapo katika kipindi cha kusisimua  na wanaweza kushinda makombe mengi miaka kadhaa ijayo.

Lakini bado Van Persie ambaye ana miaka 29 ameshindwa kukataa kuichukua nafasi ya kuichezea klabu kubwa zaidi duniani. Wachezaji wakubwa wanataka kucheza na wachezaji wenzao wakubwa - na kwa hilo Van Persie amelipata kwani atakuwa na nafasi ya kufanya uharibifu mkubwa kwenye nyavu za maadui akiwa sambamba na Wayne Rooney.

Ferguson siku zote amekuwa akiongoza timu na kuwajenga kuwa na winning mentallity na Van Persie, inaeleweka anataka kuwa mmoja ya timu ya namna hiyo.

Msimu uliopita, aliibeba Arsenal. Inabidi ujiulize ni wapi tungemaliza kwenye msimu bila mabao yake 37.

Nina hisia za kumuonea huruma sana Arsene Wenger lakini, mwishowe yeye ndio anafanya maamuzi ya mwisho katika kucheza kwa mchezaji na kutoa ofa ya mkataba mpya.

Baadhi ya watu wanasema Van Persie ingebidi aonyeshe upendo zaidi kwa Arsenal, baada ya majeruhi yote ambayo aliyapata. Lakini kama nilivyosema mwanzoni, upendo wa dhati siku hizi unatoka kwa mashabiki tu na hili jni jambo ambalo itabidi likubaliwe.

Kwa kuwaondoa wachezaji kama Ryan Giggs, Paul Scholes pale United na John Terry pale Chelsea, hakuna wachezaji wanaoweza kudumu kwenye timu moja milele.

Arsenal sasa tunajikuta kwenye wakati mgumu.

Klabu imesajili washambuliaji kama Lukas Podolski kutoka Cologne, mshambuliaji wa Ufaransa Olivier Giroud kutoka  Montpellier na kiungo wa Kispain Santi Cazorla kutoka Malaga, ambao wanaweza kufanya vizuri kwenye EPL.

Lakini angalia natumia neno "wanaweza".

Wenger anahitaji wachezaji hawa kucheza vizuri sana, lakini inawezekana sio jambo zuri sana kuwa na mategemeo makubwa sana kwa wachezaji hawa watatu wapya.

Nafunga mikono yangu nikiomba, wote wafanye vizuri mapema zaidi.

Mashabiki wengi wa Gunners wataangalia ratiba ya ligi na kufahamu tarehe za mechi za United.

Itakuwa pale Old Trafford november 3, ambayo itakuwa Birthday yangu, United wataikaribisha Arsenal kwenye mechi ya kwanza, kabla ya vijana hao wa Fergie hawajasafiri kwenda Emirates April 27.

Sitaki kufikiria wala kuwaza kwamba Van Persie atapata mapokezi mazuri na nina uhakika hatokuwa akitegemea kupata mapokezi mazuri.

Kwa bahati mbaya, Arsenal kwa mara nyingine tena ni lazima waendelee mbele kufuatia kuondoka kwa jina lingine kubwa klabuni.

Unaweza ukaweza nini wangefanya au wangekuwa na nini kama wachezaji wote wangebaki Emirates.

Kwaheri RVP - Nakutakia kila la kheri @Theatre of Dreams. 


Imeandikwa na Ian Wright 

KUELEKEA FAINALI YA BANCABC SUPER8 HAPO KESHO: HIKI NDICHO ALICHOKI-POST KOCHA WA SIMBA SELEMANI MATOLA KWENYE FACEBOOK

WANAGU HAPA NIKAMA MWAKA MMOJA NUSU ULIOPITA.
 
TUOMBE MUNGU WANA CMBA KESHO IWE KAMA HIVI

Azam FC walipotembelea kituo cha watoto yatima Moshi

JOHN BOCCO AENDELEA VIZURI SUPERSPORTS UTD.

PICHA 11 ZA RVP AKIWA KWENYE SIKU YA KWANZA YA MAZOEZI NA MAN UTD!











HIVI NDIVYO WASHABIKI WA ARSENAL WALIVYOUMIZWA NA VAN PERSIE KWENDA MAN UNITED




 Jana nilitoa nafasi kwa mashabiki wa Arsenal kuweza kutoa maoni yao juu ya suala la uhamisho wa mshambuliaji Robin Van Persie kwenda Manchester United, mamilioni ya washabiki wa Arsenal duniani walianza kuitumia kila nafasi wanayoipata kutoa maoni juu ya uhamisho huo, wengine walimtakia kheri, wengine walimkashifu na kumpa majina ya ajabu ajabu huku wengine wakijaribu hata kuchoma hata jezi zake. Kutokana na hilo nilijaribu kutoa nafasi kwa washabiki wa Arsenal ambao ni wadau wa mtandao huu kutoa maoni yao juu ya uhamisho wa Robin Van Persie. Na haya ni baadhi ya yale niliyotumiwa.
 
 
 
 
Finley Fabregas
Habari Bw. Dauda,
 
Naandika maneno haya sio kwa kejeli au furaha, mie ni muanga mkubwa wa zoezi hili.
 
Ukija katika dawati langu la kazi nna kikombe (mug) chenye charter/log ya washika bunduki,    mwanangu wa kwanza na nnae huyo tu hadi sasa anajulikana kwa Finley Fabregas (wakati wa ubatizo wake padre wa Kanisa Katoliki pale Moro aligoma, lakini baadae akaelewa), namaanisha nini ? Hapa ni kuwa RVP katutenda km ilivyokuwa mwaka jana kwa Cesc..... ila Arsenal chini ya Mkufunzi nimwite Mchumi Mzee Arsene WENGER ni mzalishaji kwani watatokea akina van Persie wengi tu msimu huu, na pale ukiondoka kwa kajeli umeumia kwani wapi akina  Flamini, Helb nk walikuwa wakupotea leo la hasha..... akituuzi tutampiga majeruhu msimu mzima (kosa lake RVP ni kwenda siko, kwa mahasimu basi).
 
Inshalaah guners ipo na itaendelea kuwepo, acha tuumie japo mechi 3 za awali,
 
 
Na Baba Finley

Ndugu Shaffih Dauda.
  Mimi kama mshabiki wa klabu ya Arsenal ya Uingereza nimesikitishwa sana na hatua iliyofikiwa na klabu ya Arsenal ya kumuuza mshambuliaji Robin Van Persie kwenda Manchester United. Katika historia yote ya klabu ya Arsenal kuwa na wachezaji wazuri na baadae kuwauza pindi wanapotakiwa na klabu nyingine lakini hii ya kumuuza Van Persie kwenda Man United ndiyo imefunga jarada. Hii inaonyesha jinsi gani sasa ushindani na uhasimu katika mpira wa miguu umekwisha.. Kitu kikubwa sasa klabu kama Arsenal inajali mapato zaidi na sio mafanikio ya klabu.Arsenal na Man United ni maadui wakubwa katika ligi ya Uingereza mpaka ukiona viongozi wao wanakaa meza moja na kujadiliana kuuziana wachezaji ujue sasa uhasimu umeisha watu wana jali pesa. Je ulisha wahi sikia America waka kaa meza moja na Russia kujadili kuuziana silaha?Je ulisha wahi sikia ati serekali ya Afganistan ika kaa meza moja na wafuasi waTaliban kujadili kuuziana silaha? Uongozi wa Arsenal umefanya yote mabaya lakini hili la kumuuza Van Persie kwa wahasimu wao Man United halitasahauliwa na mashabiki wa Arsenal duniani kote. Kila wakati timu hizi zitakapo kutana msimu huu basi vurugu zitatokea kwa washabiki kumzomea sana Van Persie au kupigana kati ya mashabiki watimu zote mbili.Biashara ya Van Prsie toka Arsenal kwenda Man United naiona kama imekiuka misingi mingi ya uadui katika timu hizi mbili. Kwa miaka mingi mashabiki wa Arsenal watamchukia sana Van Persie kuliko wachezaji wengine waowahi kuhama kama vile Nasri,Adebayor, KoloToure, Ashely Cole, na wengineo.
DOCTOR.
MSHABIKI WA ARSENAL, STOCKHOLM-SWE

OFFICIAL: ROBIN VAN PERSIE ATAMBULISHWA RASMI MANCHESTER UNITED ASAINI MIAKA MINNE

Robin van Persie akisaini mkataba wake wa miaka minne wa kujiunga na Manchester United mbele manager wa klabu hiyo Sir Alex Ferguson mchana huu makao makuu ya klabu hiyo jijini Manchester.

DEBATE: KITENDO CHA ARSENAL KUMUUZA VAN PERSIE KWENDA MAN UTD,JE NDIO MWISHO WA UPINZANI NA UHASAMA BAINA YA HIVI VILABU VIWILI ?


ROBIN VAN PERSIE akiwasili kwenye hospitali ya bridgewater tayari kufanyiwa vipimo vya afya ili kumalizia taratibu za kujiunga na MAN UTD.

RAISI JAKAYA MRISHO MRISHO KIKWETE ASEMA AHADI YAKE YA KUILETA REAL MADRID IPO PALE PALE


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa bado ni dhamira ya Serikali yake kuileta moja ya timu za Ligi Kuu ya Soka ya Hispania (La Liga) kutembelea Tanzania na amemtaka Balozi mpya wa Hispania katika Tanzania kusaidia kufanikisha dhamira hiyo.

Aidha, Rais Kikwete ameipongeza Hispania kwa kutetea ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Ulaya (Euro) 2012 katika mashindano yaliyomalizika mwezi uliopita nchini Poland na Ukraine.

Akizungumza na Balozi mpya wa Hispania, Mheshimiwa Luis Manuel Cuesta Civis mara baada ya kupokea hati yake ya utambulisho katika hafla fupi iliyofanyika jana Ikulu jijini Dar es Salaam leo, Rais alisema: “Wananchi wa Tanzania, ambako timu za Hispania, zina washabiki na wafuasi wengi, bado wanasubiri kwa hamu ziara ya moja ya timu kubwa za Ligi Kuu ya Soka ya Hispania. Tunataka ije hapa, icheze mechi moja ama mbili na itembelee mbunga zetu maarufu za wanyama,” alisema Rais Kikwete na kuongeza:

“Kama utakavyokuja kuthibitisha mwenyewe, Watanzania ni watu wanaopenda michezo na hasa soka na ni wafuatiliaji wakubwa wa Ligi Kuu ya Hispania ambako timu zenye mvuto zaidi ni Real Madrid na Barcelona.”

Rais Kikwete pia aliipongeza Hispania kwa kutetea ubingwa wake wa Ulaya.

“Tunawapongeza sana kwa kuweka historia. Kwanza mlishinda Kombe la Mataifa ya Ulaya, kisha mkashinda Kombe la Dunia. Sasa mmeweza kutetea Kombe la Ulaya. Hili halijapata kutokea kwa nchi moja kushikilia vikombe vyote viwili vikubwa vya soka duniani kwa wakati mmoja ama nchi kutetea Kombe la Ulaya.”

GOLI BORA LA SIKU: ANGEL DI MARIA NA LIONEL MESSI WALIVYOIUA UJERUMANI 3-1





IKIWA UNAMTAKA CRISTIANO RONALDO ITAKUBIDI KULIPA €1 BILLION

Kila mchezaji anayo bei yake, ingawa vilabu vimekuwa vikijaribu kila njia kuweza kukaa na  wachezaji wao muhimu, lakini siku zote inakuwa ngumu jambo lililopelekea kuwa zinawawekea vipengele vya beighali ikiwa kuna klabu itakuja kuwataka kuwanunua wakiwa bado kwenye mkataba husika.  
 Kupitia utafiti mdogo uliofanyika tumeweza kugundua na kupata kujua ni wachezaji  gani wanaongoza kwa kuwekewa vipengele vya kuuzwa fedha nyingi kuliko wenigne.


Cristiano Ronaldo
€1bn
 

Lionel Messi
€250m
 

Fernando Torres
€127m
 

Hulk
€100m
 

Thiago Alcantara
€100m
 



PICHA MUHIMU: TANGU SIKU YA KWANZA ALIPOSAJILIWA MPAKA ANAPOONDOKA ARSENAL - ROBIN VAN PERSIE


Siku akiwa anatambulishwa katika uwanja wa zamani wa Arsenal Highbury

Mazoezini siku ya kwanza

Akisherehekea moja ya makombe yake ya kwanza kabisa kushinda akiwa na Arsenal - kombe la FA Cup baada ya kuifunga Manchester United kwa penati 5-4



Majeruhi yalipoanza kumuandama

Moja ya magoli bora kabisa akiwa na Arsenal - hapa akiwatungua Charlton

Aliposhea uwanja na Thierry Henry katika awamu ya kwanza

Hapa ni baada ya kwenda kumsalimu golikipa wa Edwin Van Persie.

Hapa ni baada ya kuwafunga mabao mawili Chelsea kwenye uwanja Stamford Bridge.

Hapa ni baada ya kufungwa na Bolton kwenye mchezo wa fainali.

Kadi yake nyekundu aliyopewa kwa maamuzi ya utata dhidi ya Barcelona.

Akiombwa asiondoke

Akiwafunga mahasimu wao wakubwa Tottenham

Akishangilia magoli yake mawili aliyoyafunga dhidi ya Chelsea kwenye uwanja


Hapa ndipo Majeruhi yalipoanza kushikakasi

Siku ya mwisho aliyoyafanya mazoezi  na Arsenal huko Ujerumani.